Mshana ukipona na hili la takwimu za udini we kiboko

KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,827
1,271
katika kile kinacholalamikiwa na Waislam kuhusiana na Sensa bila kumungunya maneno TBC1 hamuwezi kukwepa hili hata Rais katika hotuba yake ameonekana kukerwa na kitendo cha taasisi ya umma kuendekeza udini.Pamoja na kuomba radhi lakini impact ya hicho kilichofanyika ni kubwa sana japo watu wanajaribu kufunika.
Mytake:
1. Ingekuwa wenyekujua nini maana ya dhamana Mshana ungekuwa umeshajiuzulu siyo kusubiri kuwajibishwa.
2. Ingekuwa ni vituo vya binafsi ndivyo vingekuwa vimerusha hicho kipindi kingekuwa kimeshafungiwa kama Mwanahalisi.
3. Waziri husika na Mwenyekiti wa bodi mzee Nyachia hili ujaliona?umechukua hatua gani?
 
hao lao moja, walikuwa wanapima maji kwa mguu matokeo yao wameyaona, TBC inamuhujumu Rais kikwete.
 
Hii inaonesha ni jinsi gani kituo cha television cha serikali (ukweli na uhakika) kinavyochakachua habari
 
Na office ya waziri mkuu, roman cathoric, na idara ya utalii pamoja na cia wajiengue kwatakwimu zisizosahihi
 
Si TBC walisema wametoa WIKIPEDIA. Mnawalaumu nini wakati masheikh wanaongoza kwa kuingia na Laptop misikitini na kuwadanganya imetengenezwa na Muislam

Mkuu kama una usingizi ni bora ukalale
 
Mshana safi sna ulichofanya imedhihirisha kuwa wewe hukustahili hiyo nafasi. JK kakunanga sna kwny hotuba yke.
 
Mshana safi sna ulichofanya imedhihirisha kuwa wewe hukustahili hiyo nafasi. JK kakunanga sna kwny hotuba yke.
Hongera Mshana! umetuamsha kama si wewe (sababu) leo hii Waislamu tungekuwa tunahesabiwa huku mfumo kristo ukizidi kueneza propaganda kuwa sisi ni wachache.....big up Mshana!
Ukifukuzwa kazi wakomalie Ofisi ya Waziri Mkuu, wizara au bodi ya utalii nao wawajibike usikubali kwenda peke yako, waliyaanza wenyewe wewe uliyakuta tu!
 
wote wadini tu, kuanzia jk, mshana, mleta mada na wachangiaji

Afadhali hao wa TBC maana wametoa source ya takwimu zao ambazo zinapatikana kwenye mitandao.
JK na CCM wao wanachowaza ni kutawala milele hata kwa gharama ya amani yetu.
CCM wametufikisha Watanzania mahala ambapo sasa tunatazamana Kiislamu na Kikristo.
 
Wanabodi.

Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakiristo, na wasiokuwa na dini tunamshukuru Mungu kwa kutupa moyo wa subira kuishi kwa upendo na kuvumiliana na kuheshimiana watu wa dini zote na wasiokuwa na dini kuna kitu kinaitwa (Coexistence) ambacho watanzania tunacho tumepewa na Mungu.

Hizi takwimu ambazo zipo kwenye idara za serikali na katika taasisi za dini zimetolewa kwa faida ya nani kisiasa, kidini, kibiashara, kimaendeleo, hau faida zake zipi takwimu zenyewe ni hizi hapa...

Ofisi ya Waziri Mkuu inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 35%. TBC1 wametangaza Wakiristo ni 52% - Waislam ni 32%. Bodi ya Utalii inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 40%. Tovuti ya Wakatoliki (www.rc.net) inaonyesha Tanzania kuna Wakiristo ni 44% - Waislam ni 34%.

Takwimu hizi zimekuwa zikitumiwa katika uteuzi na maamuzi na serikali.
 
Inabidi hao wenye hizo takwimu watuambie walipata wapi na wametumia methods gani kupata hizo.

Hamna haja serikali kutumia mabilioni kuhesabu mtu mmoja mmoja kama watu wapo wanaoweza kukaa ofisini na kutupa hizi Statistics kiulaini namna hiyo.
 
Wanabodi.

Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakiristo, na wasiokuwa na dini tunamshukuru Mungu kwa kutupa moyo wa subira kuishi kwa upendo na kuvumiliana na kuheshimiana watu wa dini zote na wasiokuwa na dini kuna kitu kinaitwa (Coexistence) ambacho watanzania tunacho tumepewa na Mungu.

Hizi takwimu ambazo zipo kwenye idara za serikali na katika taasisi za dini zimetolewa kwa faida ya nani kisiasa, kidini, kibiashara, kimaendeleo, hau faida zake zipi takwimu zenyewe ni hizi hapa...

Ofisi ya Waziri Mkuu inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 35%. TBC1 wametangaza Wakiristo ni 52% - Waislam ni 32%. Bodi ya Utalii inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 40%. Tovuti ya Wakatoliki (RCNet) inaonyesha Tanzania kuna Wakiristo ni 44% - Waislam ni 34%.

Takwimu hizi zimekuwa zikitumiwa katika uteuzi na maamuzi na serikali.

Serikali ya chama gani vile?....
 
Acha mambo ya udini mbona watu wamehesabiwa kinyume na matarajio ya wachache alafu mbona kwa sasa nafasi nyeti za nchi haziendani na takwimu ulizozitoa.
 
Wanabodi.

Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakiristo, na wasiokuwa na dini tunamshukuru Mungu kwa kutupa moyo wa subira kuishi kwa upendo na kuvumiliana na kuheshimiana watu wa dini zote na wasiokuwa na dini kuna kitu kinaitwa (Coexistence) ambacho watanzania tunacho tumepewa na Mungu.

Hizi takwimu ambazo zipo kwenye idara za serikali na katika taasisi za dini zimetolewa kwa faida ya nani kisiasa, kidini, kibiashara, kimaendeleo, hau faida zake zipi takwimu zenyewe ni hizi hapa...

Ofisi ya Waziri Mkuu inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 35%. TBC1 wametangaza Wakiristo ni 52% - Waislam ni 32%. Bodi ya Utalii inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 40%. Tovuti ya Wakatoliki (RCNet) inaonyesha Tanzania kuna Wakiristo ni 44% - Waislam ni 34%.

Takwimu hizi zimekuwa zikitumiwa katika uteuzi na maamuzi na serikali.

Hapo utaona umuhimu wa swali la dini katika sensa.

Tunajifanya hatujali dini wakati sehemu zote hizo, pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu, wametaja asilimia za Waislam/Wakristo.

Ujinga mmoja tunaofanya ni kumuona Nyerere kama mtume, na hotuba yake aliyosema kwamba hakujua namba ya mawaziri wake kwa dini imechukuliwa kama kukataa kuhesabu watu kwa dini.

Wakati huo huo dunia inabadilika. Nakubali kwamba kuna uwezekano wa namba hizi kuleta matatizo (rationale ya watu wanaosema wana nia nzuri kukataa swali la dini kwenye sensa ni kwamba wengine -let's face it, waislamu- watatumia figures za dini kuleta chokochoko). Kwa hiyo wanasema tusiweke swali la dini ili kusiwe na official government figures za idadi ya watu kwa dini.Ili kusiwe na chanzo cha chokochoko kama za Waislamu kuanza kutaka nafasi za juu/ elimu kwa quotas za dini.

This argument is wrong. Because it is based on a deception.Because it fears the truth.

Ni kama vile serikali inataka kutumia manipulation kuzuia watu kujua ukweli. Hesabuni watu, wekeni swali la dini tujue Tanzania ina Wakristo wngapi na waislamu wangapi.Ondoeni mgogoro usio lazima. Halafu mtu akileta ujinga wa kutaka nafasi za uongozi kwa misingi ya dini tutakataa.

Serikali ikikataa kuhesabu watu na kuweka kipengele cha dini, inapalia moto hizi tetesi kwamba inakandamiza waislamu. Inafanya mgogoro uwe mkubwa kuliko ulivyotakiwa kuwa.

Kama mtu anapanga kuleta chokochoko kwa kutumia namba za sensa, usipompa hizo namba ndo umempa carte blanche ya kufanya chokochoko hizo, na hata kumuongezea sympathizers.

Mimi huona vibaya sana ninapoangalia ramani za statistics na kukuta Tanzania katika vitu vingi sana iko under "Data Not Available". Sensa ni zoezi lenye gharama kubwa sana na linatokea mara moja tu kila mlongo. Kwa nini tusiweke hili swali la dini hata academicians wanaotaka kujua hizi habari katika reseraches zao (kwa mfano, kama mtu anataka kujua relationship between religious belief and family planning/ reproduction rate ili ku shape government policy, atashindwa kupata reliable government figure.

Ile argument ya Nyerere ambayo imekubalika sheepishly, kwamba serikali hailazimiki kuhesabu watu kwa dini kwa sababu haijengi misikiti iko outdated, na pengine iliweza kukubalika nyakati zile tu kwa sababu Nyerere alikuwa strongman na watu walikuwa bado hawajaweza kum challenge vizuri. Na hata yeye inawezekana kabisa alikataa kuhesabu watu kwa sababu za political expediency zilizo les benevolent kuliko alivyotaka ionekane.Kwa sababu habari ya kujua idadi ya watu kwa dini -unless you are simpleton, and Nyerere was no simpleton- itakusaidia kwa mambo mengi zaidi ya kujenga misikiti, this is a simplistic approach.Nimetoa mfano hapo wa research ya kuangalia relationship between religious belief and reproduction rates, hii inaingia moja kwa moja katika government policy.

Sasa tunaweza kushindwa kuwa na the right government policy kuhusu reproductive health simply kwa sababu tume ignore umuhimu wa kuwa na government statistics (from a reliable source such as the census as opposed to from a religious body which is not above being prone to inflating figures).

Kuna siku watu watakaa na kucheka sana hii nchi ilivyokuwa inaendeshwa. In so many ways bado tupo katika Ujamaa unaoenda kwenye Ukomunisti. Ule unaokataa kuwepo kwa dini, kwa sababu unataka kumfanya kila mtu aamini kwamba serikali ndio dini pekee.

Bora ukweli mbaya (kujua idadi ya watu kwa dini, hata kama kuna uwezekano wa habari hii kuleta matatizo) kuliko uongo mzuri (kwamba Tanzania serikali haijali kabisa mambo ya dini na hivyo haina haja ya kujua idadi ya watu kwa dini).
 
Inabidi hao wenye hizo takwimu watuambie walipata wapi na wametumia methods gani kupata hizo.

Hamna haja serikali kutumia mabilioni kuhesabu mtu mmoja mmoja kama watu wapo wanaoweza kukaa ofisini na kutupa hizi Statistics kiulaini namna hiyo.

Madhehebuya dini za Kikiristo (Wakatoliki, Walutheri, Waangalikana, Wapentekoste, na hata Makanisa mengine ya Kilokole) hutunza kumbukumbu za waumini wao. Mtafiti mahiri akipitia na kuweka pamoja kumbukumbu za idadi ya madhehebu yote ya Kikristo atabaini/kukadiria idadi ya makundi hayo ya kidini. Aidha kwa kutumia kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu na/au idadi ya jumla ya Watazania kwa mujibu waSensa za nyuma ni rahisi kukadiria idadi ya Wakristo, Waislam na Makundi mengine. Makadirio haya yanaweza kuwa na kosa kati ya +1% au -1% (99 confidence level).

........ https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ya-rais-kikwete-yatokanayo-7.html#post4503949
 
Kuna tatizo kubwa kutegemea figures za madhehebu kwa sababu hazina integrity ya level ya figures za sensa.

Kutumia ukuaji wa watu kwa sensa za nyuma ni guesswork zaidi kwa sababu watu wanabadili dini, na unapoongeza makadirio katika makadirio unazidi kupata inaccurate figures.

Njia rahisi kabisa ya ku settle this ni kuweka swali la dini katika sensa.
 
Na hizi takwimu zinasababisha hata wale waarabu wapunguze misaada ya tende na kuilekeza zaidi Zanzibar maana ndio kwenye Waislamu 99% hata Islamic bank inashindwa kuleta pesa kwenye nchi yenye idadi kubwa ya makafiri.

Mpango mpya ni kuhakikisha kila Muislamu anazaa watoto wasiopunguwa 10 ili sensa ijayo Umma wa mtume SAW uwe 80% ya Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom