Msanii Snura afungiwa kujihusisha na sanaa, TCRA waagizwa kuifuta video ya Chura mtandaoni

Nawauliza basata kwa sababu watanzania tuna tabia ya kusahau matukio hivi Leo ikatokea kuna kauchaguzi kadogo akachukuliwa Na chama cha kijani watakuwa Na ubavu wa kuzuia aliyecheza uchi wakamdingia lakini walikaa kimya kipindi cha kampeni uchaguzi mkuu hawa ni wa kuwaamini nachukulia kama ni waonevu tu hawana lolote wakojibu hilo nitawaunga mkono kwa hili.
 
c8896296aae4b652386a9ccce109567b.jpg
 
Wamemzuia kujihusisha na sanaa, ina maana hadi kuigiza kazuiwa?!
 
Wamemuonea tu, ye alishaonya kuhusu hiyo video, na alitupa u tube kwa maonyo kuwa asije na umri mkubwa asiifungue na alisema isipigwe katika tv stations na kwani haina maadili. Sasa kosa lake liko wapi?
Kosa ni la kwake kwa kutengeneza video ambayo haina maadili.
 
View attachment 344659
Katikati ni mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiwa na maafisa wengine wakizungumza na waandishi wa habari.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.

Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp.

Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.
Na zile ngoma za ajabu za tanga zifungiwe pia sijui wanasema laki si pesa. Chafu sana hadi inashangaza kuwa watu hawamuogopi Mungu. Hizo serikali haijaziona kweli? Tena hizo ni zaidi ya huyu chura.
 
Nakumbuka kuna mdau huku ndani aliwaambia basata wakae mkao wa kula chura anakuja na snura naona bila iyana wamekula chura wa snura ila sijawai kuona mchaga mswahili kama muro wa yanga na snura wa majanga
 
hii nilikuwa sijaiona kutokana na kuipuzia ila niliposkia kuwa imefungiwa ndio nimechek saiv u tube aisee upuuz mttupu /madudu kama vp tcra muifate hadi kule u tube myipige panga alah! omben hata msaada kutoka kwa watalam wa israel basii
 
Kama kuna watu wazima Tz hii ambao huangalia adult site je kwanini hii chura isipelekwe huko? Tena iwe ya kulipia kama zile zingine ili dada yetu atuingizie dola?
 
Labda niseme kuwa nilikuwa sijawahi kuisikiliza au kuiona video ya mwanadada huyu ya CHURA hadi leo nilipoamua kuitafuta kwenye youtube.

Kiukweli ngoma hii ni ngumu sana kimaadili kama kweli watanzania wanayo hayo maadili !!

Sikatai ngoma hii kupigwa ban lakini bado nina hoja ya msingi inayonifanya nimtetee mwanadada huyu aliyeibuka kivyakevyake.

Kihistoria naona kuna katabia flani cha ukandamizaji wa utamaduni wa wanaoitwa waswahili hasa hasa wale wa pwani ...

Miaka ya zamani wazaramo walijulikana sana kwa ngoma yao ya mdundiko ambayo ilikuwa ikipigwa katika kila harusi...baadaye harusi zikachukua mfumo wa kizungu wa kucheza bluzi na kunyonyana ndimi.ngoma ya mdundiko ikaonekana ya wavivu na masikini.

Baadaye wazaramo wakaja na ngoma ya mchiriku nayo haikufua dafu ikaonekana ni ya wala unga...

Ikafika wakati tukaisikia ngoma ya mnanda ambayo baadaye ikaitwa vigodoro nayo ikapigwa ban.

Sasa kina ikaibuka Singeli ambayo kinamna flani imekuwa modernised lakini vita vinaendelea ...sasa ni ngoma hizi mithili ya chura zinapigwa ban ...ni kweli nyimbo za kizungu tunazoziona kwenye luninga zina maadili zaidi ya hizi za kina snura?

Mbona ni kama wazaramo wanaandamwa?
 
Back
Top Bottom