Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Mtu anapofanya vema ama kutenda haki katika mazingira ya dhuluma tunayoijua tz yetu basi ni vema na haki tukampongeza. Hongera Kagenzi kwa kutuachia Nassari atuongoze kwa hapo Arumeru Mashariki. maana ungeweza kwa kulazimishwa ama kutetea kibarua chako ukamtangaza Sioi hata kama kashindwa na kusababisha usumbufu wa kesi mahakamani na vurugu na uvunjifu wa amani kwa wana arumeru. Ila wewe umekuwa mzalendo zaidi na kutenda haki. Kula dala kwa hilo.
 
huyu ndio alisimamia uchaguzi wa tarime baada ya kifo cha chacha Wangwe na chadema ikashinda huyu anatenda haki ila ccm watamchukia sana na ikiwezekana watamhamishia wilaya chovu kama nkasi au kasulu nk

Hivi kuna ukweli kuhusu CCM kuiba kura?.Na kwamba wasimamizi wengi wa uchaguzi wengi wao wakurugenzi si waaminifu?.Huyu jembe mtenda haki kila anaposimamia uchaguzi CHADEMA wanashinda,inawezekana akawa anapendelea chadema?
 
WAKUU,
KUMBE TARCIUS KAGENZI, YULE MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA ARUMERU EAST HAKUFANYA MAKOSA! AKIHOJIWA ALISEMA HATAUSAHAU UCHAGUZI WA ARUMERU, LAKINI KUMBE HUYU NDO ALIKUWA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO WA TARIME ULE ULIOZIBA PENGO LA KIFO CHA MBUNGE CHACHA WANGWE! ANAKUMBUKA VEMA ALIVYOLAZIMIKA KUMTANGAZA CHARLES MWERA WA CHADEMA.

MUDA MFUPI BAADA YA KUPOKEA MAAGIZO YA LUTENI YUSUF MAKAMBA KUWA AKAMTANGAZE KONGOYE WA CCM KUWA AMESHINDA BADALA YA MSHINDI HALALI AMBAYE NI MWERA, AKIWA NJIANI TOKA HOTELINI KWA MAKAMBA KUELEKEA HALMASHAURI KUTEKELEZA MAAGIZO YA MAKAMBA, ALIPATA SIMU TOKA KWA VIJANA WA CHADEMA NA MAZUNGUMZO YALIKUWA HIVI "tunajua unaenda kumtangaza kongoye badala ya mwera na unatekeleza maagizo ya makamba kuwa tangaza wakitaka waende mahakamani, sasa ukimaliza kumtangaza njoo hapa nyumbani kwako kwani kutakuwa na msiba mkubwa, kwani tumeshazingira nyumba na hatoki mtu huMU, fanya fasta tuje tuomboleze pamoja.

huyu kagenzi hakuweza kundelea kutekeleza maagizo ya makamba kwa gharama ya vifo vya familia yake, bali alimtangaza mwera, na kumfokea waziwazi makamba.

hiyvyo akiwa arumeru alikohamishiwa toka tarime, hilo hakulisahau, na asingeweza tena kuona familia yake ikiteteketea kwani anawafahamu vema wameru, tofauti yao na wakurya ni ndogo mno.


my take; haki yako hutapewa kwenye bakuli ya dhahabu, wenye masikio na wasikie.
 
Siku ile Mungu aliepusha balaa. Wale watu walisema walikuwa wamepanga kutoa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo. Kwa taarifa zilizokuwepo siku ile ilikuwa nyumba yake ichongechomwa moto kama angetekeleza maagizo yanayokiuka haki za binadamu. Aidha, aliyekuwa mgombea wa udiwani alisoma alama za nyakati akajiepusha na udanganyifu maana naye mabasi yake yangechomwa moto !!!
 
watanzania kiangalieni kwa makini sana hiki chama kinachohubiri kuchoma watu na familia zao
 
watanzania kiangalieni kwa makini sana hiki chama kinachohubiri kuchoma watu na familia zao

Watanzania kiangalieni sana chama kinacholenda kupora ushindi kwa kuwa ina dola.

Wakiogope kama ukoma chama kinachonadi sera za matusi, udini, na propaganda za kiongo na kutoa watu kafara ili mradi kishinde.
 
Kuna taarifa zinasema Kagenzi alipokea simu kutoka ikulu, aliambiwa mshindi wa halali atangazwe bila kuchakachuliwa, maana hataki kuona damu inamwagika.
 
What about Tendwa?? Hajaongea bado??

Huyu nae ni wale wale akina magamba. Si alimtishia Lema kwamba asiende Arumeru kwa sababu kawachefua wazee wa pale? Lema akaenda na akapokewa kama mfalme flani hivi (picha zipo hapa JF), hadi Tendwa yakamshuka
 
Back
Top Bottom