Msanii wa bongo fleva anatafutwa kwa kuiba simu gesti

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
519
Msanii mkubwa maarufu mwenye jina katika bongo fleva O-ten ametuhumiwa kuiba simu alipokuwa kwenye show Geita amehojiwa mchana huu katika redio makini clouds fm amekiri kuchukua simu hiyo nokia tochi iliyokuwa ya dada wa gesti kwa madai kuwa hajalipwa na promota.na amedai kuwa hata wakienda polisi atawashinda kesi
 
Bila shaka huyo msanii ana mtindio wa Ubongo!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa huyo muhudumu wa gest ndiye Promoter wake??? Kwa nini asiibe simu ya huyo aliyempa kazi ya kuimba na badala yakekumuibia musichana wajameni!!!!!!!!!!!!!!

Tena simu yenyewe NOKIA ya tochi, hana hata aibu kidogo.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Huyu jamaa si ndio alitoa enzi za mwalimu ka songi kake kanaitwa nicheki,ndani ya ka songi kuna majisifa sana'sasa kweli kaiba kinokia cha tochi,au blackbery torch?
 
Jamaa alikuwa akiongea kama anabana pua hv maana yake nn?!!
 
Msanii mkubwa maarufu mwenye jina katika bongo fleva O-ten ametuhumiwa kuiba simu alipokuwa kwenye show Geita amehojiwa mchana huu katika redio makini clouds fm amekiri kuchukua simu hiyo nokia tochi iliyokuwa ya dada wa gesti kwa madai kuwa hajalipwa na promota.na amedai kuwa hata wakienda polisi atawashinda kesi

Huyo msanii kachoka kufikiri na kachoka mawazo. Mhudumu wa guest ndo promota?
 
Hebu nichekiii ninavyong'aaaraaa X2 nicheki nipo masaki na watoto wa kishua ,,,nicheki nina mapene kibao,magari na warembo kibao,,,, dah mbwembwe zote hizi kumbe jizi la kisimu cha nokia ya tochi!!
 
Hii habari nona kama vile haijakaa sawa...isije kuwa ni 'siasa' za maji taka tu!
 
Kwani huwa wanalipwa kiasi gani kwenye onyesho kama hilo?

Labda hakulipwa kiasi alichotaka so akaamuwa kujazia na hiyo tochi?

Otherwise kama ni kweli hajalipwa, basi promota akisema ngoma droo atakubali?

Duh!
 
Maisha magumu jamani! ila hakutumia busara kudai haki yake! jamaa kafulia kiasi hiki! KUTOJIPANGA!
 
inamaana hakupewa advance? anaonekana ni msanii wa kima cha chini sana kama hana hata pesa ya nauli ya kurudi zake dar au si angeenda kituo cha polisi na mkataba alioingia na huyo jamaa ili sheria ichukua mkondo wake?
 
me nikisikiaga ishu ya hivi huwa nafurahi sana mana najua c muda mrefu wasanii wengine nao wanaojifanya kuwa wapo juu kwa kufuja vijisent wanavyopata watakuwa hivi c muda mrefu, NICHEKI HADI SIMU YA NOKIA TOCHI DAAAAAHHH HII NOMA
 
hapo kuna jambo,simu ilikuwa wapi wakati anaibiwa,alijuaje kama oten ndio kaiiba?huyu dada anamausiano na huyo promoter? Asije akawa aliliwa bure na ten,kaamua kumpakazia tu.mwaga mboga nimwage ugali.
 
Back
Top Bottom