Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Nawaasa CDM central committee members kufanya tathmini ya kina ni kwa nini wapiga kura wamejitokeza less than 50% ????? ili kuweza kutibu hiyo tatizo kwa kutoa elimu kwa wapiga kura maeneo mengine

Daftari la kudumu la wapiga kura Tanzania lina matatizo makubwa. Lina GHOST VOTERS wengi ambao waliingizwa kinyemele na NEC 2010 ili kumsaidia JK kushinda uchaguzi. Kumbuka kura za URAIS hazihojiwi na chombo chochote kile under this SUN.

Tumeona Igunga, tumeona Arumeru Mashariki, asha kumu si matusi tutaona Segerea, idadi ya wapiga kura itaendelea kuwa ndogo kulinganisha na waliorodheshwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Jaji Damina Lubuva ili kulinda intergrity na credibility yako inabidi uli-UP DATE daftari la kudumu la wapiga kura, limejaa madudu yaliyoinginwa makusudi na Jaji Lewis Makame.

Halafu pia wapiga kura wanapungua kwasababu ya tabia ya CCM ya kununua shahada za wapiga kura. Ili kukomesha tabia hiyo mbaya NEC inabidi sasa waruhusu kutumika kwa form no 13 inayomuruhusu mwananchi aliyepoteza/aliyeuza (SIC) shahada kupiga kura. Hii itasaidia ku-discorauge CCM kununua sahada za wapiga kura. Kwani kama form 13 itatumika maana yake ni kwamba CCM wakinunua shahada still hao wananchi walio uza shahada zao wanaweza kupiga kura kwa kujaza form no 13, mwisho wa siku itakuwa imekula kwa CCM, kwani pamoja na kununua shahada bado wananchi wataweza kupiga kura. Kukataza kutumia form 13 kama NEC ilivyofanya Arumeru Mashariki kunachochea tabia ya CCM kuendelea kununua shahada za wananchi, hence contributing to low voters turn out.

Hongera sana CDM kwa ushindi wa Arumeru Mashariki, CCM na MITUSI yenu kajipangeni upya.
 
Mimi napingana na wewe
Hao waliojitokeza ndio wapiga kura halisi, na ninaweza kusema kwamba wapiga kura halisi wamejitokeza kwa zaidi ya asikimia 85% kupiga kura jana.

Hao wengine ni ghost voters, special kwa ajili ya kupenyeza mabox ya kura, wewe haujiulizi mabox ya kura waliyokuwa wanahangaika nayo jana walitegemea yakatumike vipi?

Tafakari
Hilo nakubaliana na wewe hizi figure zifanyiwe audit
 
Nawaasa CDM central committee members kufanya tathmini ya kina ni kwa nini wapiga kura wamejitokeza less than 50% ????? ili kuweza kutibu hiyo tatizo kwa kutoa elimu kwa wapiga kura maeneo mengine

Mkuu hii ni kazi ya tume ya uchaguzi na wala sio ya CDM.
TALK TO LUBUVA about this.
 
patoxic taratibu....usimchongee kagenzi kwa mwajiri wake....sidhani kama ni mere mwanamabadiliko ila ni msimamizi mzuri wa haki na maendeleo!!!

Your right Kweleakwelea, Kagenzi ana simamia haki ya watu wa Mungu, hapindishi mambo kwa kumfurahisha mwajiri wake bali anatenda na kutoa hukumu isiyo na upendeleo! Hataki moyo wake uchafuliwe na damu za watu kwani amekalibia kustaafu!

Tofauti na yule aliyestaafu anayependa kunywa damu za watu na kupanda majukwaani kulumbana na akina Dogo wa Butiama!
 
Huyu jamaa ni hazina kubwa ya taifa. Kila binadamu ana mapungufu yake lakini katika suala la kusimamia haki huyu bwana nampa 100%
 
"MSIMAMIZI wa uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi, amesema kamwe hawezi kusahau uchaguzi mdogo kutokana mvutano mkubwa uliokuwapo baina ya wafuasi wa CCM na Chadema."

“Niliyoyaona uchaguzi huu, kamwe sitayasahau maana ninaweza kupata PhD (Shahada ya Uzamivu) kupitia uzoefu niliopata kwenye uchaguzi huu,” alisema Kagenzi.


“Nilimuomba Mungu aniwezeshe kutenda haki na nilichokifanya ni kutenda haki, kwani mimi siwezi kumpendelea mtu au chama chochote au kuhujumu mtu au chama chochote cha siasa,” alisema Kagenzi.
 
Huyu ni moja ya mashujaa wa demokrasia Tanzania, kama haki inatendeka hakuna vurugu wala fujo
 
huyu ndio alisimamia uchaguzi wa tarime baada ya kifo cha chacha Wangwe na chadema ikashinda huyu anatenda haki ila ccm watamchukia sana na ikiwezekana watamhamishia wilaya chovu kama nkasi au kasulu nk

Wakimpeleka tu huko, uchaguzi mdogo utatokea na watapigwa chini tena
 
huyu ndio alisimamia uchaguzi wa tarime baada ya kifo cha chacha Wangwe na chadema ikashinda huyu anatenda haki ila ccm watamchukia sana na ikiwezekana watamhamishia wilaya chovu kama nkasi au kasulu nk
Kiuno chako. Nani kakuambia Kasulu ni wilaya chovu!
 
Hongera zake wanatakiwa kina Kagenzi kama 10 tu wasio na unafiki wala nidhamu ya uoga na tz itasonga.
 
Kwa kauli yake anajua kabisa kuna wasimamizi wengine uwa hawatendi haki na wanaegemea upande fulani!big up Mr. Kagenzi,mpenda demokrasia wa kweli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom