GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Written by Nasikia kichefuchefu nikikumbuka muungano // 06/02/2012 // Habari // 46 Comments
Na John Gagarini, Kibaha
Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano amewataka Watz wasikubali kuuvunja Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba mpya.Aliyasema hayo jana Mlandizi Kibaha Vijijini wakati wa sherehe za kutimiza miaka 35 za kuzaliwa CCM Mkoa wa Pwani na kusema kuwa Watanzania wanapswa kudumisha Muungano na wasikubali kurubuniwa na wanasiasa wasioitakia mema nchi.
Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kutumia marekebisho hayo kutaka kuvunja Muungano na kuleta USULTANI jambo ambalo si zuri kwani Muungano umeleta mambo mazuri na kikubwa kikiwa ni amani iliyopo. "Kama mtu anakuja kuwaambia mvunje Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba msikubaliane naye, kwani haitakii mema nchi yetu kqwani amani na upedo vimedumu kwa kupitia Muungano hivyo tusikubali kudanganywa: alisema Dk. Bilal
Angalia hapa SMZ mkakati wao.
Vijana Zanzibar kuajiriwa uarabuni
Vijana Zanzibar kuajiriwa uarabuni
Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 6th February 2012 @ 15:15 Imesomwa na watu: 157; Jumla ya maoni: 0
NCHI za Kiarabu zikiwemo Oman, Qatar pamoja na Kuwait zimekubali kutoa ajira kwa vijana
wa Zanzibar katika nchi hizo.
Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Ajira na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Haroun Ali Suleiman alisema hayo mwishoni mwa wiki na kueleza kuwa nchi hizo zimekubali kutoa ajira na mipango ya kusaini makubaliano hayo ipo katika hatua za mwisho.
Haroun alisema viongozi wa nchi hizo tayari wamefanya mazungumzo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kuwapatia ajira zenye maslahi bora vijana wa Zanzibar.
"Kimsingi tumekubaliana na wenzetu hawa wa nchi za Kiarabu kutupatia ajira kwa vijana wa Zanzibar ambapo makubaliano yapo katika hatua za mwisho," alisema Haroun na kuongeza kuwa lengo la SMZ ni kuhakikisha vijana wanapata ajira lakini zenye mazingira mazuri yenye heshima.
Aidha, aliitaja mikakati mingine itakayozalisha ajira ni kuimarishwa kwa vyama vya ushirika pamoja na vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) kwa makundi ya wanawake.
"Tayari tumeanza kusajili zaidi ya vyama vya ushirika 3,000 pamoja na Saccos ambazo matumaini yetu makubwa zitazalisha ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake," alisema Waziri huyo.