Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Mheshimiwa aliyesimamia uchaguzi wa Arumeru mashariki sio tu ameonyesha ukomavu tu. Huyujamaa alisimamia uchaguzi mdogo Tarime 2008 baada ya kifo cha Chaha Wangwe na haki ilitendeka tena chini ya Tension kubwa.

Nimemfuatilia kama angevulunda lakini huyu ni mwanamabadiliko aliyemo kwaenye mfumo dhalimu wa kinyonyaji. Akistaafu atakuwa mwenzetu. Kwasasa yuko levo nyingine.

patoxic taratibu....usimchongee kagenzi kwa mwajiri wake....sidhani kama ni mere mwanamabadiliko ila ni msimamizi mzuri wa haki na maendeleo!!!
 
Mheshimiwa aliyesimamia uchaguzi wa Arumeru mashariki sio tu ameonyesha ukomavu tu. Huyujamaa alisimamia uchaguzi mdogo Tarime 2008 baada ya kifo cha Chaha Wangwe na haki ilitendeka tena chini ya Tension kubwa.

Nimemfuatilia kama angevulunda lakini huyu ni mwanamabadiliko aliyemo kwaenye mfumo dhalimu wa kinyonyaji. Akistaafu atakuwa mwenzetu. Kwasasa yuko levo nyingine.

Katekeleza waajibu wake
 
Tanzania inahitaji watendaji waadilifu. Pongezi kwa Msimamizi wa uchaguzi kwa kutekeleza kazi yako inavyopaswa.
 
Nawaasa CDM central committee members kufanya tathmini ya kina ni kwa nini wapiga kura wamejitokeza less than 50% ????? ili kuweza kutibu hiyo tatizo kwa kutoa elimu kwa wapiga kura maeneo mengine
 
Trasias Kagenzi ameendelea kujizolea sifa kwa kusimamia chaguzi ndogo mbili bila kukipendelea chama tawala. Mwaka 2008 alikuwa msimamizi mkuu huko Tarime, CHADEMA kikashinda. Akahamishiwa Arumeru, uchaguzi mdogo umefanyika na CHADEMA wameshinda tena.

Ninavyoona, na ninavyojua fitina za chama tawala, Kagenzi hatahamishwa tena kwa kuhofia kuwa atakapohamishiwa uchaguzi mdogo utaitishwa na CHADEMA kitashinda.

Bravo Kagenzi kwa kusimamia haki.

Ninaamini atapangiwa kazi nyingine kuna uwezekano mkubwa wa kufanya rishafo ya wakurugenzi woote na yeye kuishia kupangiwa kazi nyingine ili kutoa fundisho kwa wakurugenzi woote ambao wamefikia mahala hawaaminiwi kabisa na wabunge wa CCM kusimamia mchakato wa kukusanya maoni ya mchakato wa katiba mpya.
 
Nawaasa CDM central committee members kufanya tathmini ya kina ni kwa nini wapiga kura wamejitokeza less than 50% ????? ili kuweza kutibu hiyo tatizo kwa kutoa elimu kwa wapiga kura maeneo mengine

Mimi napingana na wewe
Hao waliojitokeza ndio wapiga kura halisi, na ninaweza kusema kwamba wapiga kura halisi wamejitokeza kwa zaidi ya asikimia 85% kupiga kura jana.

Hao wengine ni ghost voters, special kwa ajili ya kupenyeza mabox ya kura, wewe haujiulizi mabox ya kura waliyokuwa wanahangaika nayo jana walitegemea yakatumike vipi?

Tafakari
 
Ukiangalia rekodi yake kwa kusimamia uchaguzi wa Tarime kwa haki na kutangaza matokeo ya haki na leo kafanya tena kwa serikali hii niijuavyo yupo katika hali mbaya. Tumuombee kila la kheri
 
Angalau nilianza kupata imani naye pale alipoamuru msaidizi wake awekwe ndani pale alipobainika kuwa alikuwa na kura bandia 2000 alizotaka kuchakachulisha ili kuibeba CCM huko Arumeru. Tuone Polisi na wasemaji wa TUME watahukumu vipi tukio hili, na watajisafisha vipi mbele yetu. Hii ndiyo inapelekea watu kukesha vituoni kulinda kura zao huku wakihukumiwa wao ndyio wanaoleta fujo. Sasa imejidhihirisha wazi ni nani chanzo halisi cha vurugu.
 
Nawaasa CDM central committee members kufanya tathmini ya kina ni kwa nini wapiga kura wamejitokeza less than 50% ????? ili kuweza kutibu hiyo tatizo kwa kutoa elimu kwa wapiga kura maeneo mengine

Hao ambao hawakupiga kura CCM walinunua vitambulisho vyao ila katika zile dakika 90 za mchezo CHADEMA walibana na CCM kushindwa kupenyeza kura zao zilizopigwa tayari! Ni hicho tu kilichotokea, wa jaribu kupata picha ni kiasi gani fweza ilitembea kununua vitambulisha kiasi cha hao 60,000 plus kushindwa kupiga kura!
 
Mpe tano!mzazi kagenzi akiweza atafute jimbo wahal CDM tutampa kiti bila kupigwa mpe tano tena!
 
Mheshimiwa aliyesimamia uchaguzi wa Arumeru mashariki sio tu ameonyesha ukomavu tu. Huyujamaa alisimamia uchaguzi mdogo Tarime 2008 baada ya kifo cha Chaha Wangwe na haki ilitendeka tena chini ya Tension kubwa.

Nimemfuatilia kama angevulunda lakini huyu ni mwanamabadiliko aliyemo kwaenye mfumo dhalimu wa kinyonyaji. Akistaafu atakuwa mwenzetu. Kwasasa yuko levo nyingine.

Msimpatie sifa asizostahili. Huyu bwana ni sawa na wasimamizi wote aka wakurugenzi wa halmashauri. Kuna wakati unafikia waliopo juu wanaona hakuna jinsi kwa mustakabali wa uongozi wao na kumwagiza aliyeko chini asimamie haki. Huyu bwana Kagenzi hakutangaza matokeo kwa amri yake bali amepewa greenlight na waliomteua na ime- happen kuwa hali tete inatokea wakati yeye akiwa msimamizi. Mbona uchaguzi wa 2010 alichakachua?, au mmesahau?.
 
Huyu bwana ni mtenda haki, I wish angekuwapo Shinyanga 2010, labda roho ya marehemu Kamanda Shilembe ingekuwa salama mpaka sasa!
 
mnamsifia nini wkt ni kazi yake
mmeshtukia alivokuwa anakosea kosea digits wkt akitangaza?
bila shaka alikuwa na matokeo aina tatu tofauti,kama sio ulinzi imara,
kuwa na mawakala wazuri wa chadema wasio hongeka kiraisi na nguvu ya mh lema
zile kura feki 10,000,na za yule mama aliengia na hotpot la chapati likiwa na kura feki
kushtukiziwa mdaa huu tungeongea mengine
kingine asili ya wameru hawapendi dhuluma waliamua kukesha na walikuwa tayari kwa lolote
yote haya imesaidia sana kushinda halali kwa chadema
 
Trasias Kagenzi ameendelea kujizolea sifa kwa kusimamia chaguzi ndogo mbili bila kukipendelea chama tawala. Mwaka 2008 alikuwa msimamizi mkuu huko Tarime, CHADEMA kikashinda. Akahamishiwa Arumeru, uchaguzi mdogo umefanyika na CHADEMA wameshinda tena.

Ninavyoona, na ninavyojua fitina za chama tawala, Kagenzi hatahamishwa tena kwa kuhofia kuwa atakapohamishiwa uchaguzi mdogo utaitishwa na CHADEMA kitashinda.

Bravo Kagenzi kwa kusimamia haki.

Kagenzi naye ni Mtanzania kama wengine, hawezi kushindana na mabadiliko. Roho yake naye inaumia pale kura zinapoibwa, hivyo huenda asiwe tayari kuchakachua kama ilivyo kwa Wilson Kabwe wa Mwanza enzi za Law Masha Vs Ezekia Wenje
 
Back
Top Bottom