MAGEUZI KWELI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,947
- 253
Jehanamu ina wafuasi wengi sana....
mkuu, CDM hawatakuwa hivyo, ni watu makini na ndiyo maana hata watu makini hapa jamvini na kwengineko nchini huwaunga mkono...,
angalia gazeti ya TANZANIA DAIMA lilivyo na balance newz ingawa linamilikiwa na Chairman wa CDM!
Taarifa zilzopo ni kwamba Tanzania Daima linapendwa kuliko hilo la Uhuru, hata state house na taasisi nyingine ktk govt, Tanzania Daima linapendwa sana kuliko Uhuru...., hata JK ni mpenzi na msomaji mkubwa wa Tanzania Daima....!
uhuru sio gazeti.hata mleta habari anaogopa kutaja source yake.juzi nililisoma hili gazeti karibu nitapike.
Thursday, 11 August 2011 20:28
uhuru
newsroom
Wenye akili zetu tunaliamini gazeti la Uhuru kama tunavyoliamini gazeti la Tanzania Daima!
Kun watu wanaasema uhuru sio gazeti alafu hao hao wanasema chadema ianzishe gazeti na TV yake . Muelewe CDM wakiazisha gazeti litakuwa kama uhuru tu........
Kichwa cha habari (inaonesha imeandikwa tar 11/8/2011 Kama sikosei) kinaonesha kuwa Msekwa keshatinga Igunga na kukomba viongozi huko, lakini ukweli ni kuwa wakati habari hizo zikiandikwa alikuwa hajafika Igunga, amefika Igunga leo 12/8/2011. Kama alikomba mamluki wake huko Singida basi ni hukohuko ambako hakuna uchaguzi kwa sasa. Hapa Igunga mjini alipofikizia, ni CDM kwenda mbele, ushahidi ni kuwa hata Diwani wa hapa Kamanda Vincent ni wa Chadema ambae pamoja na kuwepo nguvu za Rostam katika uchaguzi mkuu uliopita alishinda kwa kura 19,000 dhidi ya Mama Ngese wa CCM alieambulia kura 800 tu! Watoa habari tujitahidi kuwa wakweli tusipotoshe wenzetu walio mbali, tutapoteza Credibility yetu.
<br />Hivi kweli viongozi wa CCM wanafikiri kwa kina kweli? Unawezaje kwenda kupiga kampeni kwenye jimbo liloachwa wazi na mwanachama wenu ambaye ameachia ngazi kwa sababu ya "siasa uchwara" na "siasa za maji taka"?<br />
<br />
Je, huko ni kukubaliana na maneno ya Rostam kuwa wao ni viongozi wa siasa uchwara, hivyo ni viongozi uchwara, wa chama cha siasa uchwara (yaani chama uchwara) ambacho kimeunda serikali uchwara?!!
Thursday, 11 August 2011 20:28
uhuru
newsroom
- Akomba vigogo wa CHADEMA
- Mbowe maji ya shingo Arusha
Na mwandishi wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeisambaratisha CHADEMA baada ya kuzoa vigogo wake wanne mkoani Singida. Vigogo hao walijiunga na Chama wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alipokuwa akiwasalimu wananchi katika kijiji cha Shelui, akiwa njiani kuelekea wilayani Igunga.
Waliojiunga na CCM ni wenyeviti wa wilaya za Iramba, Emmanuel Ntundu na Nakamia Wazaeli (Singida Mjini), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Iramba, Ela Dyelu na Katibu Mwenezi wilaya ya Iramba, Enelly Kingu. Msekwa aliwapongeza viongozi hao kwa uamuzi wa kujiunga na CCM na aliwataka kutimiza ahadi yao ya kuleta wanachama wengine 90. Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema kitendo cha wanachama hao ni salamu kuwa CCM inakubalika. Kutoka Arusha, Lilian Joel, anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika hali isiyo ya kawaida ameendelea kuwachochea wananchi kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Changa.
Akihutubia mkutano wa hadhara jana katika viwanja vya NMC, Mbowe alisema baada ya siku 30 atarudi Arusha kushirikiana na wananchi kuvamia ofisi za manispaa. Mbowe alisema sababu za uvamizi huo ni kupinga kitendo cha Changa kuwatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA.
"Tumesikia mkurugenzi ametamka anawatambua madiwani tuliowatimua, nawaomba wananchi, kesho tunarejea bungeni, baada ya siku 30 tutarudi kwa kazi moja tu ya kuandamana hadi katika ofisi za mkurugenzi na tutalala hapo na kushinda, alisema. Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, kujiandaa vyema kwa kukusanya askari kutoka mikoa ya jirani siku ya maandamano hayo.
Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho walifika Arusha kwa ajili ya kujisafisha kwa wananchi, baada ya kuwafukuza madiwani watano wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha kutoafiki kauli na wito uliotolewa na Mbowe wa kuandamana.
Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Marando, aliwasihi madiwani waliofukuzwa wasiende mahakamani, kwa madai hakuna atakayewatetea.
Madiwani waliofukuzwa ni Naibu Meya, Estomih Mallah, ambaye ni diwani wa Kimandolu, John Bayo (Elerai), Rehema Mohamed (Viti Maalumu), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rubeni Ngowi (Themi).
Last Updated ( Thursday, 11 August 2011 20:35 )