Msanii bambo avunjika mguu ajalini, alazwa muhimbili hospital

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,260
Bambo.jpeg Mkali wa maigizo ya kuchekesha Bongo, Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo alfajiri ya leo amepata ajali mbaya ya pikipiki na kuvunjika mguu wake wa kulia sehemu ya paja.
 
Tunampa pole sana BAMBO kwa kupata ajali na kuvunjika mguu na tunamuombea Mungu amponye haraka kiumbe wake
 
Sasa ile sehemu ya Babu kwenye comedy ya East Africa tutaikosa jamani. Bambo pole sana urudi bwana kuja kutuondolea huzuni kwani unatuchekesha sana wewe na Kiwewe na Massawe Mtata. Hizi pikipiki ni mbaya jamani kumbe hata wewe unadhubutu kupanda wakati hata Ulaya zinaogopeka.
 
Hizi piki piki jamani kuweni makini nazo hazifai kabisa na ni makaburi yanayotembea..pole Bambo upone haraka mkuu
 
IMG_2396.jpg IMG_2392.jpg

Ajali hiyo imetokea eneo la njia panda Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo gari aina ya DCM iliigonga pikipiki aliyokodi Bambo wakati akirudi nyumbani kweke. Dereva wa pikipiki aitwae Jumbe Juma kwa sasa hali yake ni mbaya na wote wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
 
Jamani mzee wa magumashi pole sana, Mungu atakuafu mapema tu usijali. Hata hivyo kama wewe upendi kuendesha gari uwe unamwita mdogo wako si yeye ni dreva wa mataxi na madala dala? awe anakuchukua safari zako tafadhari.
Pole sana.
 
Jamani mzee wa magumashi pole sana, Mungu atakuafu mapema tu usijali. Hata hivyo kama wewe upendi kuendesha gari uwe unamwita mdogo wako si yeye ni dreva wa mataxi na madala dala? awe anakuchukua safari zako tafadhari.
Pole sana.

Tumwombe Mungu atuepushe na ajali
 
Bambo pole sana. Mungu akuponye haraka.

Jamani hizi toyo ni makaburi yanayotembea muwe makini jamani!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom