Msitu wa Pande sasa kuwa mbuga ya kitalii

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
2,608
6,503
Mbunge wa viti maalum CDM Mariam Msabaha amemtaka waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Kagasheki kuufanya msitu wa Pande eneo la utalii kwa kuweka wanyama badala ya kupafanya eneo la mauaji.Hayo yalisemwa na mbunge huyo wakati akichangia hotuba ya waziri huyo
 
Sasa kama wakiifanya kuwa sehemu ya utalii si itakuwa pigo sana kwa serikali ya CCM na vyombo vyake vya usalama maana watakuwa wamepoteza chombo muhimu cha kutesea na kuulia wadai haki.
 
Duh huyu mbunge sijui kama atakuwa salama ngoja namsubiri Mukama na Nape lazima watamtwanga barua kwa kupingana na sera za CCM.
 
Du! Serikali ya ccm haiwezi ikakubali kipenzi chake kikubwa msitu wa pande matumizi yake yabadilike Kama ilivyo kwenye ile katiba yao ya mambo ya kutesa wadai haki
 
Tayari CCM wameridhia kuanzisha Tawi hapo Msitu wa Mwabepande.... Kwahiyo kuiweka iwe sehemu ya Utalii watakuwa Wamedharirishwa!!
 
Iwe mbuga ya watalii sio kwa ajili ya wanyama ila tutakuwa tunaenda kuangalia watu waliopewa kisago nusura kufa, naunga mkono hoja.
 
Huyu ni mbunge wa Chadema, viti maalum.hawana ubavu wa kumpa barua, wataanzia wapi?
 
Ukweli mimi sijui hiyo misitu iko upande gani ila nasikia ni hapo hapo Dar Es Salaam..si igeuzwe yote kuwa ya kitalii kama inakidhi haja?
 
Hapo kweli ni machinjioni...........ila eneo la machinjio linaweza kufungwa wakati wowote.
 
haha watu wanafikir utalii ni wanyama tuu, pengine historia yake ya mauaji(haya tuyajuayo na mengine yatafutwe kwa kuulizia raia mizoga waliyoikuta humo, wafanyakazi wa vyombo vya usalama na majambazi wastaafu), italeta mvuto kwa watalii wenye misngi ya haki za binadamu pamoja na historia za serikali dhalimu.Pengine itakuwa kumbukumbuku mbaya ya CCM kam ya waNazi
 
Iwe sehemu special kwa wanafunzi wa udaktari kwenda kujifunza anatomy ya mifupa ya binadamu yaani human skeleton
 
au waweke camping site.....watoto wakishua wawe wanaenda kupumzika weekend na hii itakuwa safi kwani kutakuwa na ulinzi au sio wadau....
 
Back
Top Bottom