Msekwa ashikilia siri za mapacha watatu

baraka boki

Senior Member
Sep 20, 2010
181
80
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, amekutana na viongozi watatu wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi, katika utekelezaji wa uamuzi wa kujivua gamba uliofanywa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) uliofanyika Dodoma Aprili 10 hadi 11, mwaka huu.

Yaliyozungumzwa katika kikao hicho yameelezwa kuwa siri kati ya Msekwa na watuhumiwa hao, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, lakini yalihusu agizo walilopewa watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa masilahi ya CCM, la sivyo wawajibishwe na chama.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM mjini Dar es Salaam, ilisema Msekwa
alikutana na viongozi hao kila mmoja kwa wakati wake na kuzungumza nao kwa faragha kama Makamu Mwenyekiti wa CCM na kama mzee wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Msekwa alikutana na viongozi hao Mei 26 mwaka huu na wa kwanza alikuwa Rostam ambaye ni Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Igunga. Walikutana saa 2.30 asubuhi.

Baada ya hapo kwa mujibu wa taarifa hiyo, alifuata Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC na wa mwisho alikuwa Chenge, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Bariadi Magharibi.

“Kwa vile Msekwa alikutana kwa faragha na viongozi hao mmoja mmoja, anayejua kilichozungumzwa ni Mzee Msekwa na wao peke yao,” ilisema taarifa hiyo ya CCM.

Gazeti hili lilizungumza na Lowassa, kutaka kujua kama alikutana na Msekwa na kama atachukua uamuzi wa kujivua gamba kama maagizo ya NEC yanavyotaka lakini baada ya kusikiliza hoja hizo, alijibu “No comment.”

Alipotafutwa Rostam, simu yake ilipokewa na msaidizi wake ambaye hakutaka kujitambulisha
jina, akasema Mbunge huyo yuko nje ya nchi na ameacha simu kwake. Chenge simu yake iliita bila majibu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua itakayofuata baada ya mazungumzo hayo ni kufikisha
kwenye vikao vya CCM taarifa ya mambo yaliyojiri wakati wa mazungumzo hayo na vikao hivyo vitatoa uamuzi utakaotangazwa kwa umma.

CCM pia imekanusha taarifa kwamba viongozi hao walipokutana na Msekwa walikabidhiwa
barua za kuwataka wajiuzulu na zile zilizodai kuwa barua hizo zimefungiwa kabatini na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

“Taarifa zote hizo zilizoandikwa na kutangazwa katika vyombo vya habari, si za kweli, ni uongo na uzushi mtupu. Hakuna barua iliyoandikwa, hakuna aliyepewa barua na wala hakuna barua iliyofungiwa kabatini,” ilifafanua taarifa hiyo. source: habari leo
 
Personally, sijui kwa nini Mzee Msekwa anajishughulisha na 'front line' pilitics hadi sasa hivi? Wazee wenzake wamestaafu au kuachana na huu usanii wa ccm na kama kushiriki kwao basi wamekuwa wakifanya hivyo kama washauri e.g Msuya, Salim Ahmed Salim, Warioba. Hawa wote walikuwa na Msekwa.

Kadri anavyoendelea na haya mazingaombwe ya vijana na mitandao yao ndivyo hivyo hivyo anazidi kujishusha hadhi. Na baya zaidi ni hili: anaonekana kuingilia 'ugomvi' usiomhusu! Magamba ni matokeo ya mtandao ambao kimsingi wajumbe wake wamegeukana, sasa yeye anataka kufukuza upande mmoja wa mtandao na kuacha mwingine 'jikoni' kwa msingi upi' na kwa maslahi ya nani? na je kweli ana uwezo huo? na je anachotetea ndicho hicho wakuu wake wanachotetea?

Mpaka hapo alifika inatosha, Msekwa angepumzika kwa amani atoe ushauri tu. Acha wafu wazike wafu wao!
 
Back
Top Bottom