Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Niliwai kuona kada wa CCM aitwaye Sabodo akichangia CDM fedha, CCM wameshindwa nini kulijadili hili lilifanyika adharani!?
 
Kutokana na kuchukiwa kila upande na Watanzania na kuihofia CHADEMA serikali na CCM wameamua kuipakia JF kuwa ni mali ya CHADEMA bila kutoa ushahidi(refer Nipashe ya April 12).

Yaani wao kila awapingaye sasa hivi ni CHADEMA wakati si kweli. Binafsi ningependa kulaani kauli hii yenye nia ya kuibana JF. WATU WOTE WAKO HURU KUJIUNGA HUMU bila kujali itikadi zao. Labda kwa vile watendaji wa CHADEMA kama Dr Slaa,Zitto,John Mnyika na Regia Mtema wao wameamua kutumia ID zao za kweli ndio maana wao wanahukumu hivyo. Tunajua kuwa vigogo wengi wa serikali na CCM ni members humu.

We say JF SHALL NEVER DIE
 
Kutokana na kuchukiwa kila upande na Watanzania na kuihofia CHADEMA serikali na CCM wameamua kuipakia JF kuwa ni mali ya CHADEMA bila kutoa ushahidi(refer Nipashe ya April 12). Yaani wao kila awapingaye sasa hivi ni CHADEMA wakati si kweli. Binafsi ningependa kulaani kauli hii yenye nia ya kuibana JF. WATU WOTE WAKO HURU KUJIUNGA HUMU bila kujali itikadi zao. Labda kwa vile watendaji wa CHADEMA kama Dr Slaa,Zitto,John Mnyika na Regia Mtema wao wameamua kutumia ID zao za kweli ndio maana wao wanahukumu hivyo. Tunajua kuwa vigogo wengi wa serikali na CCM ni members humu.

We say JF SHALL NEVER DIE

CCM wafanye mpango wanunue hii site kama wanaona ina manufaa kwao, kuanzisha mpya itachukua muda kuzoeleka
 
chuki na upendo nia matokeo ya mahusiano.

Jiulize unapaswa kufanya nini kwa nani na kwa wakati gani?

Usiishie hapo endelea kujiuliza je umefanikiwa? Kwa kiwango gani.

Halafu evaluate na ujiulize unastahili nini kati ya chuki na upendo!!!
 
Jamani wamemsahau malaria sugu na wenzake kina majimshindo je hao wote ni mahasimu wa ccm?
 
Mlio wengi humu ni chadema..... Sisi tuko wachache hiyo ni fact na siyo dhambi kwenu ila ni dosari kwetu

Forum hii haichagui dini, rangi, kabila, wala itikadi, it's for everyone, tunawakaribisha ccm kwa wingi tuje tubadilishane mawazo, karibuni sana.

RED:Ninyi kina nani? ccm? Don't worry, mshauri wenu ameshauri na ninyi muwe na forum yenu,so just be patient nanyi mtautumia huo kunyanyasa baada ya 2015, wakati mkiwa wapinzani, how do you like that?
 
Huu ni UJINGA wa hali ya juu. Yaani mie kuwa JF tayari nimekuwa MALI ya Chadema?

Mtu mwenyewe hata Kadi ya chama chochote sina na leo unaambiwa "umemilikiwa na Chadema."

JF ni watu na wala siyo Maxence Melo au sijui nani. Wale ni wadhamini wetu tu.

Ukitaka kuamini hilo, jiulize kitu kimoja: Kuna forum nyingi sana za Watanzania na Blog kibao ila kwa nini JF ndiyo inatesa namna hiyo? Ni kwa makala za wadhamini wa JF au MEMBERS wa JF?

Michuzi Blog ingeliweza kuwa kwenye nafasi ya JF leo hii ila kutokana na Michuzi kubania thread za watu na comments za watu, Michuzi blog imebakia kuwa kama kitawi cha CCM na Bwawa la Maini. Blog nyingine ya wauza nywele nayo iko juu na sababu ni kuwa wanafanya vizuri sana katika Issue ambazo wameamua wazifanye. Hata Ze-Utamu na yeye alifanikiwa saaana kwa sababu HAKUBANIA habari za watu.

JF imekuwa wazi kwa watu na kuachia habari ziandikwe na kuachwa hata kama ni SIRI NZITO ya Serikali. Zimeondoloewa tu zile ambazo au zinatukana au zina majungu. Kuachia habari huku zisomwe na watu wote wanaoingia JF ndiyo kumeifanya JF iwe hapo ilipo na kuwapa SIFA za UJASIRI wadhamini wa JF.

Ila leo mtu akija na kusema JF ni mali ya Chadema ni sawa na kusifia Jiko fulani linapika vizuri na LIMEDHAMINIWA na fulani na unasahau kuwa WAPISHI wake wakihama, jiko litabako historia. Wanataka kusema mtu kama FMes ni Chadema? Kibunango ni Chadema? Malaria Sugu, Mwiba, Junus, Kishonga, Ndalu, Tumaini, Ngongo, X-Pasters na wengine wengi wanaoshinda hapa wakimtukana Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla na wao wamekuwa ni Chadema?

Hebu mwangalia Waberoya na makala zake, unataka kusema huyo ni Chadema?

Kweli MFA MAJI, HAACHI KUTAPATAPA.......... Atashika hata kitoto cha Ndege/bata ili asizame.

Mkuu kuna contradiction kati ya utetezi wako na signature yako!
Anyway,..
Sidhani kama ukiwa unajiunga JF kuna masharti kwamba uwe mwana chadema,..
Sidhani kama viongozi wa chadema wote humu wanajua JF ina endeshwaje,..naweza kuwa najua kidogo ila kwa ulelewa wangu JF inaendeshwa na members wanao jitolea kuchangia kidogo na sio chama cha siasa (sijui kama chadema imewahi changia lakini,na hata ikichangia hiyo haiifanyi JF kumilikiwa na mchangiaji).
JF inapata umaarufu kutokana na content za vitu vinavyo patikana humu na jinsi ilivo friendly!
Sio kila anae ingia humu ni mwana chadema,wengine,tena wengi tu wanaishia jukwaa la MMU,na ndicho kinacho waleta humu!

Kama JF ingekuwa ya chadema,basi kina zitto wasinge kuwa wana lalamikiwa hapa na kuchafuliwa au kukosolewa maana tunajua media za habari za chama ni kukipamba na tena kama kuna kukosoana sio hadharani kama JF,JF kuna kila kitu wazi!

Kama JF ni ya chadema,kupambana nayo sio kuanzisha forum na wewe bali kufanya mambo mengi mazuri yatakayo jadiliwa na kuchangiwa humu na member wa ccm ambao ni wengi sana humu!

Kuna forum nyingi sana duniani,ila kwa forums ninazo zijua mimi hakuna forum nzuri kama JF,...hebu angalia
www.jamiiforums.com
MwanaKijiji.COM
Political Forum - US & World Politics Forum
CodingForums.com- Web coding and development forums. Get help on JavaScript, PHP, CSS, XML, mySQL, ASP, and more!
Computer Forums

na zingine nyingi ila yenye watu wengi ni Political Forum - US & World Politics Forum ambayo ni elf20 zaidi ya JF!

Point ni kwamba: wakifikiria kuanzisha forum au blog yoyote itakuchukua mda gani kuweza kushindana na JF?
wanadhani watashinda?
au kupambana na JF ni kuifungia kwa hila yoyote ile labda?
Wazo:wajiunge JF kwa wingi tu,na watetee mambo yao kwa hoja za maana sio kulete watu kama kina naniii humu
 
naona hawa "consultants" ni wasomaji haswa wa michango ya humu jf, lakini kinachonikera ni kufikiri hii ni forum ya chadema!!!!!
Mimi sijifichi ni mwana ccm lakini nakerwa sana na ufisadi na mafisadi.

Ccm imelilea hili tatizo kwa makusudi, sasa viongozi wetu walitegemea nini haswa?-kupongezwa kwa kula na kunywa na mafisadi? Na je wao kweli hawkuliona hili tatizo hadi waambiwe na the so-called "consultants".

Hapa ndipo panaponisikitisha maana nakitakia mema chama changu, na je vikao vingi vinavyo endesha chama vimeshindwa kuona makosa yanayotendeka?

I fear for ccm.

Uzuri wa jf ni kutoa maoni huru ili kujenga na kusahihisha makosa, kwa ripoti ya "consultants" inaelekea ujumbe umefika panapostahili na hatua zimechukuliwa-this is a positive move.

Kwa mantiki ya kufikiri kuwa jf ni ya chadema ccm itafanya kosa la kuanzisha forum yake ambayo itakosa mvuto kama itakuwa kazi yake ni kusifia viongozi na kuwapamba-kama afanyavyo issa michuzi na blogspot yake. Fuatilia kwa makini issa michuzi blogspot na utaona idadi ya watu wanaotembelea pale imekuwa ikipungua kadri sifa za viongozi (hata wale mafisadi) zinavyozidi kupambwa.

katika hili umenena.sisi wanajf hatuna kitu cha kusifia tu pia tunahitaji kulaumu.ccm ikianzisha hapo hiyo forum labda kama watakuwa wanafuta thread zetu vinginevyo wataikimbia.wakati wa kusifia ccm si huu tena.hakisafishiki.ccm ina kosea kuendekeza ukiritimba.ufamilia ni mwingi.ukihiyo ndo usiseme.watazame wanachama wake hivi sasa.wengi hawana uwezo wa kufikiri ni kupiga makofi tu.zidumu fikra za chairman.kwanini riz ana nguvu zaid kwenye uvccm?consultants wamewapotosha.
Vyombo vingi vya habari vina iogopa ccm.kazi kubwa ni kusifia tu hadi mwisho.waandishi wengi aina ya muhingo rweyemamu wanasubiri hisani za safari na kuitwa kwenye semina.wajirekebishe.siipendi ccm hata kidogo.
 
Jf ina member around 35 elfu halafu wanaotembelea jukwaa la siasa ambalo mara nyingi linawachambua ccm kila nikiangalia hawazi 150 masaa 24 na wengi ni walewale wa kila siku sasa hii idadi ya watu ni uwiano wa ngapi kwa taifa zima. Utangundua watu wanaotembelea Jf ni wachache mno.

Na kwa taarifa za ukweli watu wanaotumia mtandao kanda ya ziwa ni wachache mno lakini kwa siku za hivi karibuni sidhani kama kuna sehemu ccm inachukiwa kama Mwanza hata na walalahoi wasio jua hata Jf ni nini. Labda jambo ambalo linalozidi kuiua serikali ya ccm kwa sasa ni tiba ya Loliondo, jana nimetembelea Bunda ambako ni kituo cha kuondokea kwenda kwa babu. Kwa wastani kila siku mtu anakufa wananchi wanailaumu serikali kwa kuwachelewesha mpaka wanafia Bunda, hapa serikali ya ccm inapandikiza chuki bila kujua na sijajua kama hili wameliona.

Serious ccm wanajimaliza wenyewe.
 
hawana sera mbadala hawa..........jf ipo kwa kila mtu........haichagui haibagui............kwanza haiulizi wewe ni chama gani wakati wa kusign up au kadi yako ni namba ngapi............hawa vipi? kama wameshindwa shauri yao na mwaka huu mtajibeba
 
CCM wamekuwa kama mgonjwa aliyepima na kukutwa ana ugonjwa ambao ni terminal na prognosis inasema hataishi zaidi ya mwaka mmoja, mgonjwa huyu atakuwa kwenye denial state na kuamua kutafuta daktari mwingine ambaye atamwambie kinyume cha matokeo ya uchunguzi wa awali.

CCM kuwatumia ma-consultant kama kina (Kinana) badala ya kutumia scientific approaches wao wanakuwa na personal opinions kama ndiyo jibu. Mimi ndiyo ningekuwa consultant wao ningeanza na utafiti wa kisayansi kwa kuangalia pre 2005 states of minds ya wananchi kwa nini JK alipata 80% of total votes. Then nikaja kwenye kipindi wakati akiwa rais wananchi wangependa afanye nini hata kama asingeweza kuwafanya kuwa na maisha bora.

Kwa nini consultant hawa wanaihusisha JF leo hii kuwa ni ya CHADEMA na haikuwa hivyo mwaka 2006 kabla ya kashfa mbalimbali kuanza kuwa surfaced?, Huwezi kulaumu vyombo vya habari au mitandao kuwa inakufanya uporomoke umaarufu kama tu wewe hufanyi vitu vitakavyokuporomosha umaarufu wako. Ule utamaduni wa funikafunika wa kuficha uozo ndiyo adui namba moja wa CCM katika kipindi hiki cha utandawazi. Hata kama CCM itaanzisha vyombo vyake kwa ajili ya ku-counter inaweza tu kufanikiwa kama kazi ya vyombo hivyo haitakuwa kukanusha tuhuma, na kuleta propaganda na uongo kama tuliouona hivi karibuni wa kuhusisha baadhi ya vyama na kuipindua CCM, bali itakuwa ni kuzifanyia kazi tuhuma hizo kwa kuwashughulikia kisheria watuhumiwa, hapa nina maana justice si theatical courts kuonesha kuwa unawashughulikia while behind the scene unamwamuru hakimu apindishe maamuzi.

CCM inatakiwa kuwaacha wabunge na wanachama wake kuwa free to their thoughts and speak it openly withouth controlling them, they need to unleashe its members, kwani Trasparency is key to good governance utamaduni wa kila kitu ndani ya vikao na kuwaacha wananchi ambao kikatiba ndiyo wenye mamlaka ku-guess ni moja ya mambo ambayo yataendelea kuigharimu CCM.

JF is free from any party ndiyo maana ukijiandisha unakuwa huru kutoa mawazo yako hata kama wewe ni CCM, CDM au Independent na hakuna atakaye ifuta mada yako kama umetumia lugha ya kiungwana kuiwakilisha. Nafikiri maamuzi haya wanayoyafanya sasa ni makosa makubwa sana kwa CCM kama basis yake ni habari hapo juu. Usitumie wakereketwa wa Chama tumia watalaam ambao watakuwa tayari kukuambia ukweli hata kama sababu ya kuporomoka kwa umaarufu ni JK mwenyewe, otherwise itakuwa ni utamaduni uleule wa kulindana kuwa rais haguswi. Kwa mtazamo wangu chanzo cha kuporomoka maadili CCM ni JK mwenyewe, jinsi alivyopata nafasi ya urais na jinsi alivyokuwa akiongea hadharani kuwa alitumia miaka 10 kujiimarisha kupata uteuzi wa CCM kwa kuunda wanamtandao. Ilitakiwa JK nae awe nje kabisa ya ulingo na CCM kuongozwa na mtu mwingine kabisa kwa sasa ili kuleta usawa.
 
Asante Lilombe!
Lakini hii tayari imeshatolewa na Maxence Melo na inaendelea kujadiliwa huku jukwaani!...
 
Mimi nimejiunga JF kutokana na uwazi na uhuru wa kutoa maoni yangu pamoja na kupata habari zilizo huru, najua kuna wengine waliojiunga kutokana na matamanio ya aina hii. Lakini kitu kizuri cha kuwashukuru CCM ni kuwa wanaiongezea JF umaarufu.

Wakiwanyima matangazo tutalipia kuiendesha!
 
Niliwai kuona kada wa CCM aitwaye Sabodo akichangia CDM fedha, CCM wameshindwa nini kulijadili hili lilifanyika adharani!?

Arafat, bora umewakumbusha, maana naona macho yao kwa sasa yanaona chadema, watavua magamba na mpaka ngozi wabaki skeleton lakini wamechelewa sana, hawa inabidi wakajipange wakiwa pembeni huku wakifundishwa jinsi ya kuendesha dola na chadema.

MIMI SIJAWAHI KUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE
 
Nahiki cha tabora pia wanakiita chao yani tunachelewa sana kuchukua hatua dhidi ya hawa ccm wanataka kujiuzia viwanja vya uma
 
Mimi nimejiunga JF kutokana na uwazi na uhuru wa kutoa maoni yangu pamoja na kupata habari zilizo huru, najua kuna wengine waliojiunga kutokana na matamanio ya aina hii. Lakini kitu kizuri cha kuwashukuru CCM ni kuwa wanaiongezea JF umaarufu.

Wakiwanyima matangazo tutalipia kuiendesha!
Kwani kuna tangazo lao humu?
 
Si sahihi kusema kuwa JF ni mahasimu wa CCM, inawezekana kabisa kukawa na mahasimu wa CCM, lakini watu hao wanaitumia platform hii, kwasababu ni jukwaa huru la kutoa mawazo na kushirikishana, Je jamii forum ifanye nini kama wapenzi wa CCM wanakimbia au wnajificha itikadi zao badala ya kujitokeza na kutetea au kuchangia?

Nakata kuwa hili si jukwaa la CDM kwa kuwa mimi pia ni mwana-CCM ninachokiona hapa ni kukosa uvumilivu na mbinu za kumudu mashambulizi. Pia ieleweke kuwa kati ya mashambulizi yaliyikuwa yakitolewa kupitia mtandao huu wa kijamii, yamedhihirika kuwa ni kweli pale ambapo rais alipolaimika kuvunja baraza la mawaziri baada ya waziri mkuu kujiuzuru kwa kukumbwa na kashfa ya Richmon, mengine mengi yaliyotokea baadae ukimalizia na hili ambalo bado lipo hot in town la Kamati kuu na Skretariate nzima kuvunjwa/kujiuzuru, hayo ndiyo mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa hapa Jamii Forums, na yamethibitika kuwa ni kweli kwa sababu hatua zimechukuliwa kama mrejesho/mwitikio.

Tuache tabia ya kuandama watu pasipo sababu, bali tuwahimize wana-CCM wajitokeze hadharani na kujenga hoja na kutetea chama badala ya kujificha, na ili wana-CCM tushiriki kikamilifu katika hilo, inawapasa viongozi wetu waliopo madarakani ndani chama au serikali wafanye yale ambayo wananchi na wanachama wanayatarajia kutoka kwao na si tofauti na hapo, kwani hata sisi si mapunguani wa kusimama na kutetea ujinga.

Kuhusu hoja ya kuwa JF inaeneza chuki dhidi ya Chama na kupelekea CCM kuchukiwa, hilo ningependa kuliweka katika maelezo yafuatayo:-

CHUKI NA UPENDO NI MATOKEO YA MAHUSIANO.

Tujiulize ni nini wajibu wetu tunaopaswa kuutimiza na kuutekeleza na
kwa jamii tuitumikiay na kwa njia zipi na wakati gani...

Tusiishie hapo tuendelee mbele zaidi na kufikiria, je tumefanikiwa? kwa kiwango gani? na kwa njia zipi?

Halafu tunapokuja kwenye ku-evaluate, tujiulize tena baada ya hizo indicators/policy, process na conclution je tunastahili kipi kati ya Chuki na Upendo.
 
Mimi nimejiunga JF kutokana na uwazi na uhuru wa kutoa maoni yangu pamoja na kupata habari zilizo huru, najua kuna wengine waliojiunga kutokana na matamanio ya aina hii. Lakini kitu kizuri cha kuwashukuru CCM ni kuwa wanaiongezea JF umaarufu.

Wakiwanyima matangazo tutalipia kuiendesha!

natamani habari hiyo ingekuwa title ya kila gazeti ili JF ijulikane kila mahali
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom