Msiba

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Wapendwa wana JF nawatangazia msiba wa mdogo wangu aishie Dar. Alivamiwa na majambazi jana usiku mida ya saa 3 hivi. Walimpiga risasi sita na kufariki papo hapo. Mipango ya mazishi ni pale 92 hotel shekilango jioni hii. Mimi kwa sasa nipo njiani kurudi Moshi kushiriki pamoja na familia. Nitawapa taarifa zaidi pindi nitakapopata habari zaidi
 
pole sana mkuu wewe na familia,ndugu na jamaa zako kwa msiba huu mzito na wakinyama.


hawa majambazi huwa wana nishangaza sana,shida yao ni mali kwanini wanachukua maisha ya mtu pia? ni unyama wa hali ya juu.


Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi.
 
Pole sana, Ujambazi umekuwa tatizo kubwa sana hapa kwetu
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Mkuu pole sana, tuko pamoja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.
 
Pole sana Mkuu wewe na familia yenu yote kwa kumpoteza TUMAINI la maisha yenu. Tunawaombea faraja ya Mungu ipitayo hekima zote katika wakati huu mgumu wa maombolezo
 
Pola sana kwa msiba huu, Mungu aipe faraja familia yote wakati huu wamaombolezo na huzuni na aiweke roho ya marehemu pema peponi. Amina.
 
Pole sana Mangi
Mwemyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
 
Pole sana mkuu! Ni lile tukio la Kimara Temboni nini? Nasikia kuna watu wawili wameuawa kwa risasi maeneo hayo mida kama hiyo Ijumaa.
 
Pole sana Eeka kwa msiba huu mzito. Mungu akupeni nguvu ya kustahimili katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. May his soul rest in Eternal Peace. Amen.
 
kila nafsi hai itaonja mauti, Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu,
haiye sana mangyi
 
Back
Top Bottom