Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
duuuh hii ni hatari kwa taifa, am telling u kama hata chombo kikuu kabisa cha maamuzi ndani ya chama kinaendeshwa kipuuzi namna hii basi nchi hii sio yetu tena!! we are in trouble i mean this is absurd.. ina maana hicho chama mpaka leo hawajajua nini shida? lol acha nicheke mimi, hivi huyo consultant amefika hata darasa la kwanza? eti JF.. JF my foot! wanataka wajigawie tunu ya taifa kipuuzi sisi tuwaangaklie tu?

Sijutii kutumbukiza chooni kadi ya ccm!
 
Wanaogopa Vivuli vyao! Na bado...

Karagwe Kaisho hawawezi kushawishiwa na JF kuichukia CCM - La hasha! Wanahitaji kupatiwa huduma muhimu za jamii, Pembejeo bora za kilimo, Mbolea, na soko la uhakika la mazao yao - basi! Siyo propaganda za vyama vya siasa!

All in All - JF haiwezi kuwa genge la kushadidia uovu - Unless otherwise!
Mama yangu ana umri wa miaka 91 sasa lakini tangu uingie mfumo wa vyama vingi hajawahi kuipigia ccm. Anasema hivi - niliolewa hapa nikachota maji mtoni, nikazaa watoto nao wakachota maji mtoni, leo wajukuu na vijukuu wanachota maji kwenye mto ambao sasa uko mbali zaidi maana ule wa zamani umekauka; sasa hawa ccm niwachague kwa uzuri upi?
Huyu haijui facebook wala JF wala internet nk.
 
Lukansola,

Kweli kabisa hapo... midahalo yote walikimbia, wakathubutu hata kusema kesi za ubadhilifu zilizopo mahakamani ni kesi ndogondogo tu, leo hii wanataka kuleta youtube na forums zao?! Anyway, uwanja uko wazi na fweza wanayo (kulipa consultants for the obvious proves it)...
 
Hili ndilo tatizo kubwa la ma consultants wengi wa nchi yetu. Wanashindwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia taamula yao eti kwa kuwafurahisha watawala.

CCM imeshindwa kutatua kero za watanzania ikiwemo ufisadi uliokithiri ndani ya nchi kupitia mikataba ya kinyonyaji halafu wanasingizia Jamii Forums kumilikiwa na CHADEMA. Huku ni kukosa hoja za msingi kabisa.
Si kuna mahali imesemwa kuwa consultant wao ni Kinana? Kama ndiye huyo kweli basi ndiyo sababu naona somali ideology katika ushauri huo!
 
Mlio wengi humu ni chadema..... Sisi tuko wachache hiyo ni fact na siyo dhambi kwenu ila ni dosari kwetu
 
Mkuu,

Nilicheka tu baada ya kuiona hii habari lakini nikaja kuwaza sana; hivi CCM wanadanganywa kiasi hiki? Hawa 'consultants' wanatumia vigezo gani kuwasilisha maoni yao kwa viongozi wetu wa kitaifa?

CHADEMA wanapewa credit nyingi ambazo hata mtu huwezi kuamini kama wanapewa; ni wazi CCM wanaiogopa CHADEMA sasa kwa kuamini ina hela nyingi sana mpaka inaweza kufadhili vitu vingi tu.

Twitter, FaceBook etc nazo naona zinawatisha CCM kwa ushauri huu wa 'consultant'; huu ni upotoshaji wa wazi. Nilikuwa napuuzia lakini nahisi kuna tatizo ambalo linatakiwa kuwa addressed kwa viongozi wa kiserikali na hata vyama, hivi wao ni vilaza kuambiwa uwongo wa mchana na kuuamini?

Nina wasiwasi 'consultants' hawa wanafanya kazi kwa hisia tu

CCM naona wamejisahau kwamba wamekamata dola ili kuongoza watanzania....wamejipa kazi mpya na isiyo na makubaliano na watanzania ya kuipigia debe Chadema....ninachojiuliza ni kwa bahati mbaya au kuna namna??
 
Na wewe ni CHADEMA mkuu, si mnamilikiwa na CHADEMA?

Sasa wewe kama ndo mshauri wa CCM; unakiri kuwa nawe kwa kujisajili JF ushamilikiwa na CHADEMA?

Tatizo lenu mnaounga mkono hoja za 'upande flani' huwa mnapokutana na negativity yoyote mna-deal nayo kwa jazba.

Ninachoamini bado CCM wanaweza kuitumia platform hii vema; hoja ikijibiwa kwa hoja tutasimama vema tu. Wapo wana CCM wengi hapa, wanajibu hoja kwa hoja na wanaeleweka sana. Sasa imagine Twitter na facebook nazo wanaambiwa zimechangia CCM kuporomoka umaarufu. Mtapambana na Social Networks hadi lini mkuu?

Wapo waislam wengi humu JF, wana busara kubwa hata kueleza nashindwa, watatu kati ya Directors 6 wa Jamii Media ni waislam (FYI).

Ushabiki upi tena mkuu?

Ukweli ni kuwa wengi wa wanazi wa CDM au CCM humu naamini hawana hata kadi za vyama hivyo, well, za CCM inawezekana wengi wanazo lakini siamini kuwa ni wote wanaoitetea.

Taifa letu linahitaji zaidi ya unafiki na siasa zisizo na tija; tuna matatizo lukuki, wasomi kama wewe Barubaru mnaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuliko kushiriki siasa ambazo ni wazi mnakuwa mnajua hazijengi bali kubomoa.

Ni hayo tu kwa sasa

Ukiwa kama nahodha wa chombo unatakiwa ujue ukubwa wa chombo chako na kujua mwelekeo wa kule unakotaka kukifikisha chombo hicho. lakini vile vile unatakiwa ujue vizuri sana mwelekeona hali halisi ya njia unayopita na tabia zake za hali ya hewa.

Sasa kama kiongozi wa forum hususan hii ya waTanzania unatakiwa ujue nafasi yako katika jamii hiyo. Kiandishi tunasema kuwa kazi yako kubwa ni kuelimisha jamii, kuipasha habari jamii na kuiburudisha jamii. Kama kiongozi wa jamii huruhusiwi kabisa kushabikia au kuitolea maamuzi binafsi habari na kuipeleka kwa jamii. Kwani tunaamini kuwa kalamu ya mwandishi ni hatari kuliko bomu la nyuklia.

Nikipembua haraka haraka sana katika forum zako na maandishi mengi sana. ume base sana upande wa Chadema na kuwa forum yako kama tawi la Chadema na yeyote alie kinyume na matakwa ya Chadema basi ni adui yako pia.

Ni vizuri kusimamia haki za kuruhusu kila pande kutoa hoja zake na kuiachia jamii isome na kuamua. Wewe kazi yako kuu ni kuondoa lugha chafu na hatarishi kwa jamii.

Vile vile unatakiwa ujue wazi kuwa jamii ya tanzania hususan tanganyika sasa ina matatizo makubwa sana ambayo sio siri tena ni ushabiki wa udini. Dini moja kujiona superior than others na hilo lipo wazi kuanzia kwenye Serikali zenu mpaka vyama vya siasa. Sasa kama mwandishi na msimamizi wa forum unatakiwa kuliweka bayana hilo na kulikemea kwani so long as limejitokeza kwa wingi basi huwezi kulifumbia macho.

lakini la mwisho nazidi kukusisitizia kufata sheria na ethics za kiuandishi kwani hizo siku zote zitaifanya forum yako iwe makini na kuondoa malalamiko kwa jamii ikiwa pamoja na kupata wachangiaji makini kama walivyokuwa katika Youngafrican.
 
Mlio wengi humu ni chadema..... Sisi tuko wachache hiyo ni fact na siyo dhambi kwenu ila ni dosari kwetu
Sidhani kama nakosea kusema kuwa wengi tulio humu si wanachama wa CDM, si wanachama wa chama chochote kile. Wengi wetu tuliomo humu tunaangalia sera vs utendaji wa chama, hivyo ndio vinatuvutia, au kutukimbiza.
 
Ukiwa kama nahodha wa chombo unatakiwa ujue ukubwa wa chombo chako na kujua mwelekeo wa kule unakotaka kukifikisha chombo hicho. lakini vile vile unatakiwa ujue vizuri sana mwelekeona hali halisi ya njia unayopita na tabia zake za hali ya hewa.

Sasa kama kiongozi wa forum hususan hii ya waTanzania unatakiwa ujue nafasi yako katika jamii hiyo. Kiandishi tunasema kuwa kazi yako kubwa ni kuelimisha jamii, kuipasha habari jamii na kuiburudisha jamii. Kama kiongozi wa jamii huruhusiwi kabisa kushabikia au kuitolea maamuzi binafsi habari na kuipeleka kwa jamii. Kwani tunaamini kuwa kalamu ya mwandishi ni hatari kuliko bomu la nyuklia.

Nikipembua haraka haraka sana katika forum zako na maandishi mengi sana. ume base sana upande wa Chadema na kuwa forum yako kama tawi la Chadema na yeyote alie kinyume na matakwa ya Chadema basi ni adui yako pia.

Ni vizuri kusimamia haki za kuruhusu kila pande kutoa hoja zake na kuiachia jamii isome na kuamua. Wewe kazi yako kuu ni kuondoa lugha chafu na hatarishi kwa jamii.

Vile vile unatakiwa ujue wazi kuwa jamii ya tanzania hususan tanganyika sasa ina matatizo makubwa sana ambayo sio siri tena ni ushabiki wa udini. Dini moja kujiona superior than others na hilo lipo wazi kuanzia kwenye Serikali zenu mpaka vyama vya siasa. Sasa kama mwandishi na msimamizi wa forum unatakiwa kuliweka bayana hilo na kulikemea kwani so long as limejitokeza kwa wingi basi huwezi kulifumbia macho.

lakini la mwisho nazidi kukusisitizia kufata sheria na ethics za kiuandishi kwani hizo siku zote zitaifanya forum yako iwe makini na kuondoa malalamiko kwa jamii ikiwa pamoja na kupata wachangiaji makini kama walivyokuwa katika Youngafrican.

On that note alone, "nahodha" wa CCM tayari amedidimiza chombo chake!

Ukiichukulia forum ya wachangiaji wengi kama JF kwa mfano wa gazeti au radio, maoni yako yana mantiki kubwa sana! Tatizo kwenye forum, huyo Maxence anabezwa na kuwa challenged kama wengine. The communication is bidirectional, tofauti na radio au gazeti! Atakacho kisema Maxence kwa maandishi, wapo watakao kipinga na wale watakao kiunga mkono. Kama wote wanakiunga mkono, basi hilo si tatizo lake; ni mwono wa wanaforum kulingana na ujuvi wao, taarifa na hekima binafsi.
 
Mkuu,

Nilicheka tu baada ya kuiona hii habari lakini nikaja kuwaza sana; hivi CCM wanadanganywa kiasi hiki? Hawa 'consultants' wanatumia vigezo gani kuwasilisha maoni yao kwa viongozi wetu wa kitaifa?

CHADEMA wanapewa credit nyingi ambazo hata mtu huwezi kuamini kama wanapewa; ni wazi CCM wanaiogopa CHADEMA sasa kwa kuamini ina hela nyingi sana mpaka inaweza kufadhili vitu vingi tu.

Twitter, FaceBook etc nazo naona zinawatisha CCM kwa ushauri huu wa 'consultant'; huu ni upotoshaji wa wazi. Nilikuwa napuuzia lakini nahisi kuna tatizo ambalo linatakiwa kuwa addressed kwa viongozi wa kiserikali na hata vyama, hivi wao ni vilaza kuambiwa uwongo wa mchana na kuuamini?

Nina wasiwasi 'consultants' hawa wanafanya kazi kwa hisia tu

Mkuu Salam nyingi sana,

Mi naona tatizo kubwa CCM bado haina watu makini wenyewe uwezo wa kuongea ukweli mbele ya M/kiti wao ambaye ndiye rais pia. Hii imekuwa ni tabia ya CCM tokea zamani, kumdanganya Mkuu wao, ndio maana utakuta rais anaweza kutembelea shule ambayo haina viti badala ya viongozi wa CCM kumwonyesha Rais hali halisi ya shule ili apate picha kamili wao wapo tayari kuchukua viti shule za jirani na kujaza madarasani ili kumdangaya Rais kuwa shule ina viti vya kutosha.

Siku zote CCM inatafuta majibu marahisi kujibu maswali ambayo yanahitaji watu walibobea katika fikra, hasa Policy na strategy za kutatua matatizo, kulingana na eneo la tatizo. Mfano; katika Uchaguzi wa 2005 jimbo la Tarime niliwai kufika pale baada ya Uchaguzi na kuongea na Vijana wa jimbo la Tarime, kimsingi wananchni wa Tarime waliichukia CCM katika uchaguzi hule kutokana na matusi ya aliyekuwa Mbunge wa CCM wa awali (Mhe. Chambiri) alipo waambia wananchni kuwa Ukoo wetu uta watawala hadi wajukuu! baadaye katika kampeni alienda Mhe. Makamba ambaye alikuwa akijibu maswali ya wananchni kwa matusi tena hadi ya nguoni, lakini ukiangalia maelezo ya CCM baada ya kushindwa uchaguzi ule utakuta ukweli haumo hata kidogo.

Kama CCM haitaacha tabia yake ya asili ya kudanganya viongozi wake haitaacha kuchukiwa na wana nchni kwasababu hawatakuwa wanajua njia halisi ya kutatua matatizo asilia na watakuwa wanaongeza matatizo mapya badala ya kutatua tatizo asilia.

Hapa wametafuta jibu rahisi linalotokana na tabia ya CCM ya kuamini kuwa kila kitu kinafanyika kwa fedha hasa ya rushwa, ndio maana hawataki kusumbua akili kutafuta majibu ya maswali na matatizo asilia, wao wanaamini bila Rushwa hakifanyi chochote, hivyo hawajui kuwa kuna kitu kinaweza kufanyika kwa nguvu ya Umma na matakwa ya Raia, wao wanjua ni fedha ndio peke yake inaweza kufanya jambo.

Kama CCM hawawezi kuongelea mambo ya Richmond, Dowans, IPTL, Uhaba wa ajira, Kuteua viongozi wasio makini katika kada za utawala na Uongozi, kutumia Rushwa katika kuteuwa wagombea wao wa Ubunge. nk kama sehemu ya kujirekebisha badala yake wanaongelea kuwa kuna fedha zinatumwa kuwaondoa madarakani basi wanamdanganya M/kiti wako na huyo M/kiti wao anayedanganywa pia hana uwezo wa kuchanganya na zake kama alivyowaambia wafanyakazi mwaka jana.
 
Always the blame lies with somebody else.

CCM wanatakiwa kuweka mikakati thabiti ya kuweza kushinda 2015. Kitu kimoja ambacho waelewe ni kuwa, siku zinavyozidi kwenda, wao ndio wanazidi kupoteza wapiga kura. Sababu moja ni kwamba, vijana walio na miaka 13 mpaka 17, ambao walikuwa hawajafikia umri wa kupiga kura kwenye uchaguzi uliopita, watakuwa wamefikia huo umri. Na hawa vijana wengi wako kwenye households ambazo zimeichoka CCM. Kila kukicha wanawasikia wazazi wao wakilalamika kuhusu maisha magumu, ufisadi, mabomu, umeme..nk, vyote vilivyosababishwa na CCM.

Kwa hiyo ni dhahiri, wakati wao wa kupiga kura ukifika, hawataipigia CCM, na hawa vijana kwenye hii age bracket ni wengi. Wao wanataka kubaki kuilaumu JF. Lakini hata kwa mfano ni ya Chadema, so what? Ni sawa na kulalamika kuwa Barcelona wana Messi! Sasa asicheze, au wamevunja sheria?
 
Kama wanadhani ni rahisi waanzishe CCM forum tuone kama itakuwa kama wanavyodhani. Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo. Kama alivyosea member mmoja hapo juu, si wana pesa bana, wanaweza zitumia kuwalipa member ili wachangie.

I see JF is more than siasa za CCM na ChADEMA.
 
Mazee ya ccm bwana, yani ma fedha yote waliyonayo ndo wanazidiwa na jamiiforum, teh teh teh teh ,Tatizo nawaambieni ni mazeee akili chovu za kikomnisti.

Kwanza kwenye katiba mpya wabadilishe hicho kifungu cha kugombea urais uwe na miaka 40, katiba inakiuka haki za binadamu.Vijana wanataka kugombea Urais, waweke miaka kama ya wabunge.
 
Hii ni nzuri sana, na waanzishe basi mtandao wao.

Hivi ni mara ngapi wameambiwa kuwa JF ni mtandao huru unaowakutanisha wana na mabinti wa Tanzania waliotapakaa kila kona ya Dunia? JF inafanana na mkusanyiko wa Askari waliopigana vita ya dunia na sasa wanarudi nyumbani,wameona kuna njia ya kuuondoa ukoloni, ukandamizaji, dhuluma za kikoloni kwa kuanzisha harakati za kuikomboa Ardhi yao.

JF haina ubia wa kisiasa lakini wanachama wake ni wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa. CCM kama wanataka kuanza siasa za mitandao na waanze ila nawashauri CHADEMA wasianzishe siasa za aina hiyo, it's too low for them
 
Tunaendesha mambo yetu kwa hisia na woga. Na tatizo la hisia na woga huzaa taifa la watu waongo. Na hapa ndipo tulipofika.

Wamehisi kwa kuwa watu wengi wanaotoa maoni yao hapa wamekuwa wakikosaoa utendaji wa serikali ya CCM, basi hawa watu lazima ni wapinzani. Kisha wakaendelea kuhisi: kwa kuwa CHADEMA ndio wapinzani wetu wakuu, basi watu hawa wanaoikosoa serikali yetu ni CHADEMA, kisha wakafikia hitimisho kuu: Huu mtandao unamilikiwa na CHADEMA. Halafu watu hawa ndio wanaitwa 'consultants' wa kukishauri chama kipone!

Katika ulimwengu wa kufikiri, ukishakosea premise ya fikra zako na ukakosea mchakato wa kufikiri lazima utaishia kuwa na fikra potofu na utaibuka na utatuzi potofu na hivyo utatoa majibu marahisi kwa maswali magumu.

Ushauri wangu kwa JF ni kwamba don't bother arguing with these people-just keep on doing what you think is the right thing to do.
 
Kama kweli wamefanya na kutoa ripoti ya kweli bila woga Bravooo kwao, onyo kwao ni wasijaribu kunyamazisha watu midomo waingie tu katika ushindani halafu raia tutaamua nani mkweli na wa kumfuata, mbona wameshaanzisha magazeti yao uchwara na hayana mashiko sokoni kwa kuwa yamejaa propaganda tuu bila ukweli wowote
 
sasa ccm wamevua gamba gani kama kunawatu bado wanadanganya,
Wawe wakweli ndo watapata suluhisho sahihi, NDO MAANA SILIPII KADI YA CCM SABABU YA UPUMBAVU KAMA HUU!

Sasa hivi hata mitaani kunamilikiwa na CHADEMA kama dhana yao ndiyo hiyo,they need to be aware that Tanzanians are yearning for change not a continuation of the corrupt status quo
 
sasa ccm wamevua gamba gani kama kunawatu bado wanadanganya,
Wawe wakweli ndo watapata suluhisho sahihi, NDO MAANA SILIPII KADI YA CCM SABABU YA UPUMBAVU KAMA HUU!

mkuu henge ... jivue gamba ... LIPIA KADI YA CHADEMA
 
Tunaendesha mambo yetu kwa hisia na woga. Na tatizo la hisia na woga huzaa taifa la watu waongo. Na hapa ndipo tulipofika.

Wamehisi kwa kuwa watu wengi wanaotoa maoni yao hapa wamekuwa

wakikosaoa utendaji wa serikali ya CCM, basi hawa watu lazima ni wapinzani. Kisha wakaendelea kuhisi: kwa kuwa CHADEMA ndio wapinzani wetu wakuu, basi watu hawa wanaoikosoa serikali yetu ni CHADEMA, kisha wakafikia hitimisho kuu: Huu mtandao unamilikiwa na CHADEMA. Halafu watu hawa ndio wanaitwa 'consultants' wa kukishauri chama kipone!

Katika ulimwengu wa kufikiri, ukishakosea premise ya fikra zako na ukakosea mchakato wa kufikiri lazima utaishia kuwa na fikra potofu na utaibuka na utatuzi potofu na hivyo utatoa majibu marahisi kwa maswali magumu.

Ushauri wangu kwa JF ni kwamba don't bother arguing with these people-just keep on doing what you think is the right thing to do.

Consultant wapi hao wazee, wamepewa fedha za kufanya tafiti wamezila na ripoti wakaandika kutoka vitandani mwao. Harafu utafiti wa nini wakati kila kitu kipo wazi yani ya kwamba Rais ameshindwa kukidhi , sio kupwaya tu, bali amekuwa kama mchezaji wa rugby kucheza football kama namba tano wa kutumainiwa.
 
At the end of the day, ccm has to realise it's just a political party. It's bound to be challenged and its performance is measured by the public! So if they cant perform, while the country stumbles from one crisis to another, it is logical to lose support. This is the basics of multi-party democracy.

Exactly! and this is what has entrenched in many of our political parties...they tend to believe, albeit wrongly, that their line of thoughts are always suprime and beyond questioning by the lay.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom