Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Ajali mbaya iliyobeba roho ya mpendwa wetu Chacha Wangwe ili ilazimu tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi mdogo kuziba pengo la marehemu.Mapambano yalianza kama ilivyo sas katika jimbo la Arumeru.Tuache maneno mengi ngoja nikupe yaliyotokea wakati wa matokeo ya mwisho.

Ilikuwa hivi matokeo yalikuwa yanaonyesha CHADEMA imeshinda, lakin Mh(mume wa mwana mama machachari mbunge pale Bungen) alimtishia Mkurugenzi wa wakati huo na kumlazimisha aseme CCM imeshinda na kama atatangaza CHADEMA imeshinda Mkurugenzi atapoteza kazi.Kweli Mkurugenzi alisimamia msimamo wake wa kusimamia ukweli na haki na alitangaza CHADEMA kuwa mshindi.

Baada ya muda mkurugenzi huyo aliletewa barua yakusimamishwa kazi, kwa vile aliamini Mungu yu pamoja nae alifungua kesi mahakaman ambayo baada ya muda ilionekana hana hati na kurudishwa kazini,ila tu alihamishwa kituo na kupelekwa ARUMERU MASHARIKI ambapo ndio anasimamia uchaguzi mdogo.

Nikiripoti kutoka hapa Usa River mji mkuu wa jimbo letu tukufu ni mim Sunguratope wa jeifuuuuuuuuuuuuuu.

Sunguratope,

Kumbukumbu yangu inanionyesha huyu kagenzi alipokuwa mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya tarime na kusimamia uchaguzi ulioiaibisha ccm alifunguliwa kesi mahakamani, kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma wilaya moja ya mikoa ya kusini. Wakati kesi hiyo ikiendelea kuunguruma, akapata shutuma nyengine tena za kusafiri na gari ya halmashauri ya wilaya ya tarime hadi huko kusini kuhudhuria kesi yake, akihojiwa kwanini asijigharimie mwenyewe safari hizo kwakuwa hazikuwa na uhusiano na yeye kuwa mkurugenzi wilaya ya tarime. Sikubahatika kujua kesi hiyo iliishaje hadi nilipokuja kumsikia yuko wilayani meru.

Kwahiyo kusimamia kwake uchaguzi wa tarime kwa haki isijekuwafanya makamanda huko arumeru kurelax, kwani hata ccm wanamfahamu ni mtu wa namna gani na huenda wameshamuweka sawa ili asije kuwaumbua kwa mara nyengine, ama yeye mwenyewe atalazimika kuwabeba ccm ili kibarua chake kisije kufikia kikomo baada ya uchaguzi huu wa arumeru mashariki, kwahiyo huyu mtu ni wa kuangaliwa kwa umakini sana.
 
Naamini kuwa ccm wangesha muhamisha kama hayupo upande wao, ukichukulia kuwa historia yake wanaijua, lazma washajiweka sawa angle hiyo
 
Sijui kama wana Chadema wengi wana kumbukumbu za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru wa sasa ambaye pia ndiye msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Arumeru, Bw. Trasias Kagenzi. Kama hamkumbuki huyu huyu mwaka 2008 ndiye wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime, alimtangaza Charles Nyanguru Mwera wa Chadema kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. akimwacha mbali Christopher Ryoba Kangoye wa CCM.
Baada ya kujua hayo nadhani wana Chadema hamtakuwa tena na wasiwasi na huyu bwana cha muhimu kama mnaamini kura zitawatosha, basi zilindeni na kuhakikisha fomu zinazofika kwakwe ni zile zilizotoka kwenye vituo halali tu na si vinginevyo na huyo jamaa hana ajizi atawatangaza washindi, kama ilivyokuwa 2008.
Wakuu nawasilisha
 
mkuu hakuna gamba la kuaminiwa siasa za kipindi kile ccm walikuwa bado wanaringa leo hii wenyewe wanajua hawapendwi na katika uchaguzi usio na hila lazima wakae ndo mana siku hizi wanatumia nguvu kupita kiasi kila rasilimali waliyonayo inatumika polisi na mahakama na usipotii unaambiwa wewe chadema kama wanavyomsakama ocd wa arumeru ina maana hao wengine mambo yanaenda poa tuwe macho jamani
 
mkuu umetumwa na nani,unafikiri ccm hawajui alichokifanya tarime mpaka wamwamini Arumeru<<trust no body,tutalala vituoni
 
mkuu umetumwa na nani,unafikiri ccm hawajui alichokifanya tarime mpaka wamwamini Arumeru<<trust no body,tutalala vituoni
Nadhani nilimaanisha hicho hicho kwamba mhakikishe kura zenu ziko salama na hakuna mwanya wowote wa kuchakachua, haya sisi wapenda demokrasia tunatakia kila la heri bwana
 
Wakuu huyu jamaa ni jirani yangu kabisa.Jamaa ni mcha Mungu mno,ila nasikia baada ya kumtangaza wa tarime
alipigwa chini kwa muda usiopungua miezi sita.Sasa mtu kama huyo huwezi kujua analipa fadhila.Ukweli tuwe
makini.
 
Wakuu huyu jamaa ni jirani yangu kabisa.Jamaa ni mcha Mungu mno,ila nasikia baada ya kumtangaza wa tarime
alipigwa chini kwa muda usiopungua miezi sita.Sasa mtu kama huyo huwezi kujua analipa fadhila.Ukweli tuwe
makini.
hapa JF kuna magamba wanataka kuchanganya watu. CDM msiwasikilize watu kama hawa. So what? kama unamjua. CDM Fuateni maelekezo ya mh. Mbowe
 
Mziki wa Tarime ulikuwa mzito, pale hata kama msimamizi wa uchaguzi angekuwa JK mwenyewe ni lazima angemtangaza mshindi wa kweli. Arumeru wasimtegemee huyo mtu hata kidogo ila wao wafanye kama Tarime tuu.
 
Back
Top Bottom