Msimamo wa ACT-Wazalendo na ziara ya mfalme wa Morocco hapa nchini

ACT yatoa Msimamo Juu ya Saharawi na Ziara ya Mfalme wa Morocco

Chama cha ACT Wazalendo kimestushwa Na taarifa kwamba Nchi yetu inabadilisha msimamo wake kuhusu Sahara Magharibi. Tumepata Taarifa kwamba Mfalme wa Morocco ataitembelea Tanzania Hivi karibuni Na kusaini mikataba mbalimbali ya biashara Na Nchi yetu Kwa ahadi kwamba Nchi yetu utaiunga mkono Morocco katika kuifukuza Jamhuri ya Sahrawi kutoka Umoja wa Afrika.

Chama chetu kinaomba ufafanuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje juu ya masuala yafuatayo:

• Ni kweli msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi umebadilika?

• Tanzania itaendelea kuitambua Jamhuri ya Sahara Kama dola Huru Na kulinda kiti chake katika AU?

Sisi ACT Wazalendo tunatangaza dhahiri kwamba hatutaunga mkono kuvunjwa Kwa Msingi Mkuu wa Sera ya Mambo ya Nje ya Nchi yetu ya kusimama Na wanyonge.

Iwapo Serikali itathubutu kuipa mgongo Jamhuri ya Sahara, tutahamasisha wanachama wetu Na Watanzania wengine wenye kuheshimu harakati za ukombozi kufanya MAANDAMANO Siku mfalme wa Morocco anaingia Nchini.

Kamati ya Mambo ya Nje ya ACT Wazalendo imeandika barua Kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba kikao naye ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu suala la SAHRAWI.

John Patrick Mbozu
Katibu, Kamati ya Mambo ya Nje, ACT Wazalendo
Oktoba 12, 2016.
Ingekuwa busara zaidi kama maswali yako ungempatia mwakilishi wenu bungeni ambapo mngeweza pata majibu stahiki ambayo yangekuwa hata kwenye records za hansard. Lakini kwenye kwa kutuma kwenye jamvi hili sidhani kama utapata majibu stahili.
 
Mimi nitaishi fikra za Baba wa taifa Mwal Julius K Nyerere KWA kuitambua Sahara kama nchi huru.
 
ACT yatoa Msimamo Juu ya Saharawi na Ziara ya Mfalme wa Morocco

Chama cha ACT Wazalendo kimestushwa Na taarifa kwamba Nchi yetu inabadilisha msimamo wake kuhusu Sahara Magharibi. Tumepata Taarifa kwamba Mfalme wa Morocco ataitembelea Tanzania Hivi karibuni Na kusaini mikataba mbalimbali ya biashara Na Nchi yetu Kwa ahadi kwamba Nchi yetu utaiunga mkono Morocco katika kuifukuza Jamhuri ya Sahrawi kutoka Umoja wa Afrika.

Chama chetu kinaomba ufafanuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje juu ya masuala yafuatayo:

• Ni kweli msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi umebadilika?

• Tanzania itaendelea kuitambua Jamhuri ya Sahara Kama dola Huru Na kulinda kiti chake katika AU?

Sisi ACT Wazalendo tunatangaza dhahiri kwamba hatutaunga mkono kuvunjwa Kwa Msingi Mkuu wa Sera ya Mambo ya Nje ya Nchi yetu ya kusimama Na wanyonge.

Iwapo Serikali itathubutu kuipa mgongo Jamhuri ya Sahara, tutahamasisha wanachama wetu Na Watanzania wengine wenye kuheshimu harakati za ukombozi kufanya MAANDAMANO Siku mfalme wa Morocco anaingia Nchini.

Kamati ya Mambo ya Nje ya ACT Wazalendo imeandika barua Kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba kikao naye ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu suala la SAHRAWI.

John Patrick Mbozu
Katibu, Kamati ya Mambo ya Nje, ACT Wazalendo
Oktoba 12, 2016.
Hii ndio ACT.....chama kichanga..akili nyingi...mambo makubwa.
 
Back
Top Bottom