Mshenga kazua balaa

Edmund

Senior Member
Jul 17, 2009
123
62
Najiandaa kuoa, hivyo nikawajibika kutafuta mshenga,
Nikafanikiwa kumpata Mzee mmoja wa miaka 80 hivi lakini alifiwa na Mke miaka 16 nyuma.
nikiamini kwa umri wake na busara zake nikaona nimekula dume kumbe wapi,

UTATA UKAJA

Mara akaanza kujenga na mazoea na Mama Mkwe wangu (Mjane) kwa takribani miaka 22 sasa)
mara outing mara lunch lakini sio siri tena wapo ndani ya DIMBWI LA MAPENZI na kwa tetesi tu nasikia wanataka KUOANA.

Wana JF hii ni haki kwangu, kwao, Binti yao pamoja na familia yao na yangu?.
 
Sasa wewe mama mkwe na mshenga kua kwenye mapenzi inakuuma nini?!Nashindwa kuelewa kwanini hilo ni tatizo kwako....usijekuta unampenda mma mkwe kisiri siri!
 
ahh wewe jaman ..sasa shda ipo wap jaman?
mshenga baba yako?

akiwa na uyo mamamkwe wako kuna ubaya gan?ni ndugu ?

wewe endelea na mishe zako za ndoa/ mahusiano yao yanakuhusu nini?
au unaona wivu lyk ulimsogezea migo mshenga?

ao ni watu wazima na si ndugu km wamependana its ok ....HAIKUHUSU NA HAIDHURU MIPANGO YAKO YA NDOA ATA KDG

labda ingekuwa MSHENGA ANAMNYEMELEA MCHUMBA WAKO...UMENIPATA?
m done m out!!!

te
 
He! Kwani hapo shida yako nini? Ulitaka kuwa na mama mkwe mjane asipate mwenzake? Mimi nadhani ungelifurahi kuoa kwako wewe, kumeleta baraka zaidi kwa familia ya mkeo mtarajiwa! Msaidie mshenga na mama mkwe kuandaa sherehe ya harusi, Au una jengine? We vipi???? :violin:
 
And they lived happily forever! Napenda sana stori za staili hii
 
Edmund mbona haihusu kabisa, ilibidi ufurahi maana hata mali waweza pangiwa kidogo huyo mshenga aki bargain!
 
kwani huyo mshenga ndugu yako? as long as haikuadhiri kwenye ndoa yako shida n nn?
treeeeeee au unahofia kupata baba mkwe teh teh teh
 
Kama hujaona basi tafuta mshenga mwengine maana mdingi ameshakuwa baba yako wa kufikia, tehe tehe tehe

Otherwise, wewe si unapewa mambo, shida iko wapi????
 
Barua ya posa kapeleka? Na majukumu mengine ya ushenga anayatekeleza? Basi we subiri ndoa mapenzi yake na mama mkwe hayakuhuuu.
 
Najiandaa kuoa, hivyo nikawajibika kutafuta mshenga,
Nikafanikiwa kumpata Mzee mmoja wa miaka 80 hivi lakini alifiwa na Mke miaka 16 nyuma.
nikiamini kwa umri wake na busara zake nikaona nimekula dume kumbe wapi,

UTATA UKAJA

Mara akaanza kujenga na mazoea na Mama Mkwe wangu (Mjane) kwa takribani miaka 22 sasa)
mara outing mara lunch lakini sio siri tena wapo ndani ya DIMBWI LA MAPENZI na kwa tetesi tu nasikia wanataka KUOANA.

Wana JF hii ni haki kwangu, kwao, Binti yao pamoja na familia yao na yangu?.

Bwana mdogo ondoa shaka ndoa iko palepale, tena tarajia punguzo (discount) kubwa sana ya mahari
 
nashukuru kwa ma idea ya kutosha sikuwa na mawazo haya hata kidogo,
 
Yaani wakati naanza kusoma nikadhani mshenga wako kamgeuzia kibao mchumba wako na wanaendelea wewe ndio imetoka, kumbe mshenga na ma mkwe? kwani hao ni ndungu? kama sio sasa ni balaa gani unalomaanisha wewe hapo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom