Msimamo wa Tanzania kuhusu Syria ni upi?

Nadhan wanaunga mkono kuondoka na au kubaki kwa ASSAD!!

Hili swali MEMBE ANGEJIBU HIVI: NI KUONDOKA.........then kwenye ufafanuzi akibwana atasema alikuwa akimaanisha KUONDOKA KWA WAASI then akiwa na mabalozi atasema ni KUONDOKA kwa ASSAD kama nilivyosema mwanzoni

Take:TUMWACHE ASSAD AWAMALIZE HAWA RAIA MANAKE US+NATO wakiingia waislam wanaongea sana sasa ASSAD GO ON WAMALIZE WAARABU

Wewe unabifu na chuki dhidi ya waislam. Hivi unaona kuwa NATO kubomowa kwa mabomu sehemu ya libya ambayo wanaishi raia na kuua watoto ni kutetea haki za binaadam? NAKUOMBA UTOE MAELEZO KUHUSU JESHI WA NATO KUUWA WA AFGHAN 17 wakiwemo watu wazima wanawake na watoto, ni sawa hiyo? Mbona NATO inavamia sehemu yenye intrest zake binafsi? USA wali accused kuwa Saddam ana weapons of mass destruction, mbona walipomuua hawajituonesha? Na nani alokua akimsaidia saddam kupigana na iran? YOU HAVE BEEN BRAINWASHED!! Pole sana
 
Anaua watu analinda nchi hahahahaaaa!!!!!!!

Tatizo liko wapi? wananchi ambao si waadilifu katika hchi yako wanini? VIBARAKA WA MAGHARIBI , nini kimetokea Libya? unaona wanavohaha sasa hivi kuijenga nchi yao? wanavolalama kwanini waliruhusu NATO ipige mabomu ! huwezi kunielewwa kwasababu una chuki ndani ya nafsi yako! hata uambiwe vipi huwezi kuelewa, SUBIRI WAKATI WENU UTAFIKA TU !
 
Nimetaka kujua tu ili niweke kwenye record ili tusijekuhitilafiana uko mbele, sababu kama hizo hoja zako ndio za muhimu sana ili Taifa liweze kusikilizwa, ninalazimika kureview records kuona kama Tanzania ya Nyerere ilikuwa inasikilizwa au nini kile kilikuwa kinaendelea.
Tanzania ya nyerere sio Tanzania ya sasa. kwanza kabisa nyerere alishatengeneza jina kwa sababu kwanza kipindi kile kulikuwa na harakati za ukombozi wa bara la africa, na nyerere ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanaogopwa sana, yeye aliweka makambi mengi hapa tz ya wasouz wakiwa trained kwenda kupigana, na askari wetu wameenda sana kupigana vita angola, namibia, mozambique na zimbabwe sana.

Ukilinganisha kuwa kipindi kile kuliwa na cold war, nyerere akawa ameweka msimamo wake wa ujamaa na kujiunga na wachina na warusi, basi wazungu walikuwa wanamsikiliza sana akisema chochote kwasababu maslahi yao yalikuwa tete sana kipindi kile katika kutetea umagaribi etc. hata hivyo, pamoja na kwamba nyerere alikuwa anaongea sana na wanamsikia, kwasababu walikuwa wanajua kanchi ni kamasikini walimpuuzia tu, kwasababu walikuwa wanajua hatafika popote...na ndio maana aliachia ngazi mapemaa baada ya maji kufika shingoni, akaepuka aibu. jinsi nyerere alivyokuwa anachukuliwa kipindi kile huwezi linganisha na jinsi Russia au China walivyokuwa wanachukuliwa, wachina na warusi walikuwa wanasikilizwa sana ila vya nyerere nani alivitilia maanani zaidi ya kumfunga miguu kwa kamba bila yeye kujua?

Kubali usikubali, nchi masikini hatutakuja tuwe na sauti hadi pale uchumi wetu utakapokuwa mkubwa na hatarishi kutishia uchumi wa nchi zingine, hapo ndo tutasikilizwa. kwani souz africa akiongea na tz akaongea hapohapo unafikiri nani atasikilizwa kwanza? unaona sasaivi jinsi wachina na warusi wanavyowaendesha wamagaribu kuhusu suala la iran, syria na korea kaskaz? china na urusi wangekuwa malofa wamagaribi wasingewasikiliza kabisa.....

Hapa Tz tuiondoe CCM, tujenge nchi upya, tukiendelea uchumi wetu ukawa unashindana na uchumi wa watu wengine ndipo hapo tutanweza kusikilizwa, ila kwa sasa sisi ni malofa tu mwanangu, hatuna lolote hata tukiongea sauti zetu hazitasikika... Kwani kipindi kile Membe alipoongea kuhusu libya, uliona wamagaribi wameliweka suala hilo kichwani? walijua huyu lofa anaongea nini masikini watu wake wanaishi chini ya dola?

Hata wakiamua kutikisa tu kanchi kake anaweza kukubali hata kuruhusu ukameruni, ndiomaana wana ujasiri hata kutuambia tukubali useenge...na nchi zetu zinahahahaha tu, misaada tunataka, useeenge hatutaki...wanatunyanyasa wapendavyo. kama huna kitu mwanangu mjini hapa unaweza kuolewa...haha.
 
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.

Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?

Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?

Mzee,

Unauliza mambo mengi na magumu! Watu tuko bize na kutafuta urais, hutuachi tupambane? Hata watanzania tu na maisha yao wako kimya, seuze Syria?
 
Hoja zako zimeisha pitwa na wakati. Ni hoja za miaka ya 1980!
NAdhani hujui unalolisema,.

Kwanza naomba nikujulishe kuwa zile zote ni hila za kimagharibi KUTAKA KUINGIA IRAAN kwa urahisi, wameshakali Quwait na Saudi Arabia na Afghanistan ili iingie kirahisi Iraq, sas hivi INAHAHA KUINGIA IRAAN, na inaona kikwazo kikubwa kipo USSR Urusi , haiwezi kuipiga Syria kwa sababu ya Urusi na msimamo wake juu ya Syria na Iraan, na once ikishaingia Syria basi ni wazi wataingia Iraan kirahisi na hatima middle east yote itakuwa imekaliwa na wamagharibi.

Kinachonishangaza kwanini mnashabikia mambo ya kimagharibi sana na badala ya kuwaonea imani waarabu na mafuta yao? kuna siku PAsco alimshambuli sana mwanakijiji na misimamo yake na wagharibi leo ndio nimeamini, nahisi mwanakijiji anawapenda wamagharibi kwa ajili ya Udini! nilikuwa nikimheshimu sana lakini sasa naanza kuondoa imani na heshima yangu juu ya huyu mtu ! kweli ANANISHANGAZA !
 
Mzee Mwanakijiji, nadhani kama serikali ya Tanzania ingekuwa inazingatia ni nani anaonyesha nia ya kuleta amani ya kweli nchini Syria kati ya Uongozi wa Serikali halali ya Syria na Waasi wa nchi hiyo ya Syria kwa kupima matendo na maneno ya pande mbili hizi, basi Serikali ya Tanzania yapaswa kuunga mkono Uongozi halali wa serikali ya Syria
 
Unachekesha sana sana! ASSAD anua watu wake au ANALINDA NCHI yake dhidi ya mabeberu ya magharibi? hebu nenda deep katika hili, tumeona mengi yamefanywa na hawa wamagharibi wao wakiua wanalinda raia, rais akilinda nchi yake dhidi ya puppets wa magharibi anaua! unacheksha sana tena sana! itakuwa labda nimekosea kusema udini lakini juzi juzi nimeona Pasco akilumbana na mwanakijiji juu ya swala la yeye kuwa mrengo wa magharibi na amediriki kumuita puppet wa magharibi sasa NAAMINI !

Sasa akishindwa kulinda nchi yake itakuwaje? Atanyongwa ama ataishia Hague - matokeo yatakua mabaya zaidi kwa raia wake. Nadhani cha maana angeruhusu aina fulani ya uchaguzi huru ufanyike ili aachie ngazi na kuokoa maisha ya watu. Power ikiwa transfered kwa amani bado Urusi na China watampongeza na wataendelea kuisapoti nchi yake.
Ndio kuna makabila hayampendi (umewaita puppets?) lkn kwa nini ASADI asijifunze kwa BOTHA? Kwa madikteta ama serikali kama CHINA, Serikali ni supreme hamna anayeruhusiwa kuishinda kwa maandamano ama namna yeyote ile - ndio maana kwa China mtu kama BOTHA ni SHUJAA kuliko Mandela kwa kua hata kama alikua ameshika serikali bado aliamua kuondoa UBAGUZI WA RANGI (kwa hiari? kubanwa? hio sio tija) na kuruhusu kura huru.
 
Hute

Hauoni kwamba msimamo wako unamaanisha kwamba tuzipigie magoti nchi zilizoendelea, sababu kama hatuwezi kuchukua hatua yoyote, na sasa unadai hatuwezi hata kusema, Sababu sisi sio wafu ni lazima kuna kitu tunafanya, kama maelezo yako ni fact basi hicho kitu ni kufuata maelekezo ya nchi Tajiri, na kama hali ndio hii ni nini kinakufanya ufikirie tukiiondoa ccm madarakani ndio tutajitoa kwenye hali ya kishenzi namna hii?

Naomba nitofautiane na wewe rasmi kwamba, ni lazima tujiheshimu na tujitambue na kujitambulisha msimamo wetu sasa, no matter how poor we are.
 
Last edited by a moderator:
Hauoni kwamba msimamo wako unamaanisha kwamba tuzipigie magoti nchi zilizoendelea, sababu kama hatuwezi kuchukua hatua yoyote, na sasa unadai hatuwezi hata kusema, Sababu sisi sio wafu ni lazima kuna kitu tunafanya, kama maelezo yako ni fact basi hicho kitu ni kufuata maelekezo ya nchi Tajiri, na kama hali ndio hii ni nini kinakufanya ufikirie tukiiondoa ccm madarakani ndio tutajitoa kwenye hali ya kishenzi namna hii? Naomba nitofautiane na wewe rasmi kwamba, ni lazima tujiheshimu na tujitambue na kujitambulisha msimamo wetu sasa, no matter how poor we are.
my friend,nyerere angekuwepo ningekuambia uende ukamwulize kama alifanikiwa kwa lolote katika misimamo yako ya aina hii. ukiwa huna kitu rafiki yangu huna lolote. hata ukikataa kuwasikiliza wamagaribi utajikuta uumefika maji shingoni na kusalenda tu. nasema tuitoe ccm kwasababu nategemea pengine tukiwa na utawala mpya tutakuwa na sera na vision mpya na kujikwamua kwenye umasikini pengine kanchi ketu kakiwa kanagusa maslahi ya wakubwa kwa namna fulani hasa ya kiuchumi, basi hapo tutaanza kuwa na sauti, ila kwa sasa, matatizo yetu sisi wenyewe tu yametushinda, ya syria tutayaweza? hata ukisema nani atakusikiliza?
 
Kimsingi mambo yanayoendelea Syria sio mepesi kama tunavyofikiria. Wamagharibi wanafahamu hilo nasi twapaswa kufahamu pia. Nifafanue kidogo.

Arab spring ilpoanza pale Tunisia, ikasambaa kwa majirani Misri na Libya, ikapaa Yemen, huko ilifanikiwa maana tumeshuhudia huko kote umma ukiinuka dhidi ya madikteta wa muda mrefu wa nchi hizo na kufanikiwa, kwa msaada wa Marekani na Ulaya au la, kuwaondoa madarakani madikteta, kuwaua, kuwafunga maisha au kuwafukuzia mbali.

Lakini siyo pote ilipotokea Arab Spring, umma wa Waarab ulifanikiwa. Bahrain ilishindikana na Jordan ilizimwa. Kwa nini? Kwa nini madikteta wa Bahrain na Jordan walishindwa kungoka? Kama ni mfatiliaji wa siasa za Mashariki ya Kati utajua kwamba wafalme wa Bahrain wana urafiki wa ajabu na waMarekani maana America imeweka base zake pale na wapinzani wa wafalme wale walikuwa ni Waislam wa Kishia wenye uhusiano wa karibu na Iran - adui wa Marekani, hivyo waandamanaji hawakupata moral support kutoka Marekani. Jordan ina makubaliano ya amani na Israel na waandamanaji wa Jordan baadhi ya misingi yao kutaka kuwaondoa watawala wa Jordan ni kuvuruga ile amani ili kurudisha ule uaadui wa enzi baina ya Israel na Waarab. Wamagharibi wanayasoma yote hayo na hawapo tayari kussuport umma kijinga kijinga. Wanafatilia pia hata malengo ya umma husika.

Pale Syria, kundi la watawala ni Waislam wa madhehebu ya ki-Alawite (jamii ya Kishia) na wana uhusiano wa karibu na washia wa Iran. Wasunni walio wengi ndio wanaandamana kutaka Assad na kundi lake la Walawite waondoke madarakani. Kwa hiyo kuna element fulani msuguano fulani hivi wa vita ya kidhehebu (sectarian violence) baina ya Washia na Wasunni pale Syria.

Serikali yoyote makini haipaswi kuwa na upande kwenye misuguano ya kidhehebu, vita ya kijinga kama ile. Sisi watanzania tunapenda demokrasia, lakini hatupaswi kussupport wahuni wanaotumia dini kama kigezo cha kutaka kutawala. Hata Misri Hosni Mubarak msecular ameondolewa na nguvu ya umma eti kwa sababu amekaa pale madarakani muda mrefu, but gues what, badala ya demokrasia itawale baada ya dictatorship ya muda mrefu, Muslim Brotherhood ndio wamekuja kushika bunge na sasa wananyemelea urais. Na itikadi ya Muslim Brotherhood ni itikadi ya udikteta wa Kiislam (sharia kwa sana), kumwondoa Hosni Mubarak na kuweka Muslim Brotherhood ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga ma**.

Misuguano ya kiarab si mambo yetu, sisi twaweza mambo yetu ya Kiafrica. Waarab wanaishi kwenye ulimwengu mwingine anawaweza Marekani tu napo kwa taabu.
 
Tofauti ya Suni na Shia ni nini?
 
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.

Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?

Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?

TZ ni CHI MASIKINI, HATUFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE!
 
Sangarara, unauliza tofauti ya Sunni na Shia ni nini?

Well, kwa ufupi ni kwamba Wasunni na Washia huwa wanagombana kuhusu mrithi halali wa Mtume Muhammad(kati ya Imam Ali (Washia) na Maswahiba wengine wa Muhammad. Kama wewe si muislam huwezi kufahamu uzito halisi wa argument zao. Ni sawa na Wakatoliki na Waprotestant kuhusu theology za Bikra Maria au kunena kwa lugha and stuff. Kwa wasio waKristo they don't make sense.

Lakini kwa Washia na Wasunni ni ugomvi balaa. Msunni anaona Washia wanachafua theology na Washia hivyo hivyo. Ndio maana dini hazipaswi kupewa nafasi kwenye uendeshaji wa serikali. Dini zibaki kuwa private, tukikutana mtaani wote tujitambulishe Watanzania.

Ukitaka kujua uzito wa mambo ya Wasunni na Washia fikiria hili. Hamas political bureau (kile kikundi cha wapalestina wanaopinga Israel kwa nguvu zote) ikiongozwa na Khaleed Meshaal wameishi huku wakipata msaada wa fedha na mali na kushirikaiana muda mrefu sana kwa amani na starehe na bwana Assad wa Syria huko Damascus. Lakini Hamas ni Wasunni wakati Assad ni Alawite. Tofauti zilifichwa mpaka baada ya Muslim Brotherhood kupata nguvu Misri ambao ni Wasunni kama Hamas. Suprise, suprise, Hamas baada ya kuona Wasunni wa Syria wamemwinukia Assad, na Muslim brotherhood wamepata nguvu Misri, si wakamgeuka Assad? Sasa hivi Hamas wamehamishia makazi yao Misri na sasa hivi ni paka na panya na Assad. Sababu ni moja, Assad ni dhehebu tofauti na Hamas.

Unaona ushenzi wa ubaguzi wa kabila, au rangi au dini? Ni kama kula nyama ya mtu, Nyerere alituasa. Pale Syria kinachoendelea si kupigania demokrasia. Wamagharibi wamshagundua hilo na wapo reluctant kumpressure Assad au kuwasupport waandamanaji. WAssad ni dikteta lakini alijenga mshikamano baina ya makundi mbali mbali na dini tofauti nchini Syria. Wakristo Syria hawajawahi kupata kashi kashi chini ya Assad. Ndio maana Wkaristo wa Syria hawaungi mkono kupinduliwa kwa Assad. Wasunni wa Syria wana element za ugaidi ndani yao. Tayari wameshawafukuzia mbali wakiristo kwenye miji ya Homs, na mingine yenye Wassuni wengi. Tanzania iseme nini kweny complex situation kama hii?
 
Wanachotakiwa ni kulaani mauwaji ya wasikuwa na hatia na kushinikiza uwepo wa mazungumzo ya amani.
 
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.

Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?

Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?

Tanzania ni nchi masikini sana hawana upande kwenye mgogoro wa Syria mataifa makubwa ndio yana maslahi na mgongoro huyo ndio maana tumeona msimamo ya Urusi, China, wanatetea utawala wa Syria kwa maslahi yao na Marekani, Uingereza, Ufaransa, wanataka kuangusha utawala wa Syria kwa maslahi yao hapa Tanzania atasema nini zaidi ya kukaa kimya na kulaani mauaji tu.
 
sisi hatuna hata msimamo wenye kujali utu? what kind of neutrality is this? tembo anamkanya sisimizi halafu mtu anasema "hafungamani na upande wowote"? Mbona tuliharakisha kumlilia Gaddafi?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom