Msiba wa Mwangosi: Rais Kikwete ametoa Rambirambi?

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.

jakaya-kikwete.jpg

Rais Jakaya Mrosho Kikwete

Kifo cha Daud Mwangosi kimetikisa taifa na ulimwengu
Rais Kikwete amekaa kimya isivyo kawaida

  • Ni mwepesi kutoa rambirambi, hajafanya hivyo
  • Anakawaida kuhudhuria maziko yanayotikisa taifa, hajafanya hivyo
  • Aliwaahidia wanadipolomasia mwaka jana kuwa mauaji yale ilikuwa mwisho na haitatokea tena, sasa ndio mauaji ya kinyama yanazidi

Kawaida ya misiba mingi inayogusa jamii Rais Kikwete amekuwa mwepesi sana kutoa rambirambi, kuhudhuria maziko na pengine kutoa hata ubani kama ilivyotikea vifo vya watu mbalimbali wakiwemo wasanii kama hayati Kanumba. Msiba huo ambao umegusa na kushtua taifa lote, majirani, mataifa ya Afrika na duniani kwa kuona ukatili usio wa kawaida wa jeshi letu la Posili dhidi ya raia

Inashangaza Kikwete hatatamka lolote wala kutoa pole kifo cha Daud Mwangosi ambacho kimesababishwa na ukatili wa Jeshi la polisi, yeye Rais akiwa ndiye Jemadari Mkuu wa majesho yote nchini.

Aliwaahidia Wanadiplomasia kutotokea tena mauaji
Katika kumbukumbu zangu, Kikwete aliwahi kuulizwa na wanadiplomasia nchini (mabalozi) kuhusu mauaji yaliyotokea mara baada ya uchaguzi mkuu, mauaji ambayo yalitokea Arusha, North Mara ambako moja ya maiti ilitelekezwa barabarani na jeshi la polisi na kuwatishia wananchi.

Jibu la Rais Kikwete lilikuwa kama ifuatavyo:
"Nawaambieni mabalozi mauaji haya ni mwisho, nawahakikishieni tutafanya kila liwezekanalo kutotokea tena." Mwisho wa kumnukuru. Aliamua kuwadanganya Mabalozi hivyo isitokee bajeti kushinikizwa. Kitu cha kushangaza kumekuwepo mauaji mengi sehemu mbalimbali ambayo yanafanywa na jeshi la polisi ambalo liko chini yake kama amiri mkuu wa majeshi nchini. Hawa wanadipolomasia wakimuuliza leo imekuwaje mauaji yajirudie wakati ulituambia utahakikisha hayatokei tena, atajibu nini?

Ukimya wa Rais Kikwete, Ukimya wa Makamu wa Rais, Ukimya wa Waziri Mkuu na ukimya wa Rais wa Tanzania Visiwani inatia shaka mauaji haya ambayo wengi kuanzia viongozi wa mashirika mbalimbali yakiwemo ya dini na haki za binadamu wakilalamikia bila serikali kujali. Sina maana Rais na jeshi la polisi wamepanga mauaji, ila kutojali damu za wananchi zinazomwagika ni alama mbaya sana katika utawala ambao Rais mwenyewe amesema mara kadhaa anaendesha utawala unaofuata sheria.

Thubutu, akiwa na shida gani wakati akijua kwamba hatohitaji tena kura ya WaTanzania siku za usoni hata wakikichukia chama chake na serikali zima!!!!!!!!!!!!
 
Katika kifo cha msanii Kanumba alitoa cash Tsh 2,000,000/=

Na hapa kwa Marehemu Daudi hata salamu ya pole ya mdomo hakudhubutu!

Ila kitu ninachoamini nikwmb hakika MUNGU yupo!
 
Amehujumiwa na watendaji wake...

No no....internet ilikuwa down....

No server imeharibika......

Mama Salma alikuwa hampendi Mwangosi....

No nimesahau......alijua mwangosi ni mwandishi wa kenya....

Ok now i got it...alijua ni yule mkenya wa ulimboka ameuwawa...yes yes
 
Thubutu, akiwa na shida gani wakati akijua kwamba hatohitaji tena kura ya WaTanzania siku za usoni hata wakikichukia chama chake na serikali zima!!!!!!!!!!!!

Lakini hata kama hagombei tena uraisi kuna ubaya gani akituma salamu za rambirambi ama kutoa ubani? hilo ni suala la ubinadamu tu na kuonyesha kujali kwake.
 
Maneno mazito haya kaka, msiba huu umemchukiza na kumuhuzunisha sana mkuu wa inchi, bado anatafakari, hebu tumpe muda, huenda ubani uko njiani

Kweli anahitaji muda enh!? maziko yamefanyika na watu wanasubiri arobaini lakini mkuu wa kaya bado anatafakari?
 
Rais wetu mpendwa ana sifa ya kipekee kuhudhuria misiba ya wanachama wenzake wa chama cha ma-freemason!

Masikini Mwangosi wa watu hakuwa mwenzao, kakosa mkono wa pole wa rais wetu mpendwa!
 
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.
Huwa hutoa rambirambi kwa misiba ya wasanii wenzake kama vile Kanumba
 
Raisi Kikwete amejizolea sifa ya pekee ya kuwa mtu wa watu kutokana na kushiriki kwake kikamilifu katika shughuli za kijamii hususani misiba.

Pamoja na kushiriki kwake katika maziko lakini pia amekuwa akitoa ubani kwa wafiwa. Tunakumbuka alivyoshiriki kikamilifu msiba wa marehemu Steven Kanumba na kutoa ubani wa mamilioni ya fedha.

Tangu kutokea mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi, sijapata kusikia ama kusoma taarifa ya salam za rambirambi pamoja na kutoa ubani kwa familia ya marehemu.

Je ukimya huu wa raisi ni dalili za kupunguza mapenzi yake kwa wananchi wake?

Kama kuna yeyote ana taarifa za raisi wetu kutoa ubani ama salamu za rambirambi tufahamishane.

Duu hata mimi hili la ukimya wa Mkuu wa kaya limenishangaza sana sijui ni uoga au nini , najua anapenda kujiweka mbali na ishu tata atakuja kuongea baadaye.
 
Kutoa salaam za rambirambi sio lazima atoe kwenye magazeti.Ungewasiliana na wanafamilia kwanza.

Raisi wa nchi hafanyi kazi za kijamii kimyakimya, kila mara tunaona kwenye vyombo vya habari Raisi akitoa rambirambi kwa watu na makundi mbalimbali. Kwanini hii ya Mwangosi iwe kimya kimya kama kweli ametoa?
 
Back
Top Bottom