Mshtakiwa Kesi ya Utoroshaji wanyama atoweka kama Sailesh Vithlani

Kufuatana na kutoroka kwa huyu mpakistani anayeshutumiwa kwa kesi ya kuhujumu uchumi kwa kufanikisha wizi wa wanyama pori wetu, kuna watu wawili wanaotakiwa kukamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka ya kutumia madaraka yao kuhujumu nchi; watu hao ni jaji wa mahakama kuu aliyetoa dhamana kwa kesi isiyoruhusiwa kupewa dhamana, wa pili ni yule aliyemrudishia pasi ya kusafiria wakati mtuhumiwa hakuruhusiwa kutoka nje ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Hawa wasweke lupango halafu waseme kama walikuwa wameamrishwa na wakubwa zao kukiuka sheria, nao pia wachukuliwe hatua zifaazo.
 
Back
Top Bottom