Msanii huyu anaitia aibu tasnia ya filamu

Siasa Basi

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
1,493
4,276
Ndugu zangu nayasema haya si kwa chuki au unafki , ila wakati mwingine inabidi tuseme kama funzo kwa jamii yetu inayotuzunguka. Na si vyema kujadili maisha ya mtu lakini huyu ninayemjadili ni msanii tena ana jina kubwa tu, hawa ndio tunawaita kioo cha jamii hivyo wanapokwenda tofauti lazima tuseme.

Wapo wengi tu wenye tabia hii ambao huishi maisha yasiyo yao. Kwa sababu tu wanaitwa wasanii na wanajulikana kwenye jamii. Huyu msanii ni wa Bongo movie anaitwa Jumanne Mshindo. Ni msanii wa muda mrefu wengi mmnafaham wale wapenzi wa filamu za bongo. Ukimuona ni mtanashati kweli na Mungu kamjalia umbo lenye Pesa.
1472297737472.jpg

Katika tembea tembea yangu siku ya wikiendi, nikafika sehemu moja inaitwa Chamazi kwa rafiki yangu, kanunua huko kakibanda kake safi anakaa na familia yake. Wakati tunaendelea kupiga stori hapo nje maana nyumba yake haina fensi. Gafla nikamuona jamaa mnene anatokea kwenye nyumba ya pili yake nayo haina fensi ila ni ya zamani. Nikawa kama nimemfananisha, ikabidi niulize mwenyeji wangu, vipi huyo jamaa aliyepita hapo anafanana na msanii mmoja maarufu wa filamu. Jamaa akacheka, kisha akasema ni kweli wala ujamfananisha, Anaitwa Jumanne Mshindo na hapo ni kwao.

Nikamtania kumbe unaishi na wazazi wa msanii mkubwa hapa kwako, kilichonishangaza akaniambia sio naishi na wazazi wake pekee ata mwenyewe anaishi hapo, na nilipoaamia hapa toka mwezi 10 mwaka Jana nilimkuta hapa, anaishi maisha ya shida sana. Na hii Nyumba ninayoishi kaka yake ndiye aliyemuuzia aliyeniuzia Mimi baada ya kuikarabati. Baada ya kaka yake kuuza hii nyumba alivutia unga yote nae anaishi hapo kwao. Na ili eneo lote lenye majengo lilikuwa lao waliuza viwanja vyote wamebaki na nyumba hiyo moja ambayo haina hata nafasi ya watoto kucheza.

Sikuridhiki na maneno ya jamaa ikabidi mwenyewe niende Chamazi kwa wakati wangu kufanya utafiti. Kilichonishangaza zaidi baada ya utafiti kumbe ndiye muuza unga, kwa wale mateja wa Chamazi. Anashinda kwenye jumba bovu hapo jirani na mateja humzunguka kwa ajili ya huduma. Na anaishi hapo kwao kwa kipindi kirefu yeye na mke wake chumba kimoja, vyombo vyote kauza kabakiza kitanda tu. Nikaingia ndani kabisa kuhusu historia ya hapo nyuma ya familia yao. Baba yao alikuwa na uwezo mkubwa tu, baada ya kufariki, wakauza Nyumba pale mtoni, mashamba, viwanja n.k ikabaki Nyumba 1 iliyoko Chamazi ambayo mama yao anaishi sasa. Pesa nyingi wakagawana vijana wakala maisha.

Kilichosababisha niandike haya ni baada ya kubaini mama yao anateseka sana licha ya mtoto wake ana jina kubwa kwenye jamii na kwenye mitandao wanatupia vitu na maisha ya maigizo, ukiingia kwenye ukurasa wake Facebook unakuta kapiga picha suti kali, gari na funguo mkononi . Kumbe maigizo matupu. Walipouza Nyumba na viwanja vya uridhi yeye alikimbia kuwekeza kwenye movie, alinunua gari Kali, alipanga Nyumba nzima na furniture za kila aina, nguo za bei Kali, akawa anakesha bar kwamba aonekane ni staa mwenye Pesa. Bila kukumbuka kujenga, Pesa zilipoisha karudi kwao kumuangaisha mama yao na soko la movie halilipi kabisa. Hapo kwao ni familia kubwa sana, Nyumba ya vyumba 4, yeye anaishi chumba kimoja na mke, kaka yake nae mvuta unga chumba kimoja, kuna mdogo wake wa kike, bado wajukuu wa kike na wakiume na mama yao humohumo. Jamani hata Pesa ya kupanga chumba kimoja inakosekana unabaki kupishana na mama yako kwenye bafu moja? Kweli haya ndio maisha ya mtu mzima.
1472301229669.jpg


Wasanii badilikeni jaribuni kuishi maisha yenu halisi, kama huna sema sina, sio kudanganya watu kwenye mitandao mna maisha bora kumbe hakuna chochote, mnashindia mihogo. Fanyeni kazi zingine kama bongo movie haiwalipi, kuna mashamba kibao mkalime.
 
Umefanya jambo jema kuweka mambo wazi pasipo kumungunya maneno. Watu wengi wanaishi maisha ambayo siyo ya kwao.
Unamkuta mtu anakula bia kwenye club kubwa - nyumbani kaacha dona na dagaa ... hizo ni akili au mattope!??? Rekebika jamani.
 
Umefanya jambo jema kuweka mambo wazi pasipo kumungunya maneno. Watu wengi wanaishi maisha ambayo siyo ya kwao.
Unamkuta mtu anakula bia kwenye club kubwa - nyumbani kaacha dona na dagaa ... hizo ni akili au mattope!??? Rekebika jamani.
Ni kweli mkuu watu wanaigiza sana maisha, kama hawa wasanii wetu wamekuwa ndio wanaongoza.
 
Ni kweli mkuu watu wanaigiza sana maisha, kama hawa wasanii wetu wamekuwa ndio wanaongoza.
Unajua jamii yetu imekuwa na viumbe wa ajabu sana ...
Unakuta mtu anamponda mtu alojitahidi akajenga nyumba ndogo haya ya vyumba viwili na badala yake anamsifia anayepanga nyumba nzima. Kupanga ni shida sana, bora nyumba ndogo ya kwako kuliko nyumba kubwa ya kupanga. Alafu wanaoponda ndo hao wanaishi wa jamaa zao au kwa wazazi wao.
 
Aisee pole yake. huu ujumbe nadhani lazima aupate tuu.

hata mie naishi Chamazi magengeni yeye anaishi Chamazi sehemu gani nikamtembelee msanii wetu
Chamazi kwa mkongo unaingia hiyo barabara inayokwenda Saku Ilulu kama mita chache tu unafika kwao. Au ulizia wale mateja wanaobeba uchafu hapo Chamazi wanamfaham sana maana ndio Wateja wake.
 
Chamazi kwa mkongo unaingia hiyo barabara inayokwenda Saku Ilulu kama mita chache tu unafika kwao. Au ulizia wale mateja wanaobeba uchafu hapo Chamazi wanamfaham sana maana ndio Wateja wake.
si Kabla hujafika kiwanda cha Kova cha matofali? basi ntamuulizia leo nipige nae picha niwatumie au ntamuonesha huu ujumbe hapa ha ha ha.
 
Ndugu yangu umetisha.... Kupoteza muda wako kwenda kuyafanyia 'utafiti' maisha ya huyu jamaa.

Nadhani utakuwa mwandishi wa habari wa haya magazeti pendwa

Hongera
Hahahahaaa ndio kazi zetu hizi mkuu ni kuwafichua tu maana hamna namna, na kama kuna askari wanaopambana na madawa anitafute pm, nimsaidie kazi. Vijana pale Chamazi wanakwisha, kila unayemuona kawa zezeta
 
Back
Top Bottom