Msanii afunguka...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Ni Mlasi Feruzi, mwanamuziki aliyekuwa akifanyia kazi na kundi la Jambo Survivors, mwimbaji wa kibao maarufu cha 'Maprosoo'. Anahojiwa na Masoud Masoud katika kipindi cha muziki wa kitambo hapa TBC Taifa, anadai kuwa alirogwa, na alikwenda kwa mganga wa kienyeji kutibiwa huko Ufipani, na baada ya kutibiwa kienyeji mganga akamwambia aende hospitali ya kawaida, akafanyiwa upasuaji na kutolewa khanga nzima ikiwa imekunjwa.
Kwa mara ya kwanza celeb anafunguka waziwazi kuhusu ushirikina.
 
hahahhhahahahahahahahahahahhh hii kali,ningekuwa mie nisingesema nilienda kwa mganga wa kienyeji
 
Natamani ningeisindikiza hii alert yako kwa ngoma ya Jay-Moe ya Twende kwa Mganga ila ndio hivyo wasanii wetu hata kuweka kazi zao mtandaoni kazi... lol
 
Nimemsikia sana ,anatia hurma ,Kwa sasa yuko Z;bar na bendi ya polisi kajishikiza kwa muda! Wabongo kwa ulozi bana! tena walimzushia kifo kabisaa! Mlasi Feruzi Hanzuruni!
 
hahahhhahahahahahahahahahahhh hii kali,ningekuwa mie nisingesema nilienda kwa mganga wa kienyeji

Kwanini? Mimi huwa ni muwazi sana kwenye haya mambo, matembelea sana mitaa ya kwa waganga, kitiba zaidi.
 
Natamani ningeisindikiza hii alert yako kwa ngoma ya Jay-Moe ya Twende kwa Mganga ila ndio hivyo wasanii wetu hata kuweka kazi zao mtandaoni kazi... lol

Sijawahi kuipata hiyo, nitaitafuta.
 
Nimemsikia sana ,anatia hurma ,Kwa sasa yuko Z;bar na bendi ya polisi kajishikiza kwa muda! Wabongo kwa ulozi bana! tena walimzushia kifo kabisaa! Mlasi Feruzi Hanzuruni!

Mdada kama sauti tu anayo aisee, sijui kwanini huyo mkemwenzake aliamua kumtenda vivyo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom