Msuya: Sijui kwa nini tuilipe DOWANS!

Jamaa yuko vizuri siku akimua! Kuna siku aliandika hisia zake na kero za umeme wa mgao bila kuweka jazba zake za kidini wala UCCM aliandika kwa machungu kwa maslahi ya taifa. Leo tena amekuja na article nzuri ingawa ni copy and paste ya gazetini. Kudos SokoMoko. Kuna shida kwenye serikali ya Kikwete ameona aibu Msuya kuweka wazi kuwa jamaa wa kikwere anavurunda.

Dogo una maana gani kwenye hiyo bold? udini ni nini? hivi kikiwa na mgao wa dini gani wanataabika na wa dini ipi wanapeta? na ugumu wa maisha je? vipi kuhusu CCM wao hawakatili umeme na wanaishi sayari nyingine sio hii tunayoishi sote hawaishi TZ? Maana wewe mwenzetu haupo TZ na wala hujui kunguni wake wakoje unasimuliwa tu rudi uyaone halafu tuone kama utajadili dini hapa.
 
Tunataka Proof Ndugu.....dhambi yake pekee labda kupendelea maendeleo kwao MWANGA...hilo la uhujumu la kwako peke yako
Ni upendeleo gani wa maendeleo alipeleka huko kwao Mwanga? Alijenga shule nyingi, Hospital au alisambaza maji kila sehemu? Usikute tunaongelea Wapare kujitaidi kupata mikopo bank na kununua "chai maharage" tuna muhusisha Msuya kwasababu alikuwa waziri.
 
Nadhani Bw. Msuya ana haki kama raia kutoa maoni yake, lakini lazima tuyapime.

Ukipima kwa haraka waona wazi kuwa hayakuwa maoni sahihi. Kwanza hajafanyiwa uchunguzi au tuseme hana taarifa kamili na sahihi. Pili hakuweza kupata balance ya ripoti au maoni yake hivyo ameegemea alikotoka - CCM.

Mzee Msuya, itakuwa ngumu sana bila kuwa na ukweli na taswira halisi ya Tz ya sasa, hutaweza kuwashawishi WaTz wa leo. Ungelifanyia kazi kidogo hilo la kufuata utawala wa sheria kisha utoe maoni. Unaweza wenda kwenye maktaba (domains) utapata hali halisi kwa kupitia na kcuhambua kesi mbalimbali mle.

Hitimisho: Tz hakuna utawala wa sheria, ila tu sheria ya utawala.
 
Nilikutana na hii nikacheka sana.
MZEE MSUYA UMENENA VEMA YAFUATAYO. 1. TATIZO LA OMBWE LA UONGOZI WA TAZANIA WA RAIS KIKWETE. 2. KUTOKUWA NIA YOYOTE YA KUPIGA VITA RUSHWA KWA SERIKALI YA SASA ZAIDI YA VIONGOZI KUJINUFAISHA KIBINAFSI NA KUTETEANA WAO KIFAMILIA NA KIRAFIKI. 3. UMUHIMU WA KATIBA MPYA NA TUME YA RAIS KUSHIRIKISHA WAPINZANI (4) TUWE NA VIWANDA TANZANIA (5) FAGIO LA CHUMA LIPITE CCM KUSAFISHA NJIA (6) DOWANS KUTOSTAHILI MALIPO. YA NINI? (7) NCHI KUKOSA DIRA YA MAENDELEO (8) KIKOSEKANA VIONGOZI WAZALENDO KAMA KINA SITTA, MEAKYEMBE, NK (8) SIASA ZA NCHI KUINGILIWA WA WATU WACHAFU KAMA KINA RA,EL NK (8)UMENENA VEMA KWAMBA HUKUTAKA KULAZIMISHA WANAO KUINGIA SIASA MAANA KUWATUMIKIA WATU NI WITO. HAWA KINA JI (RZ1) WAO NI DILI. (9)WASIWASI WA AHADI HEWA ZA VIONGOZO WA CCA HASA JK, KWAMBA VIJANA WANACHUKIA SANA, SSA WAKIPATA MTU WA KUWAELIMISHA WANAGEUKA KABISA AGAINST CCM. (10) KWAMBA BADO UNA TUMAINI LA RAIS TOKA CCM (11) KWAMBA CCM IMEPOTEZA UBUNGE CONTROL YA ALL THE ECONOMIC AND POLITICAL STRATEGIC AREAS KAMA DSM, MWANZA,ARUSHA, MBEYA, IRINGA, KIGOMA, NK. NI KOSA LA KUWA NA KATIBU MKUU M[NENO BAYA] KAMA MAKAMBA NA RAIS/MWENYEKITI WA CCM MBABAISHAJI KAMA JK. PIA UONGOZI WA WAZEE WALIOISHA KAMA KINA MSEKWA, VIONGOZI WAPU-UZI KAMA KINA CHITANDA, MASHA, BURIANI NK.
AMBACHO HUKUSEMA NI KWAMBA (1) UNAWAGANDAMIZA CHADEMA KWA SABABU TU YA UTAWALA WA SHERIA. UTAWALA WA SHERIA PIA UNARUHUSU MAANDAMANO YA AMANI. (2) ULIKUWA KIONGOZI MBAGUZI, HASA KUWABAGUA WAPARE YA KUSINI (3) ULIKUWA KINARA WA MVURUGANO KATIKA DAYOSISI YA KKKT PARE UKITAKA DAYOSISI YA MWANGA YAKO NA SAME KATIKA AGENDA YAKO YA KUWABAGUA WAPARE WA KUSINI (4) KWAMBA WAZIRI DAVID MATHAYO NI MWANAO ULIYEMZAA PARE KUSINI UKIWA OFISA UTUMISHI KULE, NDIO MAAN BARAZA LA MAWAZIRI UNALIPENDA (5) ULIJITAHIDI SANA KUMPIGA VITA WAZIRI MAGHEMBE KATIKA UBUNGE WA MWANGA ILI UPATE UHAKIKA WA MWANAO DAVID KUPATA UWAZIRI KUPITIA UPARE. (6) WEWE NI MMOJA WA VIONGOZI WAKATILI TANZANIA HII, HAIJAPATA KUTOKEA. UNANIELEWA NADHANI. (7) KASORO HIZI MUNGU AKUSAMEHE HATA WEWE NI MWANADAMU. JIPIME MWENYEWE.
 
..yeye aeleze uhalali wa wananchi wale kuuwawa na kuumizwa.

..kama hawezi kulitetea hilo basi akae kimya.

..je, kuuwa na kuumiza waandamanaji ni kufuata utawala wa sheria?
 
Kwa sisi waelewa neno"RULE OF LAW" ukilichunguza kiundani zaidi lina element za authoritarianism.B'coz hata SOUTH Africa kipindi cha makaburu walikuwa wanaendeshwa na rule of law"APATHEID POLICY-the law of Racism.
Therefore Msuya haitakiwi aamini kuwa CDM kiheshimu utawala wa sheria wakati Utawala huo upo umekuwa ni fimbo ya makafiri,wadhulumaji,wauaji,waasi,wanajisi CCM kuadhibu yeyote anayejitokeza kudai Haki.
Swala hapa ni,EQUALITY B4 THE LAW then tuone kama hawa wezi(CCM) watapona mkono wa sheria.
CCM wana Phd ya Wizi,Ukipeleka kesi Mahakamani ndio kwanza watamchakachua huyo hakimu na mawakili kwa ujumla.Swala ni maandamano ili tuiangushe hii serikali Kaidi na gaidi,Tena Mataifa yasikie kilio cha wtz.
 
Waliosoma TANZANIA DAIMA ya jana wanakumbuka jinsi mwandishi Absalom Kibada alivyoandika makala ndefu akimponda Samwel Sitta kuhusu matamshi yake kuwa uamuzi wa kuilipa DOWANS haukupita kwenye Baraza la Mawaziri.

Sina haja ya kuirudia makala yote ile lakini msingi mkuu wa Bwana Kibanda ulikuwa ni kwamba Sitta amekosa nidhamu ya uwajbikaji wa pamoja yaani collectve responsibility.

Kwamba Sitta amekosea kwa kuvujisha siri za Baraza la Mawaziri na hakutakiwa kwenda kinyume na baraza hilo.
Kibanda alizidi kujenga dhana yake kwamba ameshukuru siri iliyotobolewa juzijuzi na Cleopa Msuya kwamba yeye kama

Waziri Mkuu mwaka 1995 alimshauri Rais Mwinyi kumfukuza kaz Augustine Mrema alipotoa siri za Baraza la Mawaziri na kukiuka uwajibikaji wa pamoja.

Hivyo Kibanda amejenga hoja yake kwamba kinachomweka Sitta sasa hivi ni bahati kwa sababu nchi haina Waziri Mkuu kama Msuya vinginevyo ilibidi afukuzwe kazi kama alivyofukuzwa Mrema wakati ule.

Leo walichofanya gazeti la MWANANCHI n kumhoji moja kwa moja Cleopa Msuya kuhusu sakata hili la DOWANS. Mahojiano yale na habari hii tayari kuna thread yake humu JF.

Hivyo sikirudii sana alichosema Msuya lakini tumesoma ambapo Msuya mwenyewe anasema haoni kwa nini DOWANS walipwe.

Msuya amewekeza imani yake kwa Samwel Sitta kwamba ndiye aliyeshughulikia suala la kampuni hewa ya RICHMOD bungeni hivyo kwenye baraza la mawaziri ni lazima angekuwa na taarifa za kutosha kushughulikia hoja hiyo.

Kwa kuwa tuna kauli ya Msuya mwenyewe basi hili ni anguko jingine kwa Absalom Kibanda kama ambavyo wenzetu wengine waliwahi kuhoji uandishi wake kwa muda wa miezi sita sasa.

Nawasilisha.

Source:
1: Mwananchi (ya leo):

http://www.mwananchi.co.tz/componen...8359-msuya-sijui-kwa-nini-tuilipe-dowans.html

2: Tanzania Daima (ya jana)
 
Waliosoma TANZANIA DAIMA ya juzi wanakumbuka jinsi mwandishi Absalom Kibada alivyoandika makala ndefu akimponda Samwel Sitta kuhusu matamshi yake kuwa uamuzi wa kuilipa DOWANS haukupita kwenye Baraza la Mawaziri.

Sina haja ya kuirudia makala yote ile lakini msingi mkuu wa Bwana Kibanda ulikuwa ni kwamba Sitta amekosa nidhamu ya uwajbikaji wa pamoja yaani collectve responsibility.

Kwamba Sitta amekosea kwa kuvujisha siri za Baraza la Mawaziri na hakutakiwa kwenda kinyume na baraza hilo.

Kibanda alizidi kujenga dhana yake kwamba ameshukuru siri iliyotobolewa juzijuzi na Cleopa Msuya kwamba yeye kama Waziri Mkuu mwaka 1995 alimshauri Rais Mwinyi kumfukuza kaz Augustine Mrema alipotoa siri za Baraza la Mawaziri na kukiuka uwajibikaji wa pamoja.

Hivyo Kibanda amejenga hoja yake kwamba kinachomweka Sitta sasa hivi ni bahati kwa sababu nchi haina Waziri Mkuu kama Msuya vinginevyo ilibidi afukuzwe kazi kama alivyofukuzwa Mrema wakati ule.

Leo walichofanya gazeti la MWANANCHI n kumhoji moja kwa moja Cleopa Msuya kuhusu sakata hili la DOWANS. Mahojiano yale na habari hii tayari kuna thread yake humu JF.

Hivyo sikirudii sana alichosema Msuya lakini tumesoma ambapo Msuya mwenyewe anasema haoni kwa nini DOWANS walipwe.

Msuya amewekeza imani yake kwa Samwel Sitta kwamba ndiye aliyeshughulikia suala la kampuni hewa ya RICHMOD bungeni hivyo kwenye baraza la mawaziri ni lazima angekuwa na taarifa za kutosha kushughulikia hoja hiyo.

Kwa kuwa sasa tuna kauli ya Msuya mwenyewe basi hili ni anguko jingine kwa Absalom Kibanda kama ambavyo wenzetu wengine waliwahi kuhoji uandishi wake kwa muda wa miezi sita sasa.

Nawasilisha.

Source:
1: Mwananchi (ya leo):

http://www.mwananchi.co.tz/componen...8359-msuya-sijui-kwa-nini-tuilipe-dowans.html

2: Tanzania Daima (ya juzi)
 
Ramadhan Semtawa
WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amezungumzia sakata la Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura ya Dowans akieleza kuwa mpaka sasa hafahamu kwa nini Tanzania inapaswa kuilipa fidia kampuni hiyo ya kigeni inayodaiwa kuingia nchini kitapeli.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake
Upanga jijini Dar es Salaam, Msuya alisema anaamini hata Watanzania wengine, watakuwa wanajiuliza swali hilo.

"Wakati mwingine nashindwa hata kuzungumzia suala hili kwa sababu hadi sasa, sijui Dowans wanapaswa kulipwa kwanini. Naaamini si mimi tu ninayejiuliza swali hili, hata Watanzania wengine wengi hawajui kwanini Serikali inapaswa kuilipa Dowans," alisema Msuya.

Msuya alieleza kuwa kama suala la malipo hayo limefikiwa bila idhini ya Baraza la Mawaziri kama inavyodaiwa, hapa kuna tatizo kubwa linalopaswa kuangaliwa kwa makini zaidi.

"Kama ni kweli maana sina hakika, jambo hilo halijapita katika Baraza la Mawaziri, kutakuwa na tatizo kubwa. Kwa sababu jambo kubwa kama hilo lilipaswa lipitishwe huko liamuliwe na Serikali nzima si mtu mmoja kuamua," alisisitiza.

Msuya ameungana na mawazo ya Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta aliyetaka kampuni hiyo isilipwe kwa kile alichoeleza kuwa anamwamini Sitta kwa mambo mawili; ni mwanasheria makini na ni mtu aliyelishughulikia sakata la Richmond tangu akiwa Spika wa Bunge la Tisa.

"Inawezekana Samuel Sitta analijua vizuri sana jambo hili, kwanza kitaaluma ni mwanasheria, lakini pia, yeye ndiye alilishughulikia suala hilo akiwa spika bungeni. Hivyo nadhani kuna umuhimu wa jambo hilo kuangaliwa kwa makini sana," alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Msuya amezungumzia mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi nchini na kueleza kuwa siasa nchini, imevamiwa na watu wasiokuwa waadilifu na wito wa kutumikia taifa na kutoa wito kwa mamlaka husika kutowavumilia watu hao.
 
Hoja za 6 ni kuntu na wazi! Tatizo mafisadi hawataki kushindwa ingawa ukweli wanaujua. Wako karibu kuumbuka. Hongera 6, hongera msuya, hongera watanzania. Aruta cont...
 
"Kwa hiyo uchaguzi wa mwaka 2015 haunipi wasiwasi sana, najua CCM ni chama makini, kitakaa na kujitathimini kilikosea wapi na vipi ijirekebishe. Changamoto ni hii iliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambazo ndizo tunapaswa kuziangalia na kutoka na mikakati ya kwenda mbele," alirejea kipigo hicho cha 2010 ambacho kilipunguza hadi kura za urais za Kikwete kutoka asilimia 80 hadi 61.

Alitamba pia, chama hicho kina uhakika wa kupata mgombea bora wa urais kwa mwaka 2015 ambaye anatarajiwa kukubalika vema kwa wananchi wa Watanzania wakati uchaguzi ukiwadia.
 
maana ya ujumbe wa Mzee Msuya ni kuwa "haelewi kwa nini CCM imeshinda 2010 wakati haikuwa na wagombea wanaofaa" hii anaanzia juu hadi chini....cijui na mwanaye yumo lakini ni msg muhimu kuwa "yeye na kundi lake hawaoni kama mkulu anaweza nchi? na ndio maana amesema nchi haina utwawala tena wa sheria?
 
Tunataka Proof Ndugu.....dhambi yake pekee labda kupendelea maendeleo kwao MWANGA...hilo la uhujumu la kwako peke yako


Kasome historia ya mapambano ya uhujumu uchumi chini ya Ed Moringe Sokoine. Usitake kuletewa kila kitu hapa JF
 
Nafurahi ameona kuna tatizo na kuna haja ya kujirekebisha.............kuna watu hawaoni??
 
MZEE MSUYA MGOMBEA MZURI CCM 2015 HATA AWE MAGUFULI' NI SERA AU SURA KAMA KAWAIDA??

Hivi ni kitu gani ambacho CCM inatarajia zaidi kutendea bora zaidi kwa mwaka wa 2015 bila KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI ambayo kipindi chote cha miaka 50 hawakuiweza hawakukiweza kwa kutumia Katiba ya kikoloni hii tulionayo???

Mzee Msuya mgombea mzuri Tanzania hafikiriki tena nchi hii bila kwanza wananchi tukajiandikie katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Hakika inasikitisha sana kwamba hadi hapa umekiri kwamba Watanzania kwa sasa hatuna rais mzuri nakutupendekezea tuvumilie hivo hivo mpaka tufike huko kwenye 'Tanzania nchi yako ya ahadi 2015'. Hili pendekezo halikubaliki leo wala kesho, hatudanganyiki!!!


Kwa kweli masikini kwa kutunza kumbukumbu za mashaibu yake, duniani nkote katika zoezi la kupima kama kweli ni mtu mwenye kuaminika kauli au hapana, mtu usipime! Watanzania tukigeuka kidogo nyuma kidogo katika historia, ahadi za Mzee Msuya (with due respect) ni sawa tu na mvuke kwenye pishi la makande bila maharage kule vijijini.


Kwa uchungu mkubwa Watanzania bado tunakumbuka sana tu Mzee Msuya akiwa Waziri wa Fedha wa nchii hii, wakati wa shida kubwa na misukosuko, aliwahi kuwatupia virago Watanzania walalahoi virago kwa kuwapandishia kodi kuongeza umasikini kila kona huku akikejeli kwamba shauri yao 'KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE'. Kila akijitokeza na bajeti ni kuwaacha walalahoi wakipumulia tu mashine huku kila chema akijinyakulia kwenda kijijini kwao!!


Kwa kweli huu usemi wa kimasimango wa Mzee Msuya uligeuka dondadugu kwenye ilikua ni simanzi wakati wote kwa wananchi wengi wenye kuishi kwa mlo mmoja tu kwa siku na wala haikupata kusamehewa hadi leo hii.

Mwaka wa 1995 alipojitokeza miongoni mwa watu wengine 15 wakiomba kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, walalahoi Tanzania waliibuka baada ya miaka mingi na kusema kwamba hata kabla mchakato haujaanza, Freddy Msuya akipewa tiketi hiyo kugombea basi na yeye pia AJIANDAE KUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE kwa kuwa walionelea kwamba zamu ya naye iliwadia.


Kama dalili za SIASA ZA UBINAFSI NA UCHOYO HAUKUA KITU KWA WATANZANIA basi mzee Msuya alikuja akawafikia watu pomoni kwa jitihada zake za kugeuza vijiji vyote vya jimboni kwake na vingine vingi vya majimbo ya jirani kuwa kama Ulaya.

Je, ni rais mzuri wa aina gani ambayo Mzee Msuya anaweza akatuletea ndani ya udwara ule ule wa CCM ufisadi kwa mtaji wa background ya aina hii.


Hili tatizo la umeme kuzimazima mzee wetu huistikia tu pindi anapoingia jijini Dar. Kote kule Upareni mlimani ni taa kila kona na barabara za lami hadi kwenye nyumba za mbavu ya mbwa ambazo kwa kweli ni za nadra mno kuonekana huko siku hizi. Kwa lugha nyingine walioifikisha Tanzania yetu hapa tulipo Waziri Mkuu wa zamani katika nyakwa nyakwa habaki nyuma.


Hivyo, kama mtu yeyote bado anayo malengo kwa mazuri kwa Watanzania izidiyo thamani ya ZAWADI YA BIRTHDAY KUTOKA KWA MHE KIKWETE NA MZEE MWINYI kuja kuwapigia udalali wa kutupooza wananchi kurudio ule ule usingizi wa pono huku nchi ikitafunwa na wenye meno.


Kwa kweli ni sharti kwanza Mzee Msuya akamalizane kwanza kukamilisha ndoto yetu wananchi kujiandikia upya katiba jinsi gani tungependa kutawaliwa siku za usoni, kuweka tume huru ya uchaguzi kabla ya kitu chochote 2015.

Kama anaweza akawaelimishe CCM kuhusu umuhimu wa bunge kulianzinsha mara moja mchakato ifikapo mwezi wa pili mwaka huu.


Ucheleweshaji wowote wa zoezi la mabadiliko ya kweli VIJANA NA MACHALII kibao hatutayavumilia tena kwa mtu yeyote kuingiza utani na janja za nyani.

Wazee wetu wa CCM ya miaka ya 47, kwetu sisi vijana wa leo hii tunaonelea kwamba ni aheri kufa kishujaa uwanjani kwa hili kama Ismail na Denis kuliko kuendelea kuishi kwa aibu kubwa hii na kudhalilika kila kukicha kimaisha.

Kwanza makali ya maisha kwetu hayawezi kuvumilia ahadi za hadi 2015 hizo, maisha ni sasa hivi, tuishi sote na nyinyi waungwana au hapana kwa sote kwa ujumla wake!!


Tofauti na hapo tusiendelee kutakiana ubaya kwa kuandaa karamu kubwa zaidi kuliko zile za Pemba, Arusha na Mbarali Mbeya.
 
Back
Top Bottom