...Msuya atupa mzigo kwa Mkapa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
...Msuya atupa mzigo kwa Mkapa

*Asema ndiye ametufikisha tulipo

Na Godfrey Ismaely
Majira

MAKAMU wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya awamu ya Kwanza Bw. Cleopa Msuya ameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kutosha juu ya viongozi wanaovuliwa au kujivua gamba wenyewe ili wakibainika kwamba walijipatia mali walizonazo kinyume na taratibu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Mwito huo aliutoa jana nyumbani kwake Dar es Salaam, wakati akifanya mahojiano maalum na Majira lengo likiwa ni kufahamu hatima na mwelekeo wa Taifa na tathimini yake juu ya mwenendo wa mambo ya siasa likiwamo suala la upatikanaji wa nishati ya umeme ambalo kwa sasa limeonekana kuwa kero kwa uchumi na hata uzalishaji.

"Lazima kila mmoja awajibike katika kutoa ufafanuzi awe amevuliwa au amejivua gamba mwenyewe kwa kuwa sisi wananchi tunachoitaji zaidi ni kuona hatua za kisheria zinachukuliwa dhidhi yao na ikiwezekana wawajibishwe," alisema Bw. Msuya na kuongeza.

"Zingatia kuna hatua za aina mbili ambazo zinaweza kuzaa matunda kwanza ni juu ya Chama kuwachukulia hatua za kuwapima watendaji wake na hata viongozi wanaotuhumiwa na vitendo vya ubadirifu kwa kuwavua wote madarakani.Hatua ya pili ni serikali kupitia vyombo vya dola hasa mahakama inapaswa kutumia vigezo vyake kwa kuzingatia kuwawajibisha wahusika na katika ili tunapaswa kuwa na 'Zero tolerance wakati wa kuwachukulia hatua'," aliongeza

Pia alisema kuwa suala la kuwafumbia macho viongozi wabadirifu madarakani ndiyo chanzo kinachochangia baadhi ya mipango ya maendeleo ya wananchi kutofanikiwa mapema.

"Ukienda katika Halmashauri utagundua kuwa hali ni mbaya kweli kutokana na watendaji ambao wanajihusisha na suala la hongo hasa katika mpango wa kilimo kwanza katika hatua za kuagiza na kuwapatia wakulima powertiller hivyo hali kama hii haipaswi kufumbiwa macho bali hatua zinapaswa kuchukuliwa dhidhi yao mara baada ya uchunguzi," alisema Bw. Msuya.

"Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani siyo kwa dhumuni la kuwatumikia wananchi kama awali bali kujilimbikizia mali na hata kutekeleza mipango yao.Tuchukue mfano kwa Mwalimu, watoto wake na Mzee Kawawa utagundua kuwa licha ya kukaa madarakani kwa muda mrefu maisha yao ni ya kwaida kama watanzania wengine tofauti na sasa tunavyoshuhudia watu wameenda kujilimbikizia mabilioni nje ya nchi huku wakiyaita vijisenti, wengine wakijenga majengo na kuendesha magari ya thamani kubwa bila kujali maslahi ya wananchi," alisema Bw. Msuya.

UMEME

Bw. Msuya alisema kuwa suala la umeme hata kama litaendelea kupigiwa kelele kwa namna gani nchini kama serikali na hata vyama vya upinzani havitakaa kwa pamoja wakiwemo wataalam ili kuandaa michanganuo inayoeleza namna ya kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini zitakuwa kelele ambazo hazina tija.

"Hata misimamo iwekwe ya namna gani ya kutaka kuwashinikiza vingozi walioko madarakani wakiwamo wale wa Wizara ya Nishati na Madini wajiuzulu, ufumbuzi juu ya tatizo la kudhibiti mgawo wa umeme hauwezi kupatikana kwa kuwa kinachoitajika kwa sasa ni uwekezaji na michanganuo inayoonesha namna ambavyo rasilimali zilizopo hapa nchini kama makaa ya mawe, gesi,upepo na nishati ya jua inavyoweza kutumika kuzalisha umeme," alisema Bw. Msuya.

Alisema imefikia hatua kwa serikali kuwekeza zaidi katika nishati ya umeme kupitia mipango ambayo walikuwa wanatumia awali ya miaka mitano kwa madai kwamba rasilimali zilizopo hapa nchini zinaweza kuzalisha umeme wa kutosheleza kwa matumizi ya ndani na hata kwa ajili ya kuuza nje.

"Tatizo hili tunaloshuhudia la nishati linatokana na utaratibu usioridhisha katika serikali ya awamu ya tatu, kwa kuwekeza fedha vibaya na wala siyo awamu ya nne hawa walibebeshwa mzigo tu' kutoka kwa EPA, RICHMOND lakini kwa mtazamo wangu ninaona waliohusika wote wakati wakiendelea kuchukuliwa hatua za kisheria serikali inaweza kuajiri na hata kuwatumia wataalam wa ndani na nje ili kuandaa michanganuo ya kutuondoa hapa tulipo sasa," alisema Bw. Msuya.

MALUMBANO BUNGENI

Bw. Msuya alisema kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani kwa sasa siyo kwa lengo la kuwasiadia ama kutatua kero za wananchi bali wamelenga maslahi binafsi.

"Ninakiri hadi leo hapa tangu 1992 mara baada ya serikali kufikia uamuzi wa kujiunga na mfumo wa vyama vingi sijamuona kiongozi mwenye uthabiti na mwelekeo wa kumsaidia mwananchi na hata kelele wanazopiga bungeni kwa sasa wala hazilengi kumsaidia mwananchi bali wanalenga maslahi yao tu.Kiongozi mwenye nia ya dhati kwa ajili ya kumsaidia mwananchi huwa anaadaa mchangunuo mzuri unaoelekeza jinsi ya kuzikabili kero za wananchi wala siyo kusema tu,"alisema Bw. Msuya.

UCHUMI

Kwa upande wa uchumi alisema kuwa uwezekano wa Tanzania kuipita Kenya katika ukuaji wa uchumi wake kupitia kipimo cha GDP upo wazi kwa kuwa hali ilivyo kwa sasa mwelekeo huo upo ila kinachoitajika ni jitihada na uwajibikali kwa kila mtendaji na wananchi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hasa madini, vivutio vya ukalii, mbuga, gesi na mito.

"Uchumi wetu umeendelea kukua siku hadi siku kwa asilimia saba hadi kumi tofauti na Kenya ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia tatu hadi tano lakini kwa kupiga hatua zaidi. Tatizo ni kwamba ukuaji huo wala hauonekani kutokana na kutotumia vyema rasilimali zetu lakini ninaamini zikitumika vyema siku si nyingi tutaipita hata Kenya kiuchumi," alisema Bw. Msuya.
 
"Ninakiri hadi leo hapa tangu 1992 mara baada ya serikali kufikia uamuzi wa kujiunga na mfumo wa vyama vingi sijamuona kiongozi mwenye uthabiti na mwelekeo wa kumsaidia mwananchi na hata kelele wanazopiga bungeni kwa sasa wala hazilengi kumsaidia mwananchi bali wanalenga maslahi yao tu.Kiongozi mwenye nia ya dhati kwa ajili ya kumsaidia mwananchi huwa anaadaa mchangunuo mzuri unaoelekeza jinsi ya kuzikabili kero za wananchi wala siyo kusema tu,"alisema Bw. Msuya.
Nadhani huyu mzee anashinda muda mwingi amelala kama hajaona dr slaa anafanya vitu hivyo kwa vitendo basi hatuko naye tanzania labda kaja jana au yupo lakini amelala muda wote Bajeti ya chadema nimchanganuo tosha wa namna wananchi watakavyo letewa maendeleo sio blabla za ngeleja na wana magamba wenzake nadhani ifikie pahala maoni ya wazee walio choka kama huyu yasitiliwe maanani kwani yatakua yanapotosha wananchi hasa kuhusu wamwamini nani mwenye mlengo wa kujari maslai ya umma kwa dhati. Nashukuruu kumuona dr slaa akiwa hai kila siku.

Nadhani huyu kawalenga wale wa Magamba ila sina uhakika na hili.
 
Ananishangaza huyu mzee, kwanza kusema tangu vilipaonza vyama vingi hajaona kiongozi mwenye nia thabiti ya kumkomboa mtanzania na pili kwa kusema uchumi wetu unakua kwa asilimia 7 hadi 10 halafu hapohapo anakiri ukuaji hauonekani.

Maoni yangu ni kwamba kama mtu alibahatika kuwa kiongozi na katika kipindi chake cha uongozi mambo mengi yalifeli ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa kasi kwa uchumi wetu, leo awezaje kuwa na mawazo chanya ya kututoa hapa tulipokwama? Katika kipindi chake cha uongozi ni mradi gani wa umeme waliubuni na kuuanzisha ambao uli focus miaka 100 mbele au ni kale kale kaugonjwa ka mw100 zikizidi ni mw300? Hebu tuitazame hata Congo drc leo wana mradi wa mw 10,000 sisi tulishindwa nini miaka hiyo ya kina Msuya kuwa na vision ya miaka mingi mbele?
 
Nadhani huyu mzee anashinda muda mwingi amelala kama hajaona dr slaa anafanya vitu hivyo kwa vitendo basi hatuko naye tanzania labda kaja jana au yupo lakini amelala muda wote Bajeti ya chadema nimchanganuo tosha wa namna wananchi watakavyo letewa maendeleo sio blabla za ngeleja na wana magamba wenzake nadhani ifikie pahala maoni ya wazee walio choka kama huyu yasitiliwe maanani kwani yatakua yanapotosha wananchi hasa kuhusu wamwamini nani mwenye mlengo wa kujari maslai ya umma kwa dhati. Nashukuruu kumuona dr slaa akiwa hai kila siku.

Acha porojo zako....wewe ndio utakuwa upo usingizini mpaka sasa...........Slaa kafanya nini?
tupe mfano Mmoja........Budget ya Chadema sio Mpya ni za kawaida tu kama nyingine zinazokuja zote ni porojo kama nyingine....ndio maana huyo Mkongwe wa siasa anasema hajaona.............
 
haka kazee nacho kaache unafiki yeye mwenyewe kipindi chake hakuwa msafi hivyo! na hata kama matatizo ya umeme yalitoka awamu ya tatu, still Kikwete hawezi kuepuka lawama maana uwezo wa kurekebisha (to account individuals) anao kikatiba!
 
Atoke zake huko Wakiwa Kwenye Madaraka hawasikii wala hawaoni wakitoka wanajifanya kukosoa, Si alikuwa kwenye Serikali ya Fisadi Mkapa.
Tunachokita Watanzania kuiondoa CCM na Majambazi wake, ili tujipange upya
 
Inashangaza kusikia mtu kama Msuya akisema hajaona kiongozi yoyote tangu mwaka 1992 mwenye mwelekeo wa kumsaidia mwananchi, anasahau wakati yeye akiwa kiongozi alishasema KILA MTU ATAUBEBA MZIGO WAKE MWENYEWE.
 
Au ni mimi sijui kusoma? maana nimerudia mara mbili sioni anapomlaumu mkapa..

"Tatizo hili tunaloshuhudia la nishati linatokana na utaratibu usioridhisha katika serikali ya awamu ya tatu, kwa kuwekeza fedha vibaya na wala siyo awamu ya nne hawa walibebeshwa mzigo tu' kutoka kwa EPA, RICHMOND lakini kwa mtazamo wangu ninaona waliohusika wote wakati wakiendelea kuchukuliwa hatua za kisheria serikali inaweza kuajiri na hata kuwatumia wataalam wa ndani na nje ili kuandaa michanganuo ya kutuondoa hapa tulipo sasa," alisema Bw. Msuya.

Kiongozi wa awamu ya tatu alikuwa nani ? Wewe unataka mpaka huyu Msuya ataje majina ya watu? Kwa mtu mwenye staha na diplomasia hata kutaja awamu tu kunatosha.
 
Inashangaza kusikia mtu kama Msuya akisema hajaona kiongozi yoyote tangu mwaka 1992 mwenye mwelekeo wa kumsaidia mwananchi, anasahau wakati yeye akiwa kiongozi alishasema KILA MTU ATAUBEBA MZIGO WAKE MWENYEWE.

Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe inaweza kutafsiriwa namna nyingi, labda sasa ni muda wa ku revisit scenario nzima iliyopelekea usemi ule.

Maana wengine wataona ni kiongozi anayetaka kukimbia wajibu wake wa kuongoza wananchi, na kuwaambia "kila mtu kivyake".

Wengine watasema ni kiongozi anayewaambia wananchi kwamba "maendeleo hayaletwi na kiongozi, kiongozi anafanya sehemu yake (mzigo wake) na wananchi nao inabidi wafanye kazi na kuchukua mzigo wao". Msuya alikuwa ana draw mifano yake mingi kutoka dini, na watu wa dini wanaamini kwamba kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, hakuna wa kukubebea dhambi zako ukiileta katika context ya kisiasa inaweza kuwa hakuna atakayekuletea maendeleo.

Msuya is probably being a harsh critic, lakini ukiangalia uongozi wetu, umasikini wetu na longolongo zetu he is probably right. Although that sentence does not exclude himself.
 
mambo haya ya kutafuta wachawi ndo yanasitawisha umasikini. Badala ya kutoa mawazo ya jinsi ya kutoka hapa tulipo tumejikita kwenye kutafuta umaarufu binafsi. Ama kweli uhuru kutoka umaskini bado upo mbali na jamii ya watanzania.
 
Huyu mzee anamaanisha ndani ya magamba hajaona mtu mwenye uwezo wa kuikomboa nchi. Amefocus CCM kwani ndio walioshika dola. Dr. Slaa hajakabidhiwa nchi, Slaa mwangalie jimboni kwake Karatu zamani alichokifanya, hapo ndipo mpime uwezo wake. Kwasasa Slaa kazi kubwa anayofanya ni kuwatoa matongotongo watanzania na matokeo yake tumeyaona, kwamfano hata Singida, Ruvuma, Morogoro, Dodoma kuwa na Madiwani wa Upinzani ni hatua kubwa sana. Tanzania tupo nyuma politically kuliko majirani wetu wote, mfano mdogo Malawi kwasasa hawana campaign za kijinga kama 'nitaleta maji; Kwamfano Malawi umeme ni MK 2500 sawa na Tshs 21,000/= tu na hao hawana hata makaa ya mawe. Kuongozwa na CCM ni laana kwetu, fikiria wizara inatoa rushwa kwa wabunge bajeti ipitishwe? Chukulia hili suala ingekuwa ni Zambia tu kwamfano ingekuwaje, all in all hatuna CHAMA ila tuna GENGE LA MAFIA. BORA NAZI YA HITLER AU BAARTH YA SADAM KULIKO CCM. Mungu tusaidie.
 
Acha porojo zako....wewe ndio utakuwa upo usingizini mpaka sasa...........Slaa kafanya nini?tupe mfano Mmoja........Budget ya Chadema sio Mpya ni za kawaida tu kama nyingine zinazokuja zote ni porojo kama nyingine....ndio maana huyo Mkongwe wa siasa anasema hajaona.............
Mkuu Msuya anazungumzia viongozi walioko madarakani,Dr Slaa hayuko madarakani. Tusibiri akishika madaraka tutajua tofauti yake na magamba! Kimsingi watanzania wengi wanaimani sana na Dr. Slaa kwa sasa ndiyo maana unapotaja kiongozi mzuri watu wanakimbilia kumtaja yeye japo si mtawala bado. Ukweli huu huwezi kuondoa mioyoni mwa watu ndivyo ilivyo hata kama wewe hutaki itabidi uvumilie tu ndiyo siasa.Dr. Slaa amekuwa chachu ya kuibua uozo wa serikali za ccm na kwa hili anastaili kupongezwa kwa mtanzania yoyote asiye fisadi au mchumia tumbo.Dr. Slaa na cdm wanatumia muda wao kuwaelimisha watanzania ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawajui kinachoendelea ndani ya ccm. Ujinga na kutofatilia mambo ndicho kilichowafanya ccm wajisahau na kujiona kuwa wao ni watawala milele. Ccm na serikali nadhani walifika mahali hata kusahau kuwa wao ni watumishi wa wananchi lakini kutokana na ujinga wa wananchi walijiona wao ni mabosi na wananchi ndiyo watumwa wao.Kimsingi unaweza kumwona Dr. Slaa mbaya kwa sababu ulikuwa fisadi au mchumia tumbo na sasa mambo yako yameharibika. Lakini kwa mtatnzania ambaye amekuwa akiteseka kwa umasikini na manyanyaso ya ccm anamwona Dr. Slaa ni mkombozi.Karibu kwa hoja mkuu
 
Msuya hakusema kwamba anaongelea viongozi wenye serikali au wapinzani. Isitoshe, ukiongelea "madaraka" wabunge wamepewa madaraka ya kibunge na wananchi na parliamentary privileges na katiba, unataka madaraka gani kuanza kufanya kazi ya wananchi?

"Ninakiri hadi leo hapa tangu 1992 mara baada ya serikali kufikia uamuzi wa kujiunga na mfumo wa vyama vingi sijamuona kiongozi mwenye uthabiti na mwelekeo wa kumsaidia mwananchi na hata kelele wanazopiga bungeni kwa sasa wala hazilengi kumsaidia mwananchi bali wanalenga maslahi yao tu.Kiongozi mwenye nia ya dhati kwa ajili ya kumsaidia mwananchi huwa anaadaa mchangunuo mzuri unaoelekeza jinsi ya kuzikabili kero za wananchi wala siyo kusema tu,"alisema Bw. Msuya.

Mtake msitake hili dongo linajumuisha viongozi wote, pamoja na wapinzani.

Wewe unafikiri kwa nini kataja mwaka 1992 na serikali kukubali mfumo wa vyama vingi? Anataka kuujumuisha uongozi wa serikali na uongozi wa upinzani na kusema wote si mali kitu.
 
Ni mwaka wa 6 sasa tangu Mkapa aondoke madarakani, na muda wote huo nchi imekuwa kwenye mgao wa umeme. Kwa nini Msuya hakujitokeza kipindi hicho na kusema haya anayosema sasa hivi? Kwenye semina elekezi mapema mwaka huu huko Dodoma Mzee Msuya alitoa mada na kama sikosei aliongelea 'collective responsibility' or something close to that. Hivi mtu akisema kuwa Mzee Msuya kwa sasa 'amekodishwa' kutetea walioko madarakani atakuwa anamzushia?

Uongozi wa Mwl. Nyerere umekuwa under attack recently na kama kiongozi aliyekuwepo kipindi cha Nyerere kwa nini asitoa clarification especially the fact that Mwl Nyerere ni marehemu.
 
Unaweza kuchagua kuona kauli ya Msuya kulaumu awamu ya tatu kama utetezi wa awamu ya nne, ukitaka unaweza hata kuona katumwa.

Lakini kama katumwa, kwa nini aendelee kusema tangu 1992 serikali kukubali vyama vingi hajaona kiongozi haswa Tanzania?

Na kama lengo lake ni kuitetea awamu ya nne, kwa nini aiponde sio tu kwa kusema haina uongozi, bali pia kwa ku imply kwamba haikuweza ku reverse mabaya yaliyofanywa na awamu ya tatu?
 
Mbona nasikia kale kafisadi kadogo kanaitwa David Mathayo ni katoto kake!
 
Msuya angenyamaza tu yeye ndiye wale mafisadi wa kwanza kwanza ambao hawakuweza kufurukuta sana kutokana na kibano na kumwogopa Mwalimu. Lakini hata hivyo akumbuke jinsi alivyokuwa anawapendelea wananchi wa jimbo lake hivi anafikiri wananchi wamesahau?
 
Ukisikia mzee kazeeka vibaya ndo kama Msuya. Tanzania tunahitaji kufanya mapinduzi ya kuondosha hili genge la wezi ambalo waasisi wake ni pamoja na akina Msuya. CCM ni genge la wezi.
 
Back
Top Bottom