Mswada wa sheria ya kuunda Baraza la Usalama wa Taifa wakataliwa!

teh teh ..kazi kweli kweli...niliona dalili mwanzoni wakati anatoa summary ya muswadda nikajua leo kazi ipo
 
Kilicho nishangaza zaidi leo ni Naib Spika pamoja na Dr. Slaa kuomba kuahirishwa mjadala kwa mujibu wa kanuni za bunge hakuchukua hatua ya kulihoji bunge mpaka Malechela kasema bila kutaja kanuni kamwita mtoa hoja Simba na kumnyima nafasi Hamad Rashid ili kuibeba hoja iwe ya CCM. Aibu tunahitaji spika asiwe mkereketwa wa chama kama Anna
 
teh teh ..kazi kweli kweli...niliona dalili mwanzoni wakati anatoa summary ya muswadda nikajua leo kazi ipo
haahaaah...mkuu ungemshitua kwamba inaweza kula kwake maana rejection ya aina hiyo ni ya kihistoria. 100% rejection!
 
Mh. Simba amshukuru sana Prof. Mwandosya leo aliyekua kiongozi wa shughuli za serekali bungeni vinginevyo angeaaibika zaidi. Naambiwa Simba ni mwanasheria wa Mlimani kweli ? nisaidieni napata hofu sasa na digrii za Mlimani
 
Kilicho nishangaza zaidi leo ni Naib Spika pamoja na Dr. Slaa kuomba kuahirishwa mjadala kwa mujibu wa kanuni za bunge hakuchukua hatua ya kulihoji bunge mpaka Malechela kasema bila kutaja kanuni kamwita mtoa hoja Simba na kumnyima nafasi Hamad Rashid ili kuibeba hoja iwe ya CCM. Aibu tunahitaji spika asiwe mkereketwa wa chama kama Anna

Wakati fulani speaker anahitaji atumie common sense. Suala lilikwishaonekana limeoza!! Kuendelea kulijadili nikupoteza muda. Mh Mbunge mmoja tu wa Nkasi, ndiye aliyeunga hoja mkono. Hapo unataka waendele kujadili nini tena.

kanuni zilikuwa wazi kabisa!! Hapo siyo suala la ukereketwa. Mh Slaa alikwishaongea, CHADEMA, na Mh Malecela, kaunga maelezo ya Dr Slaa. Nini tena unataka? Kambi ya upinzani siyo CUF tu, kama wewe ni mwana CUF!!. Leta hoja siyo majungu!
 
- Mleta mada bado hii mada kueleweka, vipi unaweza ukairekebisha kidogo maana wengi tunashindwa kuelewa kilichojiri hasa na the ishu, au?

Respect.

FMEs!
 
Ni nani asiyefahamu kwamba Sophia Simba, hakuna kitu pale???. JK anapenda wanaouza sura na wanja bungeni, ndiyo maana anawateuua kushika viti maalumu. Ipo siku, vitimaalumu vitachakaa tuvitupie jalalani.
 
Ingawa sijaielewa mswada ulihusu nini hasa mpaka waziri akatoa mapendekezo ya kuundwa kamati za usalama wa taifa,ninavyolifahamu bunge letu la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,haitachukua muda mrefu kabla hujasikia mapendekezo na muswada husika umepita bila kupingwa,kwa uzoefu tu ni kwamba walewale wabunge wanaosema napinga hoja fulani kwa sababu kadha wa kadha,mwisho wa siku utasikia naunga mkono hoja kwa asilimia 100.Inasikitisha sana!!
 
Huyu mama sasa anaonyesha asivyo makini. Mambo ya usalama wa taifa
Anajipangia kama kitchen party! Umakini 0. Hao wataalamu wake nao 0 tu.
 
Mkuu, muswada wenyewe ulihusu nini hasa, labda tukifahamu itasaidia kujua kama alitendewa haki kupondwa au la, si unajua tena bongo siasa za visasi?

Ulikuwa mswbda wa baraza la usalama wa taifa na yeye ndie mtoa hoja ktk wizara yake.
 
Hold on!

Mama ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais; kwa maana nyingine hii ni Ikulu, ama sio waungwana?
Miswada kama hii ni lazima iridhiziwe na baraza la mawaziri kabla ya kupeleka bungeni si ndio waungwana?
Kwa hiyo kutokuwa makini kwenye jambo zito kama hii kunaashiria nini?
Au hata kashifa ya kugawa land rover kumbe ilikuwa business as usual?
 
Kuna details zozote za kwa nini umekataliwa, nani kaukataaa na ametumia vigezo gani?

Mwaka wa uchaguzi huu, sintoshangaa nikiambiwa kuna Meremeta nyingine inaandaliwa chini yakivuli cha usalama wa taifa.
 
Pale Uhuru Road (formely Kitchwele St), kama unaenda Buguruni, ukipita Ilala magorofa ya NHC, kuna vi bar bar kibao wanapiga taarab kwa sana (at least back then).

Katika nchi inayofuata meritocracy Sophia Simba alitakiwa kuwa pale, huko bungeni isingewezekana kabisa.

Hivi huyu mama kachaguliwa au ni special seats za CCM ?
 
- Mleta mada bado hii mada kueleweka, vipi unaweza ukairekebisha kidogo maana wengi tunashindwa kuelewa kilichojiri hasa na the ishu, au?

Respect.

FMEs!

Kiujumla muswada ulikuwa na nia ya kuipa madaraka ya juu sana kamati ya usalama wa taifa, swali ni je nani zaidi kati yao na usalama wa taifa? Je usalama wa taifa umeshindwa kazi na huu muswada ulikuwa na nia ya kuwapiga chini usalama wa taifa au kutafuta alternative?

Kuna tatizo kubwa sana kwenye institutional framework hapa Tanzania, who is who, dong what, when, why, how. Kila mmoja wetu anapenda kuwa bosi au kuonekana mwenye mamlaka zaidi ya mwenzio, siku mambo gongana, hakuna wa kuwajibishwa wala kuwajibika, inabaki kurushiana mpira.
 
Wazee
Niliutazama mjadala tangu mwanzo hadi mwisho. Niseme machache:
-Kwanza, nilishangaa kwa nini mjadala huo uliletwa na kamati ya Lubeleje badala ya kamati ya Masilingi inayohusika na mambo ya usalama na mambo ya nje. Uvumi ni kuwa serikali inamwona Lubeleje kuwa ni uchochoro wa kupitishia mambo yenye utata, na yeye huyachukulia kama msahafu.
-Dhana ya kupunguza madaraka ya Rais ni nzuri lakini si katika mambo ya ulinzi na usalama. Muswada ulikosea kuweka dhana ya kupiga kura katika baraza linalopendekezwa, kwa sababu, idadi ya baraza ni ndogo inayoweza kununuliwa na kuinfluence maamuzi.
-Ni wazi, Sophia, Werema na Lubeleje wameonyesha kukosa umakini, si katika hoja, bali hata katika drafting na kukosekana kwa sensitivity. Of course hili pia ni pigo kwa idara nzima ya usalama, kwamba waliacha kitu kama hiki kiende mbele. Ni aibu kwa baraza la mawaziri lililopitisha muswada huu uende bungeni.

Mwisho naomba kuwauliza wanasheria: Hivi hakuna constitutional implications za kukataliwa kwa muswada bungeni? Hii si dalili ya kukosa imani na Rais?
 
Siamini kama JF mpaka sasa imeshindwa kupata Muswada na kuuweka hapa tuujadili! Nilikuwa naamini kuwa Mzee Mwanakijiji huwa hashindwi kupata documents na kuzibandika, watu wakaendelea kumwaga mambo wakiwa na uhakika wa kile wanachojadili, lakini sasa mmmmh!
 
Siamini kama JF mpaka sasa imeshindwa kupata Muswada na kuuweka hapa tuujadili! Nilikuwa naamini kuwa Mzee Mwanakijiji huwa hashindwi kupata documents na kuzibandika, watu wakaendelea kumwaga mambo wakiwa na uhakika wa kile wanachojadili, lakini sasa mmmmh!


ushawahi kuona ndege anakula mpunga wako hadi punje ya mwisho na mtego ukabakia pale pale; kuna ndege wengine hawategeki.
 
Back
Top Bottom