Mshahara wa TShs 900,000 hautoshi kabisa

[h=6]Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini[/h]

Hapa pabaya ina maana waliofanya kazi kwa miaka 30 nao wakubali kukosa viinua mgongo vyao, huu sasa mtego
 
ila mkuu madaktar si wana maduka ya madawa ambayo wanaiba serekalini na pia wanamiliki hospt zao nadhani wana masilai mengi tu,

Kama madaktari ndio wana maduka na wafamasia wana nini? Laki saba ukimpa Jk anaishi nayo kwa siku ngapi, nyumba ajilipie, maji, umeme na nauli ya kwenda kazini. Akifika kaZini anakutana na mgonjwa akimuomba nauli au msaada wa kununuliwa dawa--pathetic president.
 
What a statement frm my President...nimeisoma taarifa yote hii,na natangaza wazi,,SIWAPENDI MADAKTARI WOTE WANAOENDELEA KUVUNJA SHERIA NA KUTESA WANANCHI

NI WAZI WANATUMIWA,HALINA UBISHI HILI
 
[h=6]Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini[/h]

Wameuchukua huu ushauri wa rais wao, tuwasubirie watuambie maana liwalo na liwe. Kila mtanzania ajitafutie daktari wake sasa na amlipe kwa kadri anavyoweza la sivyo kwa babu Samunge na Maji marefu!
 
Mkuu, Mshahara wa sh 955,000/- ikishakatwa PPF na PAYE inabaki Sh. 720,000/- na sio Laki tano na nusu.
Kimsingi sikubaliani na Mbunge kulipwa 10,000,000/- kwa wiki4 alafu daktari analipwa asilimia 10% ya mshahara wa mbunge.

Net inakuwa 705,150
Nashangazwa na watu wanaodai hela hii inatosha
Serikali ingeboresha shule zake ili tuwe na uhakika ukilipwa hela ndogo at least watoto watapata elimu nzuri
Bahati mbaya hilo halipo
Kuna wapuuzi wanawalaumu madaktari kudai haki zao kwa sababu wao aidha kwa upuuzi au kusubiri huruma, hawajadai
Ujinga wako si wa mwenzako
Kama wamechagua maisha duni ni wao, si wao
Hii nchi ina hela za kutosha
Nyingine zimetunzwa Uswisi na nyingine zipo Kagoda nk
Serikali ina hela ya kubadili mashangingi ila haina ya CT scan
Wanapoishabikia tunashangaa
Ila dunia imejaa wajinga kuliko werevu na ndio maana hujafunguka kudai haki
Wanaofunguka lazima wawe werevu na hawa bado
Mkisikiliza takwimu kijinga hutaelewa
Mwaka 2005 gunia la mahindi liliuzwa 6,000 leo elfu 60
Kumbuka bei ya kila kitu!
Serikali inayotamba kuongeza mshahara wakati imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei na anguko la shilingi yetu ni dhaifu
Laki 4 ya 2005 ni kubwa kuliko laki 9 ya leo halafu mtu anatamba na kuna wajinga wanamsifu na kulaani madaktari
Amkeni
 
Endeleeni kulala usingizi wa pono kwa kuona sifa kuwa unafanya kazi za serikali ktk mazingira hatarishi na unaona ni sawa tu...shame on you!!!!!!!!!!!!!!
Mwisho wa siku tukitaka kuangalia umuhimu wa kila kazi serikalini tutakuta kila kazi ina umuhimu kwa kipindi chake...
Kuhusu mazingira magumu kuna watu ka polisi angaliat mishahara wanayolipwa, nyumba wanazoishi na hata vifaa vya ufanyiaji kazi, unakuta anaenda kupambana na majambazi wa silaha za kivita wao hata bullete proof hawana..Na ndo hawaruhusiwini kugoma hata kidogo unadhani wakigoma nchi itakalika?
Muhimu serikali kama kufanya review ya malipo waangalie na sehemu zote.
 
Madaktari kama mshahara mdogo katafute sehemu ya kulipa vizuri hakuna tatizo serikali hawana uwezo wa kuwalipa kama mnaona Udokta haulipi basi ingieni kwenye siasa.
 
sasa kama wameambiwa ruksa kuacha kazi si waende,kwani itakuwa wamerahisishiwa badala ya kugoma huku wanachukua mshahara(kodi zetu),na wale wanaowatetea wawajengee hospital ili wawaajili.
 
Nchi ya Maneno.Watu Wa maneno. Maneno maneno kila raia maneno.. Mafundi kweli Wa maneno..

Kwani Maneno yanasaidia kuponya wagonjwa?. Watu wanakata roho huku ati, watu wanaotakiwa kufanyiwa operations hawajui hatma zao Na Hali zao zinazidi kudorora.. Hapa watu walioshiba ugali Na Kauzu wanapiga domo tu..

Sikilizeni enyi mbweha.. Hatutaki maneno tena, Kama mnaona madai ya madaktari ni chachu tupilieni mbali wao Na madai Yao kwenye dustbins.. Na muajiri madaktari wengine Na raia tuendelee kupata matibabu ..

Mambo ya maneno ni upuuzi .. Upuuzi mtupu, huyu namlipa sana, sijui yule kidogo, ah ni majungu tu yote hayo.. ilihali wananchi maskini ya mungu tusio Na hatia tunakwisha Kwa kukosa stahiki ya tiba..

Sina Shaka kesho wahandisi nao watalianzisha.. Mhandisi kuanza Na 420,000 Na baada ya makato anakwenda hom Na 320,000 aiseee.. Hata house-girl Wa hapa masaki wanamzidi kipato mhandisi.. Erb mpo au mnachangisha michango ya stickers tu..
 
[h=6]Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana kwa pamoja kwa mambo saba.matatu tumekubaliana nusu kwa nusu na mawili ndio hatujakubaliana.[/h]
my take.sasa ww,kama zaidi ya nusu ya madai yamekubaliwa bado unakataa,nenda zako,MUME hakubembelezi tena.tafuta mwingine
 
Mwisho wa siku tukitaka kuangalia umuhimu wa kila kazi serikalini tutakuta kila kazi ina umuhimu kwa kipindi chake...
Kuhusu mazingira magumu kuna watu ka polisi angaliat mishahara wanayolipwa, nyumba wanazoishi na hata vifaa vya ufanyiaji kazi, unakuta anaenda kupambana na majambazi wa silaha za kivita wao hata bullete proof hawana..Na ndo hawaruhusiwini kugoma hata kidogo unadhani wakigoma nchi itakalika?
Muhimu serikali kama kufanya review ya malipo waangalie na sehemu zote.

Exactly! Polisi wana mishahara midogo na mazingira mabaya ya kazi
Hawagomi lakini wananchi tunakiona cha moto
Mabingwa wa rushwa
Mabingwa wa kubambika kesi
Ukikutana nao usiku heri ungekutana na majambazi ukajua moja
Yote hii sababu sheria kandamizi zinawanyima kugoma na frustrations zao wanamalizia kwetu
Kama taifa tunapaswa kukemea hili
Lazima kuwe na mfumo unaoilazimisha Serikali kuboresha mishahara ya makundii haya yasiyoruhusiwa kugoma na ikishindwa kufanya hivyo iwajibishwe
Badala ya wa-Tanzania na sekta nyingine kuwalaumu madaktari wangeunganisha nguvu kushinikiza wanasiasa kufanya wajibu wao wa ku-share keki ya Taifa na wafanyakazi
Ajabu wanawapiga vita madaktari badala ya chimbuko la matatizo ambalo ni Serikali
 
Wakati Kikwete anachukuwa madaraka mshahara wenu ulikuwa haufiki 180,000/= yeye ndiye aliyewaongeza mpaka kufikia hapo mlipo. Na mwaka huu kawaongeza sio chini ya 15% na amesema bado ataendelea kuwaongeza kila inapowezekana.

Tena huo ni wa kuanzia tu. Ni wapi watu wasio na ujuzi wanaanza kazi kwa mshahara huo Tanzania hii? Bado hamuhesabu, nyumba na marupurupu mengine kibao ambayo wenzenu hawapati.
 
Madaktari lazima watafakari suala hili kwa kina ni kweli kada ya afya ni muhimu sana lakini pia tusidharau kada nyingine kwani tukiwa na mawazo hayo nchi hii haitatawalika badae.

Wanadai wamesoma miaka mingi na masomo magumu. Hii inashangaza, nimejiuliza maswali haya na sijapata majibu, hivi mungu si ametoa vipaji kwa watu wake na mwenye kipaji fulani hata kama jambo ni gumu kwake huwa rahisi hivyo kama madaktari walipewa kipaji cha masomo hayo na hivyo hayakuwa magumu kwao ndo maana walifaulu, au la walilazimisha? Hivi unapoamua kusomea udaktari kuna mahali unaambiwa kuwa hii taaluma ni muhimu kuliko nyingine zote na kwamba malipo yake yanatakiwa kuwa zaidi ya wengine? Madaktari kumbukeni majibu mliyokuwa mkiyatoa wakati mlipochagua taaluma yenu, tuliwasikia mkisema napenda kuwa doc ili niwasaidie wagonjwa na kuokoa maisha ya watu. Leo hii mmetugeuka na kuanza kudai mishahara ya wabunge na mawaziri. Kila taaluma ina nafasi yake katika jamii na si nyie pekee
 
Wakati Kikwete anachukuwa madaraka mshahara wenu ulikuwa haufiki 180,000/= yeye ndiye aliyewaongeza mpaka kufikia hapo mlipo. Na mwaka huu kawaongeza sio chini ya 15% na amesema bado ataendelea kuwaongeza kila inapowezekana.

Tena huo ni wa kuanzia tu. Ni wapi watu wasio na ujuzi wanaanza kazi kwa mshahara huo Tanzania hii? Bado hamuhesabu, nyumba na marupurupu mengine kibao ambayo wenzenu hawapati.

Wakati mshahara ukiwa 180,000:
Gunia la mkaa lilikuwa elfu 6, ningeweza kununua magunia 30
Leo mshahara laki 9 gunia la mkaa ni elfu 40 naweza kununua magunia 22
Wakati mshahara ni 180,000 gunia la mahindi lilikuwa elfu 6 na ningenunua magunia 30.
Leo laki 9 gunia la mahindi ni elfu 60 naweza kununua 15 tu
The list goes on and on
Sukari, maharage, chumvi, nauli, dizeli na petrol, gas na mafuta ya taa, mchele
Cement, mbao, nondo, mabati...nk nk nk
Kwa kifupi laki tisa ya leo ina nunua asilimia 50 hadi 60 ya nilichoweza kununua na laki moja na elfu 80 wakati ule
Tafsiri rahisi isiyohitaji shule ni kuwa wakati mshahara iumepanda mara 5, gharama za maisha zimepanda mara kumi
Hoja ya kupandisha mshahara ni null and void na inaudhi mkitoa takwimu kama vile watu wote ni wajinga!
 
Ubongo Silaha Wewe bado tu unatumia mkaa halafu unakuja kujidai na kujisifu humu ndani? nyie ndio wale waharibifu wa mazingira, mimi nabofya gas tu. Swaafi na mazingira natunza.

Hesabu zako umekosea sana tena sana. Jaribu tena.
 
Last edited by a moderator:
Dah hapo nipite tu mimi, maana ugomvi wa Panzi Furaha ya kunguru, Maana kada za Uhasibu hazitajwi sijui sisi ndo hatufanyi kazi katika mazingira hatarishi! Maana kitendo cha kukaa na Mamilioni ya Watu kila siku ni zaidi ya Mazingira hatarishi, Maana ukiziiba tu Unanye.a Kopo, Sijui na sisi tudai Allowance ipo? Maana iyo Tsh. 446,000/= tunayolipwa na ukikata kodi kinabaki kituko! Na hapo unataka mwanao asome International School.

Umenigusa bwashee!, inabidi tushirikiane kwa karibu sana (wahasibu - uhasibu na wahasibu - ukaguzi) ili tuangalie jinsi ya kujilipa wenyewe maana kugoma hatuwezi, kuacha kazi hatuwezi na hakuna anaetujali!
 
Madaktari kama mshahara mdogo katafute sehemu ya kulipa vizuri hakuna tatizo serikali hawana uwezo wa kuwalipa kama mnaona Udokta haulipi basi ingieni kwenye siasa.

Pathetic!
Kwa hiyo unakubali kuwa Siasa ndio fani inayolipa?
No wonder we are still poor after 50 yrs
Bajeti ya wanasiasa haikosekani
Bajeti ya madokta hakuna
Bajeti ya wahandisi hakuna
Bajeti ya askari hakuna
Bajeti ya utafiti na sayansi hakuna
Bajeti ya elimu hakuna
Bajeti ya afya hakuna
Ya TISS ili kulinda wanasiasa ipo
Ya magari ya washawasha ipo
Ya wanasiasa hadi inafurika
Kwa nini tusiwe masikini??
 
Ubongo Silaha Wewe bado tu unatumia mkaa halafu unakuja kujidai na kujisifu humu ndani? nyie ndio wale waharibifu wa mazingira, mimi nabofya gas tu. Swaafi na mazingira natunza.

Hesabu zako umekosea sana tena sana. Jaribu tena.

Huna ile kiungo muhimu sana ndani ya fuvu!, unajua kipindi hicho anachosema Gas ilikua bei gani?, mtungi wa kilo 15 ulikua elf 7, leo je?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom