Msiba wa Mwangosi: Rais Kikwete ametoa Rambirambi?

Dhamira inamsuta. Walipoua kule Arusha, alisema kuwa mauaji yale yangekuwa ya mwisho, lakini yameshindwa kuwa ya mwisho kwa sababu maagizo wanayowapa polisi ya kuhakikisha mikutano ya CHADEMA haifanikiwi, ndiyo yanayosababisha vifo. Alaumiwe nani, polisi wanaotekeleza agizo la CCM au waliowapa maagizo?
Duu hata mimi hili la ukimya wa Mkuu wa kaya limenishangaza sana sijui ni uoga au nini , najua anapenda kujiweka mbali na ishu tata atakuja kuongea baadaye.
 
Ameumia mno, anahitaji muda ili afikiri namna nzuri ya kutoa rambi rambi, kifo cha mwangosi kina mambo mengi ndani yake, alikuwa cdm, alitaka kuwahoji ffu wakiwa kazini, hata hivyo, polisi hawakutakiwa kumuua wala kwenda kwa nguvu nyingi.

Nadhani, ni vizuri kwa waandishi kuendelea kuwa bila upande ili wasiwe na conflict of iterest
 
Yani unataka kutushawishi sisi watu na akili zetu tukubaliane na mawazo finyu kwamba mwandishi wa habari ama mwananchi yeyote anayekuwa Chadema anastahili kuuwawa na polisi? tena kifo chenyewe cha kinyama na kishenzi kiasi kile? Unajiona binadamu wa daraja la juu kwakuwa uko chama cha mabwepande?

Btw, una uhakika kwamba marehemu Mwangosi alikuwa Chadema? Prof. Mwandosya aliposema kwamba marehemu Mwangosi alikuwa kijana wake wa karibu sana na amemsaidia mara nyingi sana katika shughuli zake za kisiasa na kijamii wewe ulimuelewaje?

Hii ndio sera mpya ya serikali ya ccm na Raisi wake kutotoa salamu za rambirambi kwa watanzania wanaofariki kwakuwa tu ni wanaChadema!?
 
mimi naona bora tu hata asitoe maana haitakuwa na maana kama hajaweza kuwawahibisha waliotenda upumbavu huu, nashangaa sana rais kuwa namna hii, hata watendaji wake wa nao wabatunisha misuli mbele yake, hivi nchimbi alikuwa ba guts gani kutamka tena mbele ya waandishi wa habari kuwa hatajiuzulu, mwinyi hakujiuzulu baada ta mabmu kulipuka mara ngapi sujui, stupid country. hata baada ya waziri wa znz (cuf) kujiuzulu kufuatia kuzama kwa meli bado ccm hawakuwa na la kujifunza.

nchi wameifanya kuwa yao na familia zao.

Mungu shusha mkono wako tukomboe watanzania tunaangamia kwa kutawaliwa na waliokosa maarifa.
 
Katika kifo cha msanii Kanumba alitoa cash Tsh 2,000,000/=

Na hapa kwa Marehemu Daudi hata salamu ya pole ya mdogo hakudhubutu!

Ila kitu ninachoamini nikwmb hakika MUNGU yupo!

Kwa Kanumba alitoa million 2??

Serikali ikatoa million 10...................!!!

Wakalazimisha msiba uwe Dar badala ya Shinyanga ili Mkulu ahudhurie..........................!!!

Kwa Mnajimu Yahya.............. mazishi ilibidi yaahirishwe akazkwa kesho yake tofauti na taratibu za kiislamu kwa vile alikuwa safarini Namibia...................!!!

Maskini marehemu Mwangosi............................. Hata ka pole ka mdomo tu kamewashinda!!!
 
This is a good observation.It proves that what we have been thinking all along is true.That our president is not a serious president.To him issues of national significance,issues which concern the wananchi are not important.It's a pity.
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.
 
kwani mkulu yupo?? labda amekwenda swatzland kuangalia mabikra watakaoshindana mwakani ili kuolewa na king mswati!
 
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.

Mh! ni lazima kutoa ubani na tuhuma zote mlizompa? Kwa hili si rahisi mpaka hapo mambo yatakapotulia, nafikiri atatoa tu.
 
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.
Napenda style ya Kikwete. huwa anajiweka mbali na issue tata siku zote. well done JK.
 
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.

Nini Rambi rambi hata salamu za pole hajatoa siyo yeye,pinda,wala lukuvi.Connect the dot..Nafsi inawasuta
 
Acheni jamani Jei Kei naye ana UTU ndani ya Gamba lake hawezi ua alafu akatoa pole!.

Naona Yuko sahihi na akiitoa hiyo POLE basi ndiyo nitajua ni Mnafiki kwelikweli!
 
Kiongozi wetu ameenda Nchini Kenya kutoa ubani kwa wafiwa huko hapa nyumbani Ubani ni Majaliwa.........aaaaaaaaaa tusubiri wakati wa hitima
 
Rais wetu mpendwa ana sifa ya kipekee kuhudhuria misiba ya wanachama wenzake wa chama cha ma-freemason!Masikini Mwangosi wa watu hakuwa mwenzao, kakosa mkono wa pole wa rais wetu mpendwa!

Ingekuwa Mwangosi amezikwa nje ya nchi, siha shaka hata chembe kwamba dhaifu angekwenda kumzika ama kuhani msiba. I'm sorry kwamba Mwangosi kazikwa Mbeya ambako dhaifu hafagiliwi, mbaya zaidi kazikwa Tukuyu ambako anatoka mpinzani wake wa 'urahisi'! I'm sorry for that.
 
Back
Top Bottom