Msuya: Sijui kwa nini tuilipe DOWANS!

MZEE MSUYA MGOMBEA MZURI CCM 2015 HATA AWE MAGUFULI' NI SERA AU SURA KAMA KAWAIDA??

Mzee Msuya mgombea mzuri Tanzania hafikiriki tena nchi hii bila kwanza wananchi tukajiandikie katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Inasikitisha sana kwamba hadi hapa umekiri kwamba Watanzania kwa sasa hatuna rais mzuri nakutupendekezea tuvumilie hivo hivo mpaka tufike huko kwenye 'Tanzania nchi yako ya ahadi 2015'. Hili pendekezo halikubaliki leo wala kesho, hatudanganyiki!!!

Kwa kweli masikini kwa kutunza kumbukumbu za mashaibu yake, duniani nkote katika zoezi la kupima kama kweli ni mtu mwenye kuaminika kauli au hapana, mtu usipime! Watanzania tukigeuka kidogo nyuma kidogo katika historia, ahadi za Mzee Msuya (with due respect) ni sawa tu na mvuke kwenye pishi la makande bila maharage kule vijijini.

Kwa uchungu mkubwa Watanzania bado tunakumbuka sana tu Mzee Msuya akiwa Waziri wa Fedha wa nchii hii, wakati wa shida kubwa na misukosuko, aliwahi kuwatupia virago Watanzania walalahoi virago kwa kuwapandishia kodi kuongeza umasikini kila kona huku akikejeli kwamba shauri yao 'KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE'. Kila akijitokeza na bajeti ni kuwaacha walalahoi wakipumulia tu mashine huku kila chema akijinyakulia kwenda kijijini kwao!!

Kwa kweli huu usemi wa kimasimango wa Mzee Msuya uligeuka dondadugu kwenye ilikua ni simanzi wakati wote kwa wananchi wengi wenye kuishi kwa mlo mmoja tu kwa siku na wala haikupata kusamehewa hadi leo hii. Mwaka wa 1995 alipojitokeza miongoni mwa watu wengine 15 wakiomba kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, walalahoi Tanzania waliibuka baada ya miaka mingi na kusema kwamba hata kabla mchakato haujaanza, Freddy Msuya akipewa tiketi hiyo kugombea basi na yeye pia AJIANDAE KUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE kwa kuwa walionelea kwamba zamu ya naye iliwadia.

Kama dalili za SIASA ZA UBINAFSI NA UCHOYO HAUKUA KITU KWA WATANZANIA basi mzee Msuya alikuja akawafikia watu pomoni kwa jitihada zake za kugeuza vijiji vyote vya jimboni kwake na vingine vingi vya majimbo ya jirani kuwa kama Ulaya. Je, ni rais mzuri wa aina gani ambayo Mzee Msuya anaweza akatuletea ndani ya udwara ule ule wa CCM ufisadi kwa mtaji wa background ya aina hii.

Hili tatizo la umeme kuzimazima mzee wetu huistikia tu pindi anapoingia jijini Dar. Kote kule Upareni mlimani ni taa kila kona na barabara za lami hadi kwenye nyumba za mbavu ya mbwa ambazo kwa kweli ni za nadra mno kuonekana huko siku hizi. Kwa lugha nyingine walioifikisha Tanzania yetu hapa tulipo Waziri Mkuu wa zamani katika nyakwa nyakwa habaki nyuma.

Hivyo, kama mtu yeyote bado anayo malengo kwa mazuri kwa Watanzania izidiyo thamani ya ZAWADI YA BIRTHDAY KUTOKA KWA MHE KIKWETE NA MZEE MWINYI kuja kuwapigia udalali wa kutupooza wananchi kurudio ule ule usingizi wa pono huku nchi ikitafunwa na wenye meno.

Kwa kweli ni sharti kwanza Mzee Msuya akamalizane kwanza kukamilisha ndoto yetu wananchi kujiandikia upya katiba jinsi gani tungependa kutawaliwa siku za usoni, kuweka tume huru ya uchaguzi kabla ya kitu chochote 2015. Kama anaweza akawaelimishe CCM kuhusu umuhimu wa bunge kulianzinsha mara moja mchakato ifikapo mwezi wa pili mwaka huu.

Ucheleweshaji wowote wa zoezi la mabadiliko ya kweli VIJANA NA MACHALII kibao hatutayavumilia tena kwa mtu yeyote kuingiza utani na janja za nyani. Aheri kufa kishujaa uwanjani kwa hili kama Ismail na Denis kuliko kuendelea kuishi kwa aibu kubwa hii na kudhalilika kila kukicha kimaisha. Kwanza makali ya maisha kwetu hayawezi kuvumilia ahadi za hadi 2015 hizo, maisha ni sasa hivi, tuishi sote na nyinyi waungwana au hapana kwa sote kwa ujumla wake!!

Tofauti na hapo tusiendelee kutakiana ubaya kwa kuandaa karamu kubwa zaidi kuliko zile za Pemba, Arusha na Mbarali Mbeya.
 
CCM wao huwa wanafikiri kushinda tu,hawana jipya na wala hawajui ukishashinda unatakiwa kuwafanyia nini waliokushindisha.Wala ccm na Msuya wasijisumbue tena,ushindi upo dhahiri mrengo wa kushoto na wakichakachua wote tunaingia barabarani.Hatununui sura wala kushindanisha sura hapa.
 
Back
Top Bottom