~^^*^^~ msaliti ~^^*^^~

Hiki ni kielelezo ch ukiukwaji wa maadili katika jamii zetu. Mara nyingi tunasikia mahusiano baina ya watu na shemeji zao ..lakini hii ya mama mkwe nimebaki na mshangao ambayo hakupaswa kamwe kuyajua!

Huyu bwanakaka naye anastahili kulaaniwa kwa kiwango kilekile! Je huku si ni sawa na kulala na mama yake aliyemzaa? Sitaki kuamini kwamba hili linawezekana katika maisha ya kweli...ni porojo tu za Mwanakijiji za wikiendi.

MKJJ ..siku hizi umecharuka na visa vyenye viroja... siasa zimekushinda?
 
WoS.. unafikiri kipi ni chepesi? mtu kulala na binti yake au dada kulala na kaka yake au mtu kula na mkwe wake?
 
duh.. yaani kutoka kwenye hadithi umepostulate kwa jamii nzima ya watu with no qualification whatsoever? yawezekana msingi wa mahitimisho yako hautokani hata chembe na kisa cha masimulizi.

MMKJ,

Asante kwa hadithi. Nina swali moja dogo. Msimulizi anasema alichomwa kisu cha moyo na kikashindiliwa kabisa. Je alipona? Kama hakupona imekuwaje atoke kuzimu kuja kusimulia hilo tukio hapa tena?

Tiba
 
Mwanakijiji nadhani kutokana na mikasa yako ya kunako hadithi ulistahili kuitwa BAZAZI. Unanilazimisha kila wakati kuwa nafuatilia hadithi zako. Keep it up please
 
ushauri kwa mwanakijiji. mimi binafsi ningependa kuona upande wako wa pili wa kiutunzi zaidi ya mapenzi. mapenzi ni marahisi kuyatungia simulizi ndio maana asilimia 90 ya nyimbo ni mapanzi tu. kuna maisha zaidi ya mapenzi. andika simulizi hizo na nadhani itabandikwa kwenye jukwaa la lugha
 
Guys, you should remember that our brother Mwanakijiji is a Philosopher you should therefore abstain from stopping challenging your brains. I do not think Mwanakijiji wants to tell us about some imaginary mother in laws who sleep with their daughters husbands. May we try to give this story a real life interpretation? is this story related to the political situation in our country?
 
MSALITI

Na. M. M. Mwanakijiji


Nilihisi kuna mtu amesimama karibu na kochi nililokuwa nimejilaza. Ni ile hisia ambapo bila kuangalia nyuma unahisi kuna mtu anakunyemelea au kuna mtu anakuangalia na unapogeuka unakuta ni kweli. Nilikuwa nimejilaza chali kwenye kochi kubwa la rangi nyeusi huku Radhiya akiwa bado amekaa juu yangu. Shanga zake zikiwa zinaning’inia na kugusa kiuno changu. Kiunoni mwake alikuwa amejifunga kanga tu, tulikuwa tumeloa jasho, miili imechoka huku usingizi ukitupitia taratibu. Ilikuwa ni mara ya pili ndani ya saa moja tulifanya mapenzi ya nguvu.

Hisia hiyo ya mtu kuwa karibu ilinishtua mimi na kabla sijafanya lolote Radhiya naye alishtuka pia. Tulipofumbua macho yetu tulipigwa na butwaa la mwaka. Mke wangu Husna, alikuwa amesimama pembeni ya kochi tulilokuwa tumejilaza. Mkononi alikuwa ameshika kisu kikubwa chenye ncha kali kilichokuwa kinameremeta. Alikuwa amekunja uso wake, huku machozi yakimtoka na midomo ikimtetemeka. Kabla sijapata nafasi ya kusema Radhiya alijiondoa kwa nguvu na kuruka pembeni huku akishikilia kanga iliyokuwa ikimning’inia. Hakufanya ajizi alinyakuwa mkoba wake uliokuwa mezani na funguo za gari lake na kukimbilia mlangoni huku akijaribu kujisitiri na kanga yake. Alitoweka.

Nilijaribu kuinuka haraka kumuwahi Husna kabla hajafanya uamuzi atakaojutia milele, lakini sikuwa na bahati hiyo. Husna alikiteremsha kisu chake kwa nguvu zake zote za kikike, kama vile mkulima anavyoshusha jembe kwenye ardhi ngumu. Ncha ya kisu ilipenya upande wangu wa kushoto wa kifua changu. Kama vili pini inavyopenya kwenye karatasi, ncha ya kisu ilikita ndani ya moyo wangu. Nilijaribu kupiga kelele, hata hivyo nilichoweza kusema ni “Ahhhh”. Maumivu makali yaliingia katika kila kona ya mwili yangu. Nilijaribu kuuzuia mkono wake asikandamize hicho kisu. Sikufanikiwa kwa hilo pia. Husna alikuwa amepania. Alikichomeka kisu kwa nguvu zaidi huku akikitingisha juu na chini.

Damu ilianza kunivuja kwa wingi, mwili wangu uliokuwa umeloa jasho sasa ulikuwa kama ardhi iliyokuwa tepe kwa mvua. Damu ilisambaa kifuani na ilitiririka kwenye kochi na sakafuni. Kiza kilianza kuniingia. Nilijaribu kujitahidi kufumbua macho kumwomba Husna msamaha, sikuweza. Husna alibakia akiniangalia jinsi uhai ulivyokuwa ukinitoka taratibu. Nilijuta kumsaliti mke wangu, nilijuta kuwasaliti watoto wangu, nilijuta kuisaliti dini yangu na ndoa yangu. Sikuweza kuomba msamaha kwa mke wangu wa miaka minne. Nilitamani muda urudi nyuma na malaika ashuke kuniokoa. Swala zangu hazikujibiwa. Mauti yalinifika taratibu.

Kwa mbali nilisikia sauti za watu zikisogea karibu na nyumba yangu iliyoko eneo la Isamilo Mwanza karibu na Maghorofa ya NBC. Neno la mwisho nililolisikia ilikuwa ni sauti ya Husna:

“Utangulie kuzimu!”



* * *​

Husna alifikishwa kwenye kituo cha Polisi cha Kati kilichoko kando ya Ziwa Victoria karibu na jengo la makao makuu ya CCM Mwanza. Aliingizwa katika chumba cha kutolea ushahidi ili aandike maelezo yake kabla ya kupelekwa rumande ambapo atasubiri kufikishwa mahakamani. Maelezo ya Husna yalikuwa yakichukuliwa na mpelelezi Richard Fundi, mmoja wa wapepelezi vijana wa Idara ya Upepelezi ya mkoa wa Mwanza. Richie (kama alivyojulikana mtaani) alikuwa ni mpepelezi aliyehitimu mafunzo yake huko Uingereza kwenye chuo cha New Scotland Yard.

“Jina lako tafadhali” Aliuliza Mpel. Richie
“Naitwa Husna Mohammed Ali” Alijibu Husna huku akimtaza mpelelezi huyo aliyekuwa akiandika majibu yake hayo. Pembeni kulikuwa na kaseti rekoda, iliyokuwa ikirekodi mahojiano hayo.
“Tafadhali tueleze ilikuwaje uamue kumuua mumeo Bw. Mohammed Ali” Aliuliza mpelelezi huyo.

Husna alianza kusimulia kisa kizima cha mkasa huo.


* * *​

Nilipigiwa simu na rafiki yangu ambaye alinidokeza kuwa anafahamu kuwa mume wangu alikuwa na mwanamke mwingine aliyekuwa akimleta nyumbani kila mara nyingi ninapokuwa kazini hasa wakati wa mapumziko ya mchana. Mara kadha wa kadha nilijaribu kukanusha madai hayo kwani nilijua mume wangu asingefanya vitendo kama hivyo na alinipenda kwa dhati. Kila kitu nilichotaka alinipa na mimi nilijitahidi kwa kila hali kuwa mke mwema na mama mzuri kwa watoto wangu.

Nilikuwa ni mzuri wa kuzaliwa kwa tabia na kwa umbo. Niliurithi uzuri huo toka kwa mama yangu. Nilikuwa ni mahiri kitandani na sikumnyima mume wangu mahaba ya kweli na nilikuwa na uhakika kuwa na yeye alikuwa haninyimi kitu. Alinipa nami nikampa. Tulijaliwa watoto wawili Husein na Rehema. Tulijaliwa nyumba nzuri na miradi kadha wa kadha ambayo mimi niliisimamia. Hakuna kitu nilichotaka ambacho hakunipa. Hivyo tetesi za kuwa mume wangu kuwa hakuwa mwaminifu nilizitupilia kando. Niliita ni wivu wa jirani.

Hata hivyo miezi michache iliyopita, mume wangu amepunguza hamu yake kwangu. Nimejaribu kuweka kila aina ya vikolombwezo ili kutia sukari zaidi katika penzi letu na ndoa yetu bila mafanikio. Nimejaribu kumpa penzi la kushitua, kama akiwa hana hili wala lile nilijaribu kumpa vitu. Zamani alikuwa hapotezi muda alikuwa akinirukia utadhani jogoo liliachiliwa bandani. Hii miezi michache hata hivyo ameanza kunisukuma kando. Zimeanza kupita wiki bila ya mimi kupata “mkuno wa nguvu” wa kuniridhisha roho yangu. Hii ikaanza kunitia wasiwasi, kwani nakumbuka ndoa nyingi huanza kuvunjikia chumbani. Niliamua kufanya uchunguzi wa kina nijue ukweli wa mambo.

Siku ya tukio, nilimwambie mume wangu kuwa nitaenda huko Kijerezi kumtembelea rafiki yangu na sitarudi hadi jioni. Niliondoka nikiwa nimefungasha vitu vichache kabla yeye hajaondoka kwenda kazini. Sikwenda mbali. Nilijificha nyumbani kwa jirani yangu (aliyekuwa akinipigia simu kunitahadharisha) hadi nilipomuona mume wangu ameondoka kwenda kazini. Nilirudi nyumbani na kujifungia kwenye kabati lililokuwa sebuleni kusubiri ni nini kitachotokea. Kwa vile nilikuwa nimechoka kwa kupanga mipango hiyo, nilipitiwa na usingizi nikiwa nasubiri humo kabatini.

Sikusikia ni wakati gani waliingia ndani au mambo waliyoyasema na kuyafanya kabla ya mimi kushtuka. Kilichoniamsha katika usingizi wangu humo kabatini ni sauti ya malalamiko ya kimapenzi. Nilifungua mlango wa kabati hilo ili kupata upenyo wa kuweza kuona kilichokuwa kikiendelea. Niliweza kumuona mume wangu akiwa amelala chali, mikono yake ikiwe imezunguka ****** ya mwanamama mmoja ambaye alikuwa amemkalia juu. Huyo mwanamama alikuwa amevalia chachandu za rangi mbalimbali. Niliweza kuona kwa uzuri kabisa mgongo wa mama yule na eneo zima la ajali. Niliweza kumuona jinsi alivyokuwa akimkatikia mume wangu na kumwendesha kama farasi! Masikini mume wangu. Uume wake ulikuwa ukiingia na kutoka ukiwa umeloa na unang’ara kama sime iliyopakwa mafuta! kwa nguvu, huku jasho likiwatoka. Nguo zao zilikuwa pembeni sakafuni. Kulikuwa na kanga kwenye ukingo wa kochi. Ilikuwa ni kanga yangu yenye maandiko “wazuri na wabaya ni walewale”.

Waliendelea kufanya mapenzi, miye nikiwa nimeshikwa na butwaa na sikujua nifanya nini. Kifundo cha uchungu kilinishika. Walipeana Walipofika kilele yule mwanamke alimuangukia mpenzi mume wangu kifuani. Aliivuta ile kanga na kujifunika kiunoni. Mume wangu aliileta mikono yake kumkumbatia huku akiwa bado ndani yake bila shaka akifurahia masalio ya mlipuko wa volkano. Machozi yalianza kunitoka, nilitamani niruke toka nilikojificha na niwasute hadharani. Nilitamani ulimwengu mzima uje kushuhudia jinsi yule niliyempenda alivyonisaliti. Nikiwa nawaza hayo niligundua kuwa mume wangu ameanza kusinzia (ulikuwa ni udhaifu wake mkubwa akishafanya mapenzi). Na yule mwanamama naye alianza kukoroma kwenye kifua cha mume wangu.

Nilihakikisha kuwa wamesinzia nilipotoka kwa kunyata na kuelekea jikoni. Nilitamani nichemshe mafuta ya moto niwamwagie. Baada ya kufikiri sana niliamua kuwa anayestahili kuadhibiwa ni mume wangu na siyo yule mwanamke. Huyo mwanamke sikuwa namjua na yeye hakunijua. Niliamua kuchukua kisu cha kukatia nyama na kuamua kulipiza kisasi. Moyo ulinidunda kwa kasi, machozi yalinitiririka upande mmoja, na viganja vyangu vilikuwa vimelowa jasho. Mikono na midomo ilinitetema. Niliapa kwa mizimu ya mababu zangu wa kichaga, nitampa somo la milele. Nilinyemelea taratibu hadi niliposimama karibu ya wapenzi hao wawili. Nilikusudia kuikata shingo ya mume wangu mbele ya mwanamke huyo. Sikutaka kumgusa mwanamke huyo. Niliinua kisu, nikavuta pumzi, na nilikuwa tayari kukiteremsha. Mume wangu alifumbua macho. Kabla sijakiteremsha kisu, yule mwanamke naye alizinduka, akaniangalia usoni. Sikuamini macho yangu! Kabla sijasema chochote na kabla yeye hajasema chochote alikurupuka, akachukua hiyo kanga tu, na mkoba wake akakimbilia nje.

Mume wangu alitaka kukimbia, sikumpa nafasi. Nilikiteremsha kisu haraka kwenye kifua chake na nilikishindilia kuhakikisha kuwa hataamka milele. Nilisimama karibu kuhakikisha kuwa amekufa. Nilimtakia heri ya kuzimu. Nilikuwa hapo hadi polisi walipotokea.


* * *​

“Asante kwa maelezo yako” Mpel. Richie alisema baada ya kuhitimisha kile alichokuwa akiandika.
“Hata hivyo nina swali moja” Alisema kabla ya kuizima ile rekoda.
“Uliza” Husna alijibu.
“Kwanini hukuamini macho yako ulipomuangalia yule mwanamama? Unamjua?” Richie aliuliza akimbulia macho Husna, binti wa miaka ishirini na miwili ambaye licha ya mambo yote yaliyokuwa yakiendelea uzuri wake haukufichika.

Husna alivuta pumzi ndefu, aliifikicha mikono yake, na alimwangalia mpelelezi huyo kwa muda. Hatimaye alisema,

“Ndiyo namjua; huyo mwanamke alikuwa ni mama yangu mzazi!”

Chumba kizima kiligubikwa na ukimya uliokatishwa na kanda ya kurekodia ilipofika mwisho na kujizima. Hawajawahi kusikia kisa cha usaliti wa namna hiyo.


MWISHO
[/QUOTE

Kwa kweli hiyo story ni nzuri na ni fundisho sana kwa wale wanaopenda wakwe zao. Naamini Husna alipata pigo kubwa sana baada ya kuona mama yake anatembea na mume wake.......

WITO WANGU KWA WANANDOA WOTE... TUWE WAAMINIFU KATIKA NDOA ZETU. TURIDHIKE NA WAKE/WAUME ZETU
 
duh.. yaani kutoka kwenye hadithi umepostulate kwa jamii nzima ya watu with no qualification whatsoever? yawezekana msingi wa mahitimisho yako hautokani hata chembe na kisa cha masimulizi.

Mkuu MKJJ, nilichokifanya ni kuchambua hadithi zote na kutoka na dhamira mojawapo ya mwandishi kwa mujibu wangu. Sijawahukumu kabila kwa ujumla wao bali nilionesha kama ambavyo mwandishi alitaka tuone. Lakini all in all, kwa kuwa kazi ya sanaa ni kuonesha kilichomo kwenye jamii husika, I think I was right.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom