<br />mbona huwa mnaandika source: mwananchi, raia mwema, east african, sasa mbona hii haijaandikwa source? Mwenye akili anajua litakuwa aidha uhuru, jambo leo ama habari leo
uhuru hilo EEETI CHADEMA YASUSIWA ARUSHA
HAHAHAHAHHA SIJUI MHARIRI WAKE KASOMEA WAPI!???
Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.
Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga
Mchagga mwenzako katoa amri jana ujiandae kwenda kwenye maandamano sio kukaa mbele ya Laptop tu unaleta porojompuuzieni huyu mpuuzi na kilaza wa JF
<br />Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.<br />
Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga
Wale wote mateka wa Mbowe, ni amri sio ombi mnatakiwa mjiandae kuandamana kwenda kuvamia ofisi za Halmashauri kwa nguvu.
Mmepewa mwezi mmoja wa kujiandaa ili muandae visu na mapanga
Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!
[h=2][/h] Thursday, 11 August 2011 20:28 newsroom
* Akomba vigogo wa CHADEMA
* Mbowe maji ya shingo Arusha
Na mwandishi wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeisambaratisha CHADEMA baada ya kuzoa vigogo wake wanne mkoani Singida. Vigogo hao walijiunga na Chama wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alipokuwa akiwasalimu wananchi katika kijiji cha Shelui, akiwa njiani kuelekea wilayani Igunga.
Waliojiunga na CCM ni wenyeviti wa wilaya za Iramba, Emmanuel Ntundu na Nakamia Wazaeli (Singida Mjini), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Iramba, Ela Dyelu na Katibu Mwenezi wilaya ya Iramba, Enelly Kingu. Msekwa aliwapongeza viongozi hao kwa uamuzi wa kujiunga na CCM na aliwataka kutimiza ahadi yao ya kuleta wanachama wengine 90. Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema kitendo cha wanachama hao ni salamu kuwa CCM inakubalika. Kutoka Arusha, Lilian Joel, anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika hali isiyo ya kawaida ameendelea kuwachochea wananchi kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Changa.
Akihutubia mkutano wa hadhara jana katika viwanja vya NMC, Mbowe alisema baada ya siku 30 atarudi Arusha kushirikiana na wananchi kuvamia ofisi za manispaa. Mbowe alisema sababu za uvamizi huo ni kupinga kitendo cha Changa kuwatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA.
"Tumesikia mkurugenzi ametamka anawatambua madiwani tuliowatimua, nawaomba wananchi, kesho tunarejea bungeni, baada ya siku 30 tutarudi kwa kazi moja tu ya kuandamana hadi katika ofisi za mkurugenzi na tutalala hapo na kushinda, alisema. Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, kujiandaa vyema kwa kukusanya askari kutoka mikoa ya jirani siku ya maandamano hayo.
Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho walifika Arusha kwa ajili ya kujisafisha kwa wananchi, baada ya kuwafukuza madiwani watano wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha kutoafiki kauli na wito uliotolewa na Mbowe wa kuandamana.
Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Marando, aliwasihi madiwani waliofukuzwa wasiende mahakamani, kwa madai hakuna atakayewatetea.
Madiwani waliofukuzwa ni Naibu Meya, Estomih Mallah, ambaye ni diwani wa Kimandolu, John Bayo (Elerai), Rehema Mohamed (Viti Maalumu), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rubeni Ngowi (Themi).
Last Updated ( Thursday, 11 August 2011 20:35 )