Msiba wa mpenzi na Sherehe ya ndugu!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,762
59,067
Guys..kama tunavyojua msiba hua haupangwi!Sasa ikatokea siku ambayo ndugu yako ana sherehe ambayo katika hali ya kawaida huwezi kukosa hata kama uko mbali!Siku hiyo hiyo kwa bahati mbaya mwenzi wako (hata kama hamjaona..kwenye mahusiano ambayo ni solid kiasi cha kushirikiana mambo ya kifamilia)akapatwa na msiba wa mtu wake wa karibu sana (kaka..dada..mama..baba n.k!)...utaenda wapi??Kusikitika na mpenzi au kufurahi na familia yako!!
 
hii ngumu, itabidi mpenzi aliyefiwa awe muamuzi, maana hata akiamua uende huko kwenu then hatakasirika. na kama mtu anajua mpenzi anamuhitaji basi hapo. ila msiba kama upo mji mmoja unaenda muda ukifika, kama mji mwingine basi kazi
maelewano mie naona
 
haina ugumu wowote, unaenda kwanza kwenye msiba halafu baadae ndiio kwenye sherehe
 
Lizzy, msibani kwanza na kama bado kuna muda wa kutosha kwenye sherehe vinginevyo hakuna ubaya kuikosa sherehe kwa kuamua kwenda msibani. Mzima wewe?
 
Mimi naona hapo ni wakati mzuri wa kuonyesha mapenzi yako kwa mpenzi wako.Na inabidi mtu umfariji mwenzako kadri ya uwezo wako maana sherehe haziishi itakuja nyingine tu.Lakini msiba mtu anakufa mara moja,na ikumbukwe kuwa kama utamwacha mwenzi wako katika wakati mgumu kama huo naye lazima atajiuliza kuhusu mapenzi yako kwake,na unaweza kuishia kumkosa mpenzi wako sababu ya sherehe ya siku moja.
 
Guys..kama tunavyojua msiba hua haupangwi!Sasa ikatokea siku ambayo ndugu yako ana sherehe ambayo katika hali ya kawaida huwezi kukosa hata kama uko mbali!Siku hiyo hiyo kwa bahati mbaya mwenzi wako (hata kama hamjaona..kwenye mahusiano ambayo ni solid kiasi cha kushirikiana mambo ya kifamilia)akapatwa na msiba wa mtu wake wa karibu sana (kaka..dada..mama..baba n.k!)...utaenda wapi??Kusikitika na mpenzi au kufurahi na familia yako!!
Hapa pazuri! Kuna mambo mawili...
Naona Mapenzi na Huzuni.
Msibani hakuna mapenzi ila kuna Huzuni...kwenye sherehe kuna Furaha.
Hivyo ni vizuri uanze kwenye Huzuni.
Ila mtihani utakua ...iwapo hiyo Sherehe kutohudhuria kwako haitofanyika...hapo utatia akili ya kuchanganya na zako!
Kisha kwenye msiba hata usipoenda hautoharibu au kukosekana kwako mambo yataenda..hapo utachanganya akili zako na muhusika!
Ila ni vizuri kuangalia wapi uwepo wako ni muhim zaidi.
 
Mi mzima mpendwa!Vipi wewe?

Miye poa kabisa, namshukuru Muumba wetu. Hiyo avatar yako Mhhhhhh! naona jamaa analinda mali zake hahahahahahah. Mwambie asiwe na wasi na BAK hahahahahah.

 
Jamani msiba muusikie tu kwa jirani lakini ukikufika hasa kwa mtu wa karibu,huwezi kuthamini tena mambo ya sherehe kama una akili,kujumuika msibani ni kujaribu kutoa faraja kwa mfiwa kwani death is among the best of imposibles
 
Jamani msiba muusikie tu kwa jirani lakini ukikufika hasa kwa mtu wa karibu,huwezi kuthamini tena mambo ya sherehe kama una akili,kujumuika msibani ni kujaribu angalau kutoa faraja kwa mfiwa kwani death is among the best of imposibles
 
Back
Top Bottom