Mshahara wa serikali PGSS 14

Mimi naomba kujuwa tofauti ya PGSS na PUTS?
Tofauti ni kwamba PGSS ni mfumo wa mishahara ya mashirika ya umma au wafanyakazi wasio wanataaluma katika vyuo vikuu (chini ya TCU) na taasisi za elimu ya juu za umma (chini ya NACTE). Na PUTS ni mfumo wa mishahara kwa wanataaluma wa vyuo vikuu vilivyo chini ya TCU na taasisi za elimu ya juu za umma chini ya NACTE zinatumia mfumo wa PHTS ila mafungu ya PHTS yako juu kuliko ya PUTS.
Asante natumaini umenipata
 
Kamateni kazi jamani kama mmezipata na muwatumike watanzania kwa moyo kwa mishahara hiyo si haba bwana, take home ni kama shilingi 790.... hadi 800...
 
SINA HAKIKA NA VIWANGO VYA SASA KUTOKANA NA NYONGEZA ZILIZOFANYWA. LAKINI NGAZI HIYO NI YA JUU KATIKA MAAFISA WA SERIKALI SENIOR/KARIBIA PRINCIPAL OFFICER. Mwenye figure akupatie

Wale watu wa parastatal organisations wanaweza wakasema kitu maana hiyo iko applicable huko.Serikali kuu kuna TGS,TGTS,TGOS etc.
 
Tofauti ni kwamba PGSS ni mfumo wa mishahara ya mashirika ya umma au wafanyakazi wasio wanataaluma katika vyuo vikuu (chini ya TCU) na taasisi za elimu ya juu za umma (chini ya NACTE). Na PUTS ni mfumo wa mishahara kwa wanataaluma wa vyuo vikuu vilivyo chini ya TCU na taasisi za elimu ya juu za umma chini ya NACTE zinatumia mfumo wa PHTS ila mafungu ya PHTS yako juu kuliko ya PUTS.
Asante natumaini umenipata

Ohoooo............
 
Ahsante sana, nimekuelewa vizuri... lakini mbona hata wasio wanataaluma (non-academic staff) katika vyuo vikuu, mfano UDSM kwa Lab scientists wanalipwa kwa mfumo wa PUTS?
 
Mkuu hapo kwenye nyekundu labda kama wameanza hivi karibuni. Lakini nakumbuka rafiki yangu wa karibu mwenye master degree aliyeajiriwa kama Lab Scientist hapo UDSM alikuwa analipwa kwa PGSS. Ili kuondoa pengo kubwa lililokuwepo kati yao na teaching staff ilibidi Lab. Scientist waongezewe kitu kinaitwa risk allowance kwenye mishahara yao na kuwafanya kuwa na take home sawa na teaching staff waliosawa nao kielimu.
 
Lab Scientists wanalipwa scale inayoitwa PUSS, sio PUTS. Hata hiyo PUSS haiji automatically, lazima uombe re-categorization from PGSS to PUSS iwapo umefikia level fulani ya utumishi, na usipoomba utabaki na PGSS ambayo ndiyo ipo by defaulty. PUSS ipo juu kidogo kuliko PGSS, lakini ukipewa hiyo unaondolewa sifa za mafao fulani kama vile overtime (kama itakuwepo), kwani utakuwa umeingia scale ya seniors. Kuna watu hawapendi kwa makusudi kuiomba PUSS kwa mtego wa overtime, hata kama wamefikia level ya kuwa na sifa za PUSS! Hiyo PUTS kama ilivyoelezwa hapo juu, ni ya academic staff
 
Ahsanteni wakuu kwa maelezo toshelezi!
 
Mkuu hapo kwenye nyekundu labda kama wameanza hivi karibuni. Lakini nakumbuka rafiki yangu wa karibu mwenye master degree aliyeajiriwa kama Lab Scientist hapo UDSM alikuwa analipwa kwa PGSS. Ili kuondoa pengo kubwa lililokuwepo kati yao na teaching staff ilibidi Lab. Scientist waongezewe kitu kinaitwa risk allowance kwenye mishahara yao na kuwafanya kuwa na take home sawa na teaching staff waliosawa nao kielimu.

Mkuu ikiwa Lab scientist na Teaching staff wenye viwango sawa vya elimu wanakuwa na take home sawa, nini faida ya kuwa teaching staff (wakati wanakazi kubwa sana kuliko lab scientists), imagine wanafundisha lakuni hawana overtime kama lab scientists, teaching staff wanafanya kazi za kusahihisha mitihani hadi majumbani kwao (wakati huo scientist anakula good time).

Vile vile wanatakiwa wa publish papers ili wapande madaraja, lakn hilo halipo kwa scientist, scientist anapanda daraja kwa elimu yake na uzoefu wake kazini! Kwanini watu wanang'ang'ania kuwa teaching staff? Kwanini wasi ji re-categorize kuwa ma lab scientists?

Kuuliza si ujinga!
 
Back
Top Bottom