Msanii anayeshika uhusika wake ipasavyo afariki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WASANII wa kikundi cha Jakaya Theater wamekumbwa na simanzi baada ya mkurugenzi wao kufariki dunia kwa kuangukiwa na kontena maeneo ya Kimara Resort jijini Dar es Salaam
Msanii huyo aliyefariki dunia ni Thomas Senzige [29] ambaye alikuwa muongozaji wa kikundi kinachorushwa mchezo unaoendelea sasa katika kituo cha televishen cha ITV

Senzige alipata ajali Jumamosi ya Mei 14 mwaka huu, majira ya jioni, katika eneo la Kimara Resort

Alipata ajali hiyo wakati alipokuwa akitokea kwenye kikao chake cha harusi na kuelekea kusherehesha sherehe katika ukumbi wa Resort na alikodisha pikipiki hilo akitokea maeneo ya Manzese na alikodisha pikipiki na alipofika eneo hilo waliangukiwa na kufunikwa na kontena lililokuwa na namba T 840 na kufariki dunia papohapo

Katika ajali hiyo pia dereva aliyekuwa akiendesha pikipiki aliyokodiwa Renatus aponali [25] alifariki dunia
 
may the R.I.P
Inasikitisha sana maana makontena na uzito wake lazima hata watu walishindwa kuwaokoa.

Sad
 
Maskini....Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi!!Pole nyingi kwa wafiwa!
 
Poleni wanaJakaya Theater! Bila shaka mwenye jina atatoa ubani kwa familia
 
mungu ametowa pia ametwaa jina la bwana liabudiwe,
poleni wafiwa wote,wasanii na wan Jf kwa ujumla
 
IGP inabidi atueleze kwa nini makontena mengi hayafungwi kamba - yawe tupu au yamejazwa mizigo?
 
Back
Top Bottom