KWA hisani ya manispaa ya Kinondoni msikiti wa Mtambani karibu na hospitali ya Dr. Mvungi na ubavuni mwa soko chafu na lenye harufu mbaya kuliko yote Tanzania umetunukiwa kuwa na udi na uvumba wa aina yake.
Udi na uvumba huu wenye harufu sawa ya mizoga iliyonyeshwea na mvua kisha kupigwa na jua na kisha tena kunyeshewa mvua au harufu mbaya ya maiti anayeendelea kuharibika kila kukichwa hakika huwafanya pamoja na imani yao Wsswalihina wa hapo kuishukuru serikali kwa kutosikiliza kilio chao miaka nenda, miaka rudi.
Manispaa hiyo ambayo imeruhusu vilabu vya pombe na maduka ya kuuza vileo yastawi karibu na msikiti huo inaelekea inawapenda sana waumini wa Kiislamu kwa hiyo wanaona raha waumini wakistarehe na harufu hiyo mbaya hata mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Inavyoelekea ni kwamba manispaa hiyo haina diwani wala mtendaji yoyote mwislamu kiasi ambacho maimamu hapa wameanza kudai kuwepo na serikali ya Kiislamu Tanzania- hasira yao ninaielewa mie ambaye nimeshindwa kabisa pamoja na jitihada zangu zote kuendelea kuswali msikiti wa Uvundo- au Mtambani kwa jina maarufu zaidi.
Harufu hiyo sidhani kama ina madhara. Maana kama ingelikuwa na madhara mabwana na mabibi afya wa Kinondoni bila shaka wangekwishaisharuri serikali hima kuondoa uvundo huu ili nao wapate thawabu za serikali isiyopendeka kupendwa!
Kutokupendwa huku bila shaka kunachangiwa si haba na watendaji na madiwani kuonekana kubweteka na kuyaachia matatizo kuendelea kuwa matatizo siku ingia, siku nenda!