Msemaji wa Ikulu aikingia kifua ndege ya Raisi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::6/17/2008
Huu ulikuwa ni mradi mwingine wa fisadi Mkapa alioufanya akiwa amebakisha miezu mitatu kumaliza awamu yake. Wakala alikuwa ni yule yule mhindi aliyelipwa 'commission' ya $12 million katika ununuzi wa rada iliyogharimu $42 million

Msemaji wa Ikulu aikingia kifua ndege ya Raisi

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

WAKATI wasomi na baadhi ya wabunge wakitaka ndege ya kifahari ya Rais iuzwe, Ikulu imeikingia kifua ikisema ndege hiyo haiwezi kuuzwa kwani bado inatumiwa na mkuu huyo wa nchi.

Kauli hiyo ya Ikulu imekuja wakati wasomi na baadhi ya wabunge, wametaka ndege hiyo iliyonunuliwa kwa sh 42 bilioni ipigwe mnada, kwani imekuwa ni hasara kwa serikali kwa kuchangia matumizi mabaya ya fedha za umma.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, alisema ndege hiyo bado ni muhimu kwa matumizi ya safari za Rais.

Rweyemamu alifafanua kwamba, siyo kwamba ndege hiyo haitumiki kabisa bali inatumika wakati ikibidi kutumika.

''Ndege ya Rais inatumika inabidi si kwamba haitumiki kabisa kama inavyoelezwa. kwa mfano juzi juzi aliitumia katika safari ambayo ilimfikisha hadi Kampala,'' alisema Rweyemamu.

Rweyemamu alisisitiza kwamba, Rais ana hadhi yake hivyo ni lazima anaposafiri awe na ndege kama hiyo.


Mkurugenzi huyo wa Ikulu alifafanua kwamba, ndege hiyo ilinunuliwa kwa makusudi ya matumizi ya Rais ikiwa ni salama.

Alipoulizwa vipi ndege hiyo imekuwa haitumiki sana lakini inafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara tena nchini Marekani, ambako hutumia fedha nyingi, alisema matengenezo pia yanafanyika ikibidi si kila siku.

Alisema ndege hiyo haifanyiwi matengenezo bila sababu za msingi kama inavyoelezwa, bali hufanyiwa ikibidi.

''Rais ana hadhi yake, msafara wake na yeye mwenyewe lazima uwe salama, kwa hiyo matengenezo pia tukumbuke ni kwa ajili ya usalama wa Rais na msafara wake," alisema na kuongeza:

''Ndege inayo mbeba Rais lazima iwe salama, yeye na msafara wake wanahitaji usalama wakati wa kisafiri.''

Wiki iliyopita wasomi na wachumi waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kampuni ya Ernst&Young, walitaka serikali kupunguza matumizi yasiyo na msingi, ikiwa ni pamoja na kuuza ndege hiyo.

Baadhi ya wasomi ambao ni wahadhiri kutoka Chuo cha Kilimo Sokoine (Sua) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walisema licha ya ndege hiyo kutotumiwa na Rais bado imekuwa ikifanyiwa matengenezo mara kwa mara nchini Marekani.

Katika hatua nyingine, Ikulu imesema ingependa kuona duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa wa Zimbabwe hapo Juni 27, unakuwa huru na haki.

Rweyemamu alisema ni wakati wa kuomba Zimbabwe isiingie katika machafuko, akasisitiza kwamba Tanzania ingependa kuona haki na matakwa ya raia katika kuchagua yanazingatiwa bila kukiukwa.

Duru ya pili ya uchaguzi nchini Zimbabwe inatarajiwa kufanyika Juni 27, hata hivyo tayari kumekuwa na hali ya hatari baada ya Rais Robert Mugabe kutangaza kuingia msituni iwapo upinzani utashinda, huku Katibu Mkuu wa Chama cha Movement For Democratic Change (MDC) Tendai Biti, akikamatwa kwa tuhuma za uhaini.
 
Salva unakazi kweli kweli ya kutetea visivyo teteeka!

Utauweka wapi uso wako siku ambao yote na hasara zote zinazo tokana na ndege hii ziatakapo wekwa wazi?

Kulinda ugali ni kazi kubwa sana, mpaka mtu unakuwa mtumwa wa nafsi yako kwa kulazimika kusema kwamba unakubaliana na kitu ambacho una uhakika hukubaliani nacho!
 
Hivi wamekwenda iwekea defence system kama Air Force One? Ka-Gulf stream ketu katarudi kakiwa na anti-missile mechanisim, special wax to prevent rain spots a special toilet that cleans the president without him using mkono and all sort of vikorombwezo.

Tuambieni Dege lina milage gani mpaka sasa, maana tuna mtalii pale Magogoni.
 
Huyu jamaa naona hata hiyo taaluma aliyonayo hamsaidii na hata kama ni kulinda kibarua tusifike huko tutakuja kuangamizana kisa kutetea ugali. haiwezekani watu wazima na akili zao tuseme kwamba hiyo ndege haifai na ni hasara kwa serikali ya nchi masikini kama hii lakini yeye anatetea kuwa ni kwaajili ya kulinda hadhi ya rais...kweli tunafikia mahali pa kulinda hadhi ya rais kwenye umasikini na ufisadi kama huu wakati Kagame anauza VX za serikali ili kuokoa garama sisi hapa tunatetea ndege?? ipo siku...
 
Ulaji wa watu huo jamani..................wakale wapi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Maumivu...........Uchungu...........Wizi..........Ubinafsi...........
 
Hivi wamekwenda iwekea defence system kama Air Force One? Ka-Gulf stream ketu katarudi kakiwa na anti-missile mechanisim, special wax to prevent rain spots a special toilet that cleans the president without him using mkono and all sort of vikorombwezo.

Tuambieni Dege lina milage gani mpaka sasa, maana tuna mtalii pale Magogoni.

Mchungaji, hapa ulikuwa una lengo la kuchangia mada au unataka kuuwa watu kwa vicheko. Teh teh kwi kwi, eti asitumie KONOZ. Ama kweli JF ina Utamu wa aina yake.
 
Mchungaji, hapa ulikuwa una lengo la kuchangia mada au unataka kuuwa watu kwa vicheko. Teh teh kwi kwi, eti asitumie KONOZ. Ama kweli JF ina Utamu wa aina yake.

Mnasemaje wenyewe wataalamu, fasihi au ? Maana kama dege kila siku lina mafua, inabidi tujiulize gharama hizi kubwa kila siku haba na haba zityatosha kununulia ndege mpya.

Lakini huwezi jua, labda tekinolojia mpya inasababisha tuipeleke upate KONOZ free toilet!
 
Back
Top Bottom