Mswaada wa maslahi ya vigogo wapingwa tena

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by amini // 19/01/2012 // Habari // No comments

jussa-564x272.jpg
Posted on January 18, 2012 by zanzibaryetu
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akiongea na Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee
Mswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa serikali wastaafu ambao umewasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi umepata pigo baada ya wajumbe waliochangia kuukata na kusema haulengi kuweka usawa wa maslahi ya wananchi walio wengi. Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akichangia mswada huo alisema kwamba umekuja katika wakati ambao haustahiki kwa sababu wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku huduma mbali mbali za maendeleo zikiwa duni.
‘Leo tunaleta mswaada huu wakati wananchi wetu wanaishi katika maisha duni sijuwi kama watatuelewa….elimu ipo duni huku mahitaji ya hospitali katika chumba cha wagojwa mahututi (ICU) yakiwa katika mazingira magumu’ alisema Jussa. Alisema yeye binafsi ataupinga mswaada huo kwa sababu haujakidhi mahitaji ya wakati huku huduma za maendeleo zikiwa bado haziridhishi hata kidogo.
Mwakilishi huyo alisema ni vizuri kuwatunza viongozi wastaafu ambao wameleta mchango mkubwa kwa taifa hili kutokana na uongozi busara na hekima zao. Lakini alisema huu si wakati muafaka wa kuwasilisha mswaada huo kwani wananchi wengi matarajio yao katika serikali ya umoja wa kitaifa kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi na maisha ambayo hayajafikiwa kwa sasa.
Awali Mwakilishi wa jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif alisema yeye haungi mkono mswaada huo kwa sababu umelenga zaidi katika kuimarisha hali za viongozi wastaafu wa kisiasa na huku watumishi wa umma wanaostaafu wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Alisema ni jambo la busara kuwapatia mafao wastaafu ambao mchango wao kwa taifa ni mkubwa lakini zaidi ilipaswa kuangaliwa hali ya uchumi wa visiwa vya Zanzibar na muelekeo wa uchumi.
‘Hivi sasa tunashindwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo skuli pamoja na kujenga hospitali bora kwa sababu hatuna fedha za kutosha….kwa nini tunataka kutumia fedha nyingi kuwalipa mafao wastaafu pamoja na familia zao?’alihoji Mwakilishi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini aliwasilisha mswaada wa mafao ya viongozi wastaafu ikiwa unaletwa hapo kwa mara ya pili.
Dk Mwinyihaji aliwaambiya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba mswada huo umefanyiwa marekebisho makubwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya viongozi hao ambapo sasa tafsiri ya viongozi wa kisiasa imepanuliwa zaidi ambapo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameingizwa katika mswaada huo.
 
Kazi ipo barzani mwaka huu. Nasikia mambo yalikuwa hot sana.

Tuombe kheir
 
Nchi za watu hizo bana. Watajua wenyewe; hata wauze visiwa walipane, shauri yao.
 
Back
Top Bottom