Elections 2010 Msekwa & Makamba: Ni Kweli CCM Ina Wanachama Million 5 Walio Hai?

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
  • Nimewasikia kupitia vyombo vya habari kwa nyakati tofauti Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara wakisisitiza kuwa CCM ina Wanachama Million 5 na kuwa hizo kura wana uhakika nazo.
  • Assume Tanzania ina Watu 43.2 Millioni
  • Wanye Umri zaidi ya Miaka 18 ni 60% = 26 Million (NBS)
  • Waliojiandikisha hadi sasa ni: 18 Million (NEC).
  • Assume waliojiandikisha katika vyama vya siasa kama Wanachama ni 25% ya 26 Million = 6.5 Million (My guess kutokana na uzoefu wangu wa ushiriki wa watanzania katika siasa, naweza kusahihishwa kama kuna mwenye data)
  • Kwa mtaji huo ina maana kama CCM inao 5 Million, upinzania una 1.5 Million.
  • Dr. Slaa anadai kadhaminiwa na Wanachama wa Chadema 1.3 Million (Si mikoa yote).
  • CUF inao wanachama wengi pia, 2005 lipumba alipata kura zaidi ya Laki 9. Huenda Wanachama wa CUF pia wameongezeka.
Swali na Msingi: Je ni Kweli na Uhakika kuwa CCM inawanachama hai Million 5?
 
Kama kwa haikika ina Wanachama Million 5 walio hai na Watiifu kwa CCM, basi ni dhahiri ushindi utakuwa ni wa CCM.
 
Kwani kura za maoni walishiriki wangapi? Nakumbuka majimbo mengi ilikuwa kura jumla ziko chini ya 10,000. Wilaya nyingi zina majimbo mawili mawili. We can get something outta this.
 
Kwani kura za maoni walishiriki wangapi? Nakumbuka majimbo mengi ilikuwa kura jumla ziko chini ya 10,000. Wilaya nyingi zina majimbo mawili mawili. We can get something outta this.

Unahisi nini Mkuu?

Mwaka huu kuna Jumla ya majimbo 232 ya zamani Ongeza majimbo mapya nadhani yapo 7. Jumla Majimbo 239.

suppose kila jimbo lilikuwa na Kura 10,000. Then ina maana jumla ya kura ni Millini 2.32. Ina maana watu 2.68 hawakupiga kura.

Lakini pia historia inaonyesha kuwa turn up ya wapiga kura haifiki 100%. Je, hizo kura 5 Million zitapatikana zote?

Imekaaje hii?
 
Nikiwaona na kuwasikia hawa mediocre 2,Makamba na Msekwa nataka kuikana nchi yangu kabisa!
 
Uchaguzi wa Serikali za mitaa waliojitokeza walikuwa ni aslimia isiyofikia 62% ya waliojiandikisha.
 
Back
Top Bottom