Msanii wa bongo flavor timbulo anacopy nyimbo za x-maleya wasanii wa camroon

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,644
68,593
Ebu Sikiliza hizi nyimbo kwanza:

Timbulo-Domo Langu Zito


x-maleya--Yelele(Domo langu zito remix)


Timbulo-Wa leo wa kesho


x-maleya--Tchokolo(wa leo wa kesho remix)


My Take:Wasanii umizeni kichwa mtakuja kuwa sued na hela hamna,hamkumbuki TID na Jamaa yule wa Nyota yako wa Comoro?

Ukiangalia kwenye youtube x-maleya wali-upload wimbo Mwezi wa 4 2009 kipindi hicho dogo nadhani analima viazi gairo hata DSM hakujui.
 
Last edited by a moderator:
dah huyu mwalimu mwenzetu kumbe hamna kitu anapiga chabo nyimbo za watu shame
 
That's very disappointing aisee, yaani dogo kaweka maneno ya kiswahili tu basi, ni wizi kama TID alioufanya kipindi kile, shame on u mwalimu timbulo
 
Looh jamaa feki kumbe

Ni zaidi ya feki amekopy nyimbo mbili kwa wasanii walewale,wkt wenzake wanakopy mara moja tu,nadhani baada ya kufanya vizuri domo langu zito akaona ngoja aibe wimbo mwingine,100% jamaa si msanii ni photocopy ya msanii
 
That's very disappointing aisee, yaani dogo kaweka maneno ya kiswahili tu basi, ni wizi kama TID alioufanya kipindi kile, shame on u mwalimu timbulo

Kajiabisha sana,na usikute akiojiwa redion atakwambia yeye ajui ni idea yake tu sema zimefanana lakini 2times?? Kufanana idea nakubali kama vile Fa na jaymo(nataka demu na mimi na mabinti dam dam,melody tofauti na beat tofauti),sasa huyu mwalimu timbulo kila kitu kacopy
 
dah huyu mwalimu mwenzetu kumbe hamna kitu anapiga chabo nyimbo za watu shame

duh jamaa ni mwalimu??hapa sasa napata picha kwa nini taifa linapoteza dira..
Ila ndio tabia za walimu kuvamia fani za watu siunamuona ata Roma anavyopigapiga makelele.
 
kamanda umemuumbua jamaa!! Au wewe producer wake mmedhulumiana mshiko?
 
kamanda umemuumbua jamaa!! Au wewe producer wake mmedhulumiana mshiko?

Hapana mkuu me si producer kabisa na hata sijui kucheza na fruit loop,ila hii issue kuna watu wameibua na mie nikaona nishee na JF
 
Halafu kuna mijinga hapa inayo sisitiza tuwaenzi wasanii uchwara wa bongo.
huyu jamaa afungwe gerezani kwa wizi.
sasa unakuta mwenzie katumia vyombo halisi halafu yeye kaiga kutumia beats zao za kitoto!
 
Taratibu jamani......
Mwancheni dogo naye atusue. Maadamu remix zake zinabamba, sioni shida. Hata MwanaFA walisema anatafsiri nyimbo za Fedrostar, lakini tunaona hadi leo ni mkali. Hata T.I.D kwenye Nyota Yako tunajua ilikuwaje.

Lakini mbona kucopy nyimbo hata mamtoni kupo, tumesahau mkasa wa Haiti, akina Jimmy Fox, Wyclif Jean, Lionel Richie na wenzake akina Celin Deon wameimba wimbo wao. Na ktk kundi kubwa lote ni Lionel Richie pekee aliyekuwa kwenye original version ya wimbo ule.

Mbona tunawabania madogo, au tunataka waingie vichochoroni wakafanye ujasiriamali wa roba za mbao? Let's be serious. Mi dogo namkubali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom