Msimu wa utalii Zanzibar na kasheshe lake kwa wageni Waswahili

Bassanda

Member
May 14, 2009
53
3
Msimu wa utalii katika kisiwa cha Zanzibar umepamba moto mwezi huu wa Julai lakini kuna mambo na vijimambo kwa wageni wenyeji. Hivi majuzi kuna jamaa mmoja katokea Zanzibar alikuwa kaenda huko kikazi akitokea bara. Anasema imemtokea si chini ya mara mbili kuondolewa kwenye chumba cha hoteli mbili tofauti alikokuwa kafikia baada ya watalii wa kizungu kuwasili kwenye hoteli hizo. Kinachotokea ni kwamba kama wewe ni mswahili, haijalishi uwe umetokea bara, Zanzibar au kwingineko, uombe tu wasitokezee wazungu wakahitaji kupata vyumba hapo ulipo. Kama vyumba havitoshi ukiwa mswahili utaambiwa "yakhe tulisahau kukujulisha kuna wageni wanawasili leo walishafanya bukingi siku nyingi, hivyo tunakusihi utafute hoteli nyengine". Ukibahatisha kubakia, utashanga huduma kama ya breakfast inabadilika. Mtaanza kuhudumiwa hadi matunda ambayo mlikuwa hamyapati mlipokuwa wapangaji waswahili watupu. Kwa hivyo ukitokea bara ukaenda na hasira zako Unguja haitakusaidia kwani hoteli nyingi Zanzibar ndiyo mchezo wao huo, inabidi tu uwe mpole hakuna ujanja. Tunashukuru kwa bara upuuzi huo haupo na mtu akikufanyia hivyo mtafikishana pabaya, kwanza hawezi kudhubutu!
 
Kwani hao wazungu wanakwenda kwenye hotel hizo bila kuwa na buking? Kwa kawaida watalii wanafanya buking mapema kwa jinsi kwamba wenye hotel wanakuwa wanajua ni kina nani wanakuja na nafasi zao za vyumba zinakuwa wazi. Iweje haya unayosema yajitokeze?
 
si mzitaje majina kama mna uhakika huduma ilibadilika kabla ya kufika wazungu na baada yake?
 
Hiyo ni discrimination.Sheria zetu zinasemaje kuhusu hilo? Na ukigoma inakuwaje?
 
Kwani hao wazungu wanakwenda kwenye hotel hizo bila kuwa na buking? Kwa kawaida watalii wanafanya buking mapema kwa jinsi kwamba wenye hotel wanakuwa wanajua ni kina nani wanakuja na nafasi zao za vyumba zinakuwa wazi. Iweje haya unayosema yajitokeze?
Inawezekana labda ni Backpackers, wengi wanakuwa hawafanyi booking.
 
Unakubali vp kutoka ilhali ulishalipia for certain no. of days? Kwani kuna tofauti ya rate katika malipo ya hivyo vyumba kwa wageni na wenyeji
 
Hii imekaa kaa kiuswahili.....

Kwanza zitaje hizo hoteli na nina amini Waandishi wa Tanzania bara wataenda kutafuta habari huko kwa nguvu. Hii ni makala safi kabisa ya kuandika ila kabla hawajawa na uhakika, hawawezi kukurupuka na kuanza kumwaga wino kwa habari iliyoandikwa kwa woga ndani ya JF.

Hata hivyo asante kwa kutujuza na nina uhakika kuna watu wataifatilia kama ni ya kweli au imepikwa na kuopolewa JF...
 
huo ubaguzi upo hata hoteli za Mombasa. tena zile ambazo zipo ufukweni yaani ni tabu tupu waswahili sisi ni pombav sana
 
Uwongo huu.
Hembu weka majina ya hizo hoteli na data za huyo aliefika mie nitawasiliana na wamiliki watoe maelezo hapa.

Wewe usilete issue za ubaguzi kwa kuonekana Zanzibar haithamini wageni wazalendo.

Labda nikupe angalizo tu,ni kwamba ujue kuna Tofauti ya Hotel na Guest Houses kwa matumiz ya Dar na Zanzibar.
Huku sehem nyingi watu wana Imani zao,Huwezi kuwa kila siku unazoa machangudoa Pale Bwawani Comba Disco kisha unaendanao kwenye Chumba cha hoteli ukafikria watakukubalia uzinifu huo,maana kuna watu ndio zao,wakija wanatafuta chumba basi kila siku katoa dem huyu kaleta huyu.Zanzibar Ujinga huo wa Tandalle huku hautakiwi.

Sasa mwambie huyo Jamaa yako afunguke.
 
Enhe, sinema ndo inazidi kunoga BASANDA lete maneno,sie tulozoea gesti naona hatutakiwa Unguja.
 
Ila watanzania kwa kulalamika lalamika na kuzua uongo sijui mnafaidika na nini? Mimi natoka bara na niko Zanzibar kikazi. Kabla sijafika niliambiwa mengi kuhusu wazanzibar lakini nimefika sijaona hata chembe ya ubaguzi tena zaidi wazanzibar wana upendo na wako juuu sana kwa uaminifu kuliko bara. Kabla hujamuonyesha kidole mwingine jitathmini kwanza...
 
Ooyooo tatizo si ubaguzi na kama ubaguzi basi hata na huku bara upo na tatizo hilo ni la malipo ya hotel na malipo ya mzungu ni Dolla yenye baraka ya dunia na ya huyu mswahili kutoka bara malipo yake ya pesa ya madafu ambayo haina Thamani au kama haina baraka ndo hayo mizengewe na bado tutachonga sana
 
Back
Top Bottom