MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, amewataka wabunge wanaolalamika kuwapo kwa fedha chafu zinazomwagwa majimboni mwao waache hadithi na badala yake wapeleke ushahidi.
Msekwa amesema ofisini kwake kuwa, madai hayo pamoja na ya CCM kutumia fedha za mafisadi, yamekuwa sawa na hadithi inayochosha.
Haya madai sasa yamekuwa kama hadithi hao mafisadi ni akina nani, tumechoka kusikia, ila ningeshauri kuwa wanaosema hivi wangewataja hao wanaozimwaga hizo fedha chafu na wanapozitoa, alisema Msekwa.
Alisema madai hayo ni moja ya dalili za kuwapo kwa vuguvugu la uchaguzi na wasiwasi, kwa vile sasa Tanzania inaelekea katika mwaka wake wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Kama nilivyosema hapo mwanzo haya yote ni vuguvugu na joto la uchaguzi watu wana wasiwasi na nafasi zao, wanasema tu lakini hakuna mwenye ushahidi, alisema.
Juzi gazeti moja la kila siku, liliwakariri baadhi ya wabunge wakilalamikia kumwagwa kwa fedha chafu katika majimbo yao, ili kuhakikisha kuwa nafasi zao zinachukuliwa na hawafurukuti katika uchaguzi ujao.
Gazeti hilo liliwataja wabunge hao kuwa ni Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (CCM) na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Wajumbe hao nao walidai kuwa watazipokea fedha zinazodaiwa kutolewa kwa ajili ya uwashawishi wa kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu mwakani lakini hawatadanganyika.
Nashindwa kuona kuchoka katika kauli hii! Naiona kama kauli ifaayo kwa utawala bora!
Ama kweli ile asilimia 70 aliyosema Kiwete haiko tunakofikiria tu bali hata miongoni mwa wanaojifanya wako katika asilimia 30 ya upande wa pili.