Mshahara kima cha chini wizi mtupu

Masanja, mkuu nimekusoma vizuri na nimefurahia sana mchango wako, unaonyesha kuwa umepangilia vyema maoni yako!
You have some valid points lakini mimi bado nasisitiza ya kuwa 135,000 shs hata nchi kama Thailand ni pesa nyingi sana. tofauti ni kuwa bei za vifaa Tanzania ni za UK, kwa sababu hatuzalishi kila kitu tunaagiza kutoka nje, viatu vya nje, kalamu tunaagiza kutoka nje, etc. Wakati wenzetu wale Asian Tigers wana viwanda vyao vya kuzalisha. Na ndo nimeuliza uzalishaji wa mwalimu.
Hilo la mwalimu wa primary kuwa na mchango mkubwa ningekubali kama kweli walimu hawa wangekuwa wako katika standard (siyo wale waliofeli form 4) na kama wangekuwa kweli wanafundisha siyo kuvizia ku-chaji watoto tuition. Hivi unaona siku hizi knowledge ya watoto wetu wanaotoka shule? Inabidi kama mwajiri uhangaike kuwapa elimu upya! Ni aibu!
Mi nimeshasema serikali haiwezi kuMANAGE effectively anything, kheri private sector. Na ndo maana nasema serikali ingekubali uanzishaji wa Charter school kama kule Marekani ili shule ziwe run by private sector with government subsidy ili watoto waweze kugharimu elimu ya shule binafsi.
Kuhusu walimu, tatizo tuna walimu wengi wa primary ambao hawafai katika kazi zao, wale ambao ni truly qualified hawako katika public sector. So ndo maana hata mshahara ni relative to their ability (at least that is the view in general), and my respect for the few exceptions. Lakini mi naendelea kusema tusitake kuishi beyond our means, awe mwalimu au mkurugenzi. Na mishahara itakapokuwa realistic hata bei zitakuwa realistic.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom