Mshikamano Toronto:Binti Mtanzania Yuko ICU

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,426
Wana bodi, kama kawaida yetu sisi Watanzania hushirikiana kwenye shida na raha, kuna binti Mtanzania kwa jina la Eva Gembe, aliyekuwa amelazwa ICU hospitali moja mjini Toronto nchini Canada akisumbuliwa na Brain Tumor, amefariki dunia.

Up-date 1.
Kwa Toronto, msiba uko kwa Dada wa Marehemu, Juliet Gembe, alikuwa mwanahabari Channel Ten kabla hajaelekea Toronto. Mopango ya kuurudisha mwili nyumbani kwa mazishi inafanywa na Watanzania walioko Toronto, ikiratibiwa kwa karibu na Jamii ya WaTZ wa hapo Toronto.

Kwa Dar es Salaam, msiba uko nyumbani kwao, kwa Mzee Gembe, lile ghorofa pale Upanga, baada ya Califonia Dreamer.

Kazi kubwa kwa sasa ni resources mobilization mwili wa Dada yetu tuurejeshe nyumbani.

Update -2
MSIBA TORONTO, CANADA

Marehemu Evaline Gembe

Familia ya Bwana na Bibi Gembe wa Upanga-Dar-es-salaam na Tabora, wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Evaline Gembe(pichani) kilichotokea hapo juzi tarehe 30.3.2010 huko Toronto,Canada. Evelyne amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa dada yake, Julie huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka. Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : CIBC (Canadian Imperial Bank of Commerce)

ACCOUNT NUMBER: 5681839
TRANSIT NUMBER: 00902
INSTITUTE NUMBER: 010
SWIFT CODE: CIBCCATT

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwa Sania Esmail.Anuani yake ni saniae@yahoo. ca au kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:

1025 SCARLETT ROAD,

APT 606, BUZZ # 178
TORONTO ON, M9P 3V3.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Julie +1 416-247-8318
Esmail Manambi- +1 647- 299-2572
Victor Wambura- +1 647-428-4118
Prosper Luteganya- +1 905 626 3764

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi - Amen.

Source. Michuzi


Poleni wafiwa wote,

RIP Eva Gembe.
 
Mungu ampe rehema zake kama ni ndugu jiran wa karibu simamia maandiko haya
ukiwa unasali Biblia inasema"SITAKUFA BALI NTAISHI NIKIYASIMULIA MAKUU YA BWANA" Eee Mungu ulie hai unaesamehe maaelfu na maelfu na kuwarehemu tunaomba mrehemu ndugu yetu huyu ambae kwa mamlaka uliotupa na maandiko si haki yake kuishi kwa kutumia machine mwenyezi mungu wewe ndie njia yetu sote...tunakukabidhi ndugu yetu huyu mrehemu dhambi zake zote alizofanya kwa kuwaza kunena na kutenda...hakuna linashindikana kwako ee baba
tunavunja nguvu za giza zilizo mkuta mpaka sasa akiwa ICU...tunakataa roho ya kuishi ICU...ulisema baba katika kitabu cha HESABU 14:28 Lolote mtakaalosema nitafanya kwa mamlaka uliotupa tunatangaza ndugu yetu kuwekwa huru tunamtoa huko ICU kwa jina la YESU
ukiwa kama mcha Mungu wote na tuseme
Amen
 
Ni kitu kizuri kusaidia hope wale waliopo jirani wanaweza kufanya the needful help. Lakini Mkuu Pasco ungejitahidi kuweka bayana ni msaada gani unahitajika zaidi hasa ukizingati binti yuko ICU kwa sasa
 
Mungu keshamsaidia, kwanza kwa kutokuwepo Bongo na uvimbe wa ubongo ni nafuu kubwa kwake. Sasa tuombe tu dawa/ upasuaji/ mionzi zifanye kazi na madaktari na wauguzi waongozwe na Roho wa Mungu katika kumhudumia
 
Ni kitu kizuri kusaidia hope wale waliopo jirani wanaweza kufanya the needful help. Lakini Mkuu Pasco ungejitahidi kuweka bayana ni msaada gani unahitajika zaidi hasa ukizingati binti yuko ICU kwa sasa
.

Kwa mgonjwa wa ICU, kinachohitajika zaidi ni maombi, sala na kuonyesha mshikamano, solidarity kuwa Watanzania ni wamoja 'we are one wherever we are'.

Natanguliza shukrani.
 
Wana bodi, kama kawaida yetu sisi Watanzania hushirikiana kwenye shida na raha, kuna binti Mtanzania kwa jina la Eva Gembe, aliyekuwa amelazwa ICU hospitali moja mjini Toronto nchini Canada akisumbuliwa na Brain Tumor, amefariki muda mfupi uliopita

More update coming soon.

RIP Eva Gembe.
 
Mungu ampe rehema zake kama ni ndugu jiran wa karibu simamia maandiko haya
ukiwa unasali Biblia inasema"SITAKUFA BALI NTAISHI NIKIYASIMULIA MAKUU YA BWANA"
Amen

huwezi kuibuka out of no where na kusema sitakufa bali nitaishi kuyasimulia matendo makuu ya Bwana. Mungu sio mfanya niashara ya neno. inatakiwa uwe mtendaji wa neneo kabla.
 
Thats sad RIP

Raha ya milele umpe Ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa Amani. Amen
 
huwezi kuibuka out of no where na kusema sitakufa bali nitaishi kuyasimulia matendo makuu ya Bwana. Mungu sio mfanya niashara ya neno. inatakiwa uwe mtendaji wa neneo kabla.

Wewe mbona mkali hivo? Mi sioni tatizo hapa, just feel sorry for our deceased sister please
 
Wana bodi, kama kawaida yetu sisi Watanzania hushirikiana kwenye shida na raha, kuna binti Mtanzania kwa jina la Eva Gembe, aliyekuwa amelazwa ICU hospitali moja mjini Toronto nchini Canada akisumbuliwa na Brain Tumor, amefariki muda mfupi uliopita

More update coming soon.

RIP Eva Gembe.

Msaada unatafutwa ni kuhusu maziko yake au namna gani ya kusaidia, wekwni taarifa nzuri ndg zangu.
 
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...JINA LA BWANA LIHIMIDIWE...dada EVA sisi tulikupenda sana lakini BWANA AMEKUPENDA ZAIDI...kapumzike kwa amani....AMEN
 
Back
Top Bottom