Msemakweli kasema ukweli kuhusu mafisadi wa elimu?

Mmakonde nakupa senksi
kinachoonekana hapa ni kundi la mafisadi wengine ambao labda nao wako katika mkondo huo huo wa kupata hizo fake Phds, sasa wanawashwa na Msemakweli.

Kama hutaka usisome, na TUC imewashauri wapeleke vyeti vyao kujisafisha sasa tatizo liko wapi, siwapeleke.

Na mwisho kama hilo halitoshi ili wajisafishe zaidi wanede mahakamani kumshitaki Msemakweli si kawachafua.

Acheni udwanzi wa kuteteana hapa ni mafisadi na Msemakweli Big Up, huu ni mwanzo mzuri, with spelling mistakes or not... ujumbe umefika loud and clear!!!

Wasalaam

Hii one track mind mentality ya "if you are not with us 100% you are against us 100%" ni medieval indeed.

Inawezekana kabisa kwa hawa vihiyo wenye PhD feki kuwa na makosa na huyu jamaa akawa msanii anayetafuta pa kutokea tu bila ya kuwa na kitu concrete.

I refuse to look at the world with the lens of inauthentic simplicity, however dramatic and appealing that may seem.
 
Tuwe wakweli...Msemakweli amesema kweli kwa takwimu ambazo yeye anazo..Hivyo hao unawaita waheshimiwa kama Wamekashifiwa wende Mahakamani..kwani huko ndo haki hupatikana na Msema wongoi na Msemakweli atajulikana...sasa wewe ndugu yangu..unataka akupe reference ili iwe nini..alichokisema anakiamini kutokana na ushahidi aliokuwa nao...nway.. may be uko pamoja na hao mafisadi wa Elimu...But na wewe kosoa kwa hoja na sio as yo did..I hope ur Tsh 3000 is nothing kwa msemakweli...Kipi bora ur 3000 au to be Jailed..We vipi....Think critically pumbavuuu....!!!

Unless sheria zetu ziko tofauti lakini hao ni public figures so hawawezi kwenda mahakamani.
 
Unless sheria zetu ziko tofauti lakini hao ni public figures so hawawezi kwenda mahakamani.

Kama ni hivyo basi Mtikila asingefungwa kwa kumkashifu Nyerere au kuwekwa rumande kwa kumkashifu Kikwete. Wanaweza kwenda mahakamani kabisa kwa bongo, ingekuwa nchi za wenzetu wangejiuzulu tu ikaisha. Hawa ni watu binafsi kabisa linapokuja suala la sheria, kama kuforge huko kumefanywa na serikali kwa niaba yao basi wasishitaki. Vinginevyo wanatakiwa kuwaeleza wananchi ukweli wa tuhuma zao, ama mahakamani au kwa kuitisha press conference
 
Msemakweli kasema kweli au kasema uongo? KAMA KASEMA UONGO wale ambao wako "aggrieved" kwa nini wasichukue hatua? Jamani mbona watanzania tunakuwa wepesi wa kusahau? Juzi juzi Rostam, Mukono (mwanasheria), nk waliwaka kama moto wa petrol walivyoambiwa kwamba ni mafisadi..wakasema wanakwenda mahakamani! What happened? Did they go? Hurraaaay! Niambieni Masanja mwana wa Mkulima!

The same kwa huyu Msemakweli. Inawezekana amekosea uandishi, hakutumia "scientific language" inayokubalika na wasomi humu...nk....lakini central issue ni kwamba watu aliowataja waligushi vyeti au walivipata vyuo ambavyo havitambuliki! Au wanadai kuwa na taaluma ambazo hawana! Either way ni waongo!. Na mbona hatujamuona hata mmoja anaita press conference kama walivyozoea kujitetea? Please people lets be honest. Tuache kutetea hizi mediocricy na incompetence za viongozi wetu.

Infact To me naona, Msemakweli amekuwa BOLD enough kufanya kitu ambacho watanzania wengi tunaogopa. (Unajua watanzania sisi wengi ni walalamishi..lakini ukija mda wa kutenda wengi tunajificha nyuma ya pazia...kusubiri nani ataanza.....) Tuache huu ujanja ujanja wa kukwepa issues. Kwangu mimi kitendo cha kuwasema mawaziri kwa kuandika "kitabu" ni jambo la kishujaa ambalo no body has ever done.

Lakini ushangae sasa..hata humu JF tumeshakuwa na thread kibao za degree fake za akina Nchimbi na Kamala. Lakini kelele zinaishia humu humu JF. Msemakweli kaenda mbali kidogo na kusema what he knows...hapa wanakuja JF EXPERTS NA PREMIUM MEMBERS kumuhukumu Msemakweli....Aliyekashifiwa akadai mabilioni mahakamani. Period.
 
You spot....ameeleza bila kuweka reference. Hata kama allagetion zake ni za kweli, siwezi kuamini kwa sababu hajatoa sababu za kuniaminisha. Tufikirie inside and outside, left and right, top and down, parallel and perpendicularly.

Msemakweli anaweza kuwa kasema kweli, but what is the authentication anayoyasema. Kila mtu akipublish speculation zake itakuwaje nchi hii?

Hivi unadhani waliotuhumiwa wangekuwa wamesingiziwa wasingeenda mahakamani kufungua kesi ya defamation?Kuna tofauti kati ya kitabu cha kitaaluma na non-fiction kama aliyoandika Msemakweli.Hakulazimika kuweka reference.
 
Watanzania tuwe makini kuwatambua mafisadi na vibaraka wao serikalini!!! Kumbukeni ni wangapi waliojaribu kuhoji tu kwenye public wakawekwa ndani... sasa msemakweli mpaka amechapisha kijarida, sijasikia ya makeke ya viongozi wetu ya kuwahi mahakamani

Lets be fair, there is some truth kutoka kwa msemakweli ndio maana wanamgwaya kumnyamazisha

perhaps niko wrong
 
Mimi sijakisoma kijitabu hicho, na wala sina haja ya kuepewa references au authetications zozote kujua kuwa cheti cha elimu kilichotolewa na degree mill siyo halali. Ni vivyo hivyo, mtu yeyote anayedai kuwa na elimu inayoendana na cheti hicho, ingawa "hakugushi cheti" chenyewe atakuwa "amegushi elimu" anayodai kuwa nayo kwa kupitia cheti hicho. Mtu wa aina hiyo haruhusiwi kabisa kujipatia" ....all Rights, Privileges and Responsibilities Thereunto Appertaining" na elimu anayojifanya kuwa nayo.

Mtu kujiita Dokta huku hana elimu ya udakitari, ni kujipa rights na privileges za udakitari ambazo hastahili, mtu huyo anagushi elimu. Hebu fikiria mtu atakayekuja na MD ya kutoka degree mill na kujidai hakugushi cheti na hivyo anataka kuwafanyia watu upasuaji wa moyo; atakuwa anagushi ujuzi asiokuwa nao. Yaani atakuwa amejipa responsibilities asizostahili

Ripoti ya awali ya bwana Msemakweli ilikuwa inahusu mawaziri na wabunge kama vile Chimbi, Mahanga, Nagu, Kamala, na Dialo ambao wanajulikana wazi kuwa elimu zao zimetoka kwenye degree mills zinazojulikana. Kwa vyovyote viule, watu hawa wamegushi elimu hizo na wanafanya makosa kwa kuendelea kujipatia privileges ziendazo na elimu hizo huku wakijua kuwa hawazistahili.
 
Mafisadi wana mbinu nyingi ndg zangu!....huyu nae nina mashaka km siyo kibaraka wao na kwa kweli naunga mkono ale ugali wake akalale kuliko kuleta uchovu humu.
 
Wewe KIRANGA umenielewa vizuri haswa. Ni dhahiri unaelewa maana ya kufanya utafiti. Mimi ningekuwa Msemakweli ili niheshimike na nisitoe nafasi ya kushambuliwa na wasomi wenzangu kajarida hako au kitabu hicho ningeandika kisayansi. Sasa hakana hata sifa ya kuitwa kitabu wala msomi mwingine akitaka kukirejea unakirejea vipi? Mimi siungi mkono ubabaishaji na ufisadi wa kielimu wa baadhi ya viongozi wetu. Kwa nini yeye Msemakweli hakwenda mahakamani kuwashtaki hao wahusika? Baadhi ya wachangiaji wanadai eti hao viongozi ndiyo waende mahakamani kumshtaki Msemakweli. What a suggestion!!

Msimamo wangu uko pale pale approach aliyoitumia Msemakweli si wa mtu aliyeenda shule.
Najua baadhi yenu nimewaudhi lakini ninachoweza kusema ni poleni. Yeye si mwanasheria? Aende mahakamani. Kama hawezi hiyo kesi amuuzie Mtikila ambaye ndiye bingwa wa kwenda mahakamani. Mauzo ya kijarida kake part of the proceeds amlipe Mtikila ili aende mahakamani.
 
yaani Tanzania kipimo cha kuwa mtu ameonewa ni kwenda mahakamani! hata kama kweli muhalifu, akifika tu mahakamani basi msafi.

au kama ni dhaifu umeonewa usipoenda mahakamani basi wewe una makosa

Au kama umemchukulia mtu mjinga(ukapuuza), ukaona ukae kimya basi Tz wewe ndio unaonekana mchafu


Haya nawapelekea hawa mafisadi wa elimu mahakamani nataka mwongozo wa sheria na standard ya kuwahukumu!

I repeat nataka akina Nchimbi na wenzake waende jela kwa kusoma non accredited university, diploma mills n.k , nataka kipengele cha sheria cha kuwahukumu na standard bora ya elimu ya nchi yetu

ukiona tunakubali la Msemakweli, lazima tujue kuwa hapa tulipo hatujafika bure, we have no direction, principals, laws, standard n.k yaani tunajudge watu au vitu kulingana na mwonekano wao! what a shame!!
 
Ndugu Kibanga umekasirika kwa sababu nimetoa arguments za kisomi au? Narudia kusema I decided to challenge Msemakweli on his own ground. Yeye kaja na maelezo hayo akijifanya kuwa ni msomi ilihali katuletea umbea. Nimesema mimi nisichokubaliana naye siyo kuwa hao waheshimiwa ni wasomi fake au kinyume chake. Hapana. Mimi ninasema hoja zake hazina msingi wa kisomi. Ndugu Kibanga try to control your emotions by being objective. Kuandika hapa hata kama nigetakiwa kulipa ningelipa tu. Sema sasa la sivyo just shut up man!!

Mkubwa Marigwe
Nikupongeze kwa hoja zako makini, binafsi nimesoma hicho kitabu na sikuona uthibitisho wowote kuhusu awa mabwana. Ni kweli kwamba waheshimiwa wetu wana degree za kununua lakini hii haimpi mtu fulsa ya kuandika speculation, mie leo hii naweza kuibuka na kusema fulani amenunua degree lakini bila ya uthibitisho hoja yangu haitokuwa na nguvu. Kwa watu makini sidhani kama wanaweza kushabikia kijarida cha Msemakweli. Yeye kama angependa jarida lake litumike kwa kizazi kijacho kama reference angeweka publishers na mwaka wa kuchapishwa lakini hivi havipo. Leo hii mtu akisema ni kijarida kaandika mwenyewe na kuprint nyumbani kwake kisha kutoa copy nani atabisha?
 
Mathias asante sana kwa kuwa mwelewa. Wewe umeenda shule. Umenielewa vizuri. Nisemalo mimi ni kuwa Msemakweli anadai yeye kasoma basi nilitegemea literature yake ambayo ni research ingeonekana kisomi pia ili ajipambanue na hao anaowatuhumu.
Mwaka 2005 ndugu Alfred Ngotezi alishindwa kura ya maoni kwenye jimbla Buchosa huko Sengerema na Mheshimiwa Chitalilo. Alilalamika kuwa mheshimiwa katoa taarifa za uwongo kuhusu elimu yake. Hakuishia kusema na kulalamika tu bali alisafiri hadi Uganda akaenda kwenye shule na vyuo husika ambao nao wakatoa ushahid wa kimaandishi ambao ulithibitisha kuwa Chitalilo kadanganya. Ngotezi akapeleka malalamiko CCM na kwa DCI. DCI summoned the MP. Of course baadaye suala hilo likazimwa kwa sababu wangelifuatilia kama la Kihiyo Temeke Chitalilo na CCM wangepoteza. Na CCM haikuwa tayari kupoteza au kwenda kwenye bye election. Lakini nina hakika 2010 Chitalilo hata akishinda kura ya maoni hatarudi. Angalau Ngotezi proved his case scientifically.
 
Hivi kuandika kwamba fulani amesomea "shahada" yake chuo ch Pacific University huko USA (mfano) ambacho hakitambuliwi na mamlaka husika ya kudhibiti viwango vya elimu katika hiyo nchi, inahitaji "literature" gani? Perhaps Iam naive, lakini naona watu hapa we simply want to argue for the sake of arguing. Na siyo kuangalia hoja. Who doesnt know kwamba Pacific University siyo chuo kinachotambuliwa? Or wee need to "cite" scientific sources? Please people...

Hapa hakuna short cut wala nini. Its simply the fact that Mama Nagu, Nchimbi et al "wamesoma" vyuo ambavyo havina sifa ya kutoa hiyo elimu. Sorry its a bitter reality. Kama umesoma chuo ambacho "hakiexist" you should remain outside the spotlight. Kuendekeza ujinga wa hawa "wasomi" ni kudhihaki watu wanaohangaika usiku kucha wakitafuta hivi vyeti kihalali.

Shame on them, shame on their apologetics!
 
Ndugu Masanja naona nihame kidogo kutoka kwenye mada ya msingi. Kuna kitu kimoja ambacho naona baadhi ya Watanzania wanapenda kuiga vitu ambavyo wakati mwingine huwa hawaelewi chimbuko lake na bila ya kuzingatia itifaki. Na hili nimeliona kwa MCs wengi. Utakuta wanapomtambulisha mtu wanamuita mheshimiwa ilhali hana sifa za kiitifaki kuitwa mheshimiwa. Unamkuta hata mbunge anapojitambulisha anasema "mimi naitwa mheshimiwa Marigwe" wakati adabu ya lugha inataka ujiite tu mimi ni Marigwe. Sasa uje ukutane na wasanii au hata waganga wa kienyeji "mimi naitwa profesa Marigwe". Kwa hali hii ambayo ilikuwa ni speciality ya wasanii wanasiasa nao kutokana na usanii wao nao wametumbukia huko mpaka kutafuta vyeti fake. Ili aitwe tu Doctor Marigwe wakati hizo sifa hana. Wanasiasa wengi wa Tanzania wanalewa na titles kabla ya majina yao. Ni wenda wazimu wa kijinga tu. Jitu lilipokuwa secondary likuwa failure sasa limepata hela kwa njia ambazo pia za kiujanja na kilaghai anataka ili akamilike aitwe profesa. Hao ndiyo wazazi amabo wako tayari watoto wao waibie mitihani. Jamani hili linatisha. Ndiyo maana weledi unapotea pole pole. Unamkuta mtu wa cheo cha Juu mahakamani au Polisi hajui hata vipengere vya kawaida vya sheria iwapo ni kosa au siyo kosa kwa raia kuwa pingu mpaka miundwe tume. Hivi leo inakuwaje hukumu ya High Court iruhusu mgombea binafsi na Attorney General asielewe the full implications za ruling hiyo avute miguu karibu mwaka mzima kukata rufaa? Ni ukihiyo all the way ndugu zangu
 
Kwa nini usahihishe kazi iliyoandikwa kwa lengo jingine.

Uliambiwa hii ni academic publication? Gundua lengo na mwandishi na utaona jinsi alivyofanikiwa.

Usijejikuta uko kundi hilo hilo la vyeti feki na unahangaika kujisafisha.\
 
Msemakweli ni mtu ambae Mtanzania yeyote anaeipenda nchi hii atamuunga mkono kwa kazi nzuri ya ujasiri aliyoifanya ya kuwaumbua hawa mafisdi wa elimu. Nasema huyu bwana anastahili pongezi kwasababu athali za kupuuzia hawa wezi wa elimu kwa Taifa letu ni kubwa na mbaya sana na nisawa na athari za ufisadi mwingine wowote ule. Mafisadi hawa wa elimu kama mafisadi wengine wanatumia njia za mkato kupata heshima ya elimu wasiostahili; na kama hatuthibiti tabia hii vijana wetu wengi wataacha kusoma vizuri na kupata elimu stahiki kwasababu wataona kuna wengine wanapata shahada wanazozihitaji kwa njia ya mkato na matokeo yake tutakuwa na watu wanaojiita wasomi kumbe ni vihiyo na nchi haiwezi kuendelea! Kwakutambua hasara nchi yetu itaipata kwa kuendekeza ufisadi huu wa elimu naunga mkono juhudi za huyu Msemakweli na ningemuomba apanue wigo wa utafiti wake mpaka wabunge wetu kwenye baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki kwani kule kuna PHD fake kama mbili hivi zinasinzia na kutuabisha kwa michango yao dhaifu!!
 
jamii inahitaji haki na si taratibu za wazungu kuanza kuhoji mambo kupoteza uhalisia,

big up msemakweli
 
Ndugu Masanja naona nihame kidogo kutoka kwenye mada ya msingi. Kuna kitu kimoja ambacho naona baadhi ya Watanzania wanapenda kuiga vitu ambavyo wakati mwingine huwa hawaelewi chimbuko lake na bila ya kuzingatia itifaki. Na hili nimeliona kwa MCs wengi. Utakuta wanapomtambulisha mtu wanamuita mheshimiwa ilhali hana sifa za kiitifaki kuitwa mheshimiwa. Unamkuta hata mbunge anapojitambulisha anasema "mimi naitwa mheshimiwa Marigwe" wakati adabu ya lugha inataka ujiite tu mimi ni Marigwe. Sasa uje ukutane na wasanii au hata waganga wa kienyeji "mimi naitwa profesa Marigwe". Kwa hali hii ambayo ilikuwa ni speciality ya wasanii wanasiasa nao kutokana na usanii wao nao wametumbukia huko mpaka kutafuta vyeti fake. Ili aitwe tu Doctor Marigwe wakati hizo sifa hana. Wanasiasa wengi wa Tanzania wanalewa na titles kabla ya majina yao. Ni wenda wazimu wa kijinga tu. Jitu lilipokuwa secondary likuwa failure sasa limepata hela kwa njia ambazo pia za kiujanja na kilaghai anataka ili akamilike aitwe profesa. Hao ndiyo wazazi amabo wako tayari watoto wao waibie mitihani. Jamani hili linatisha. Ndiyo maana weledi unapotea pole pole. Unamkuta mtu wa cheo cha Juu mahakamani au Polisi hajui hata vipengere vya kawaida vya sheria iwapo ni kosa au siyo kosa kwa raia kuwa pingu mpaka miundwe tume. Hivi leo inakuwaje hukumu ya High Court iruhusu mgombea binafsi na Attorney General asielewe the full implications za ruling hiyo avute miguu karibu mwaka mzima kukata rufaa? Ni ukihiyo all the way ndugu zangu

Inaonekana umebadili mawazo,ni jambo jema,tofauti na hapo chini,juu unaonyesha kukubaliana kuwa msema kweli kasema kweli?

Marigwe said:
4. Kijarida cha Msemakweli ni majungu ambayo yamejaa fitina na chuki tu. Naomba mnielewe. Mimi sijasema kuwa hao Waheshimiwa wana vyeti halali au vya kughushi. Mimi niachosema ni kuwa maelezo ya Msemakweli hayawezi kukubalika kirahisi bila ya kuwa “authenticated scientifically”. Na huo ndiyo usomi. Msemakweli anadai kuwa waheshimiwa hao ni mafisadi wa elimu na yeye je? Kundi lake ni lipi. Anajiita mwanasheria. Hivi mwanasheria utafanya madai bila ya kuyathibitisha na vielelezo?

Sijui sasa authentification unahitaji ya nini na wakati umeshakiri kuwa hayo yote aliyosema msema kweli ni kweli?ama macho yangu?Ni bora ufafanue kama nimekuelewa vingine.
 
JMushi1 mimi sisemi kuwa hao waheshimiwa wanavyo vyeti genuine. Hapana. Mimi ninachofanya ni kumsaidia Msemakweli kuwa katika nyanja ya maandishi ambayo yamefanyiwa utafiti anatakiwa awe na supporting documents. I am not challenging the contents of his article. No. I am challenging his style of presentation in that it lacks intellectualism and authenticity taking into account that he claims to be a learned brother. In other words he claims to be an intellectual while he is actually suffering from intellectual dishonesty as well. That is all. Hayo aliyoandika angeyathibitisha na documentation na kama ni thesis ningempa hata cheti au hata honorary PHD. Ni hilo tu. Otherwise tuko pamoja kuwa sikubaliani hata kidogo na ukihiyo.
 
MAFISADI WA ELIMU

Jana nilikinunua kijarida kilichoandikwa na Ndugu Msemakweli, Kijarida hicho kinauzwa shs 3,000.
Na kwa sababu sisi watanzania tunapenda sana habari za umbea kwa upumbavu tulionao tutanunua tu hicho kijarida na yeye atapata hizo pesa bila ya jasho.

So kumbe na wewe umenunua,so na wewe ni mmoja wa Watanzania MABWEGE..
Hiv hao jamaa waliokashifiwa we ndo msemaji wao!!!wamekutuma..mbona wao wako kimya..kitu gani kinakuwasha hadi ujipe kazi ya kuwatetea..unalipwa???
Nina mashaka sana na uwezo wako wa kufikiria..umekiita kijarida feki,then umekinunua..unashanga sana ndugu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom