Msajlii wa vyama adhibiti hawa wanaorudisha kadi za CCM

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Hivi kwa nini huwa wanazipeleka kwa viongozi wa CHADEMA wakati sio waliowapa, toa maelekezo hizi kadi ziwe zinarudishwa ofisi za CCM.

Na aliyeanzisha huu mchezo ni nani?
 
inafaa uwe mwimbaji wa taarabu!maana huo ni mpasho sio siasa!inakuuma nini watanzania kujitambua kwa sasa
 
Bongolala na Losambo naamini hamjaelewa alichomaanisha mtoa mada!

This is JF! Si kila kiandikwacho ndivyo kilivyo.......
 
Hivi kwa nini huwa wanazipeleka kwa viongozi wa CHADEMA wakati sio waliowapa, toa maelekezo hizi kadi ziwe zinarudishwa ofisi za CCM.

Na aliyeanzisha huu mchezo ni nani?

Huu ni utaratibu ulioanzishwa na CCM wenyewe walipokuwa wanawashawishi wanachama wa vyama vingine enzi zile za ujinga kurudi CCM, walikuwa wanatumia mtindo wa kuonyesha kadi zilizorudishwa kwao kama njia ya kudhoofisha vyama vya upinzani. Sasa kibao kimegeuka wembe huo huo unawanyoa wao.
Kwa hali ya siasa za Tanzania siyo rahisi kwenda kwenye chama unachotaka kuhama na kurudisha kadi yao kufanya hivyo ni kutafuta matatizo. Lakini huu ndiyo utaratibu katika mabadiriko. Mchawi akiokoka hawezi kupeleka tunguli zake kwa wachawi wenzie bali anazisalimisha kwa mchungaji aliyejaa Roho Mtakatifu akazichome.
 
Standards za Vitambulisho vingi ni kwamba, kwa nyuma huwa kinaandikwa ukikipata kimepotea ukirudishe kwa issuing authority, CHADEMA huwa wanazirudisha hizi card ofisi za CCM?
 
Standards za Vitambulisho vingi ni kwamba, kwa nyuma huwa kinaandikwa ukikipata kimepotea ukirudishe kwa issuing authority, CHADEMA huwa wanazirudisha hizi card ofisi za CCM?

ile ni card ya ccm sio identity ya ccm.
wewe kweli una akili za kiccm, wapi kwenye ile kadi ya ccm pameandikwa ni kitambulisho na kikipotea kirudishwe kwa ccm? kile ukikiokota kichome moto.
sasa hivi ile siyo kadi ya ccm bali ni kadi ya umasikini wa mtanzania.
 
hahaaaaaaa... Wakati just kidding anakusanya za wapinzani ulichekelea eh?

Mbowe atazipelekakwa jk 2015
 
Hivi kwa nini huwa wanazipeleka kwa viongozi wa CHADEMA wakati sio waliowapa, toa maelekezo hizi kadi ziwe zinarudishwa ofisi za CCM.

Na aliyeanzisha huu mchezo ni nani?
Alianzisha mchezo huo ni ccm hivyo acha tu uendelee mimi sioni ubaya wake hata kidogo.hiyo ndio inaitwa kunya anye kuku akinya bata ataambiwa kahalisha.kumbuka kuwa kuwa wote wamejisaidiatofauti ni aina ya kinyesi walichotoa.
 
kutokana na wanajf kuwa na tabia ya kuelimishana,kuepuka kufanya makosa yaleyale kila mara!
Hapo kwenye msajiri palikuwa pasomeke MSAJILI.
 
Nadhani ni promotion na "photo opp." hasa kwa wale wanaovuna wanachama toka chama kingine. Sioni haja kwa msajili kuingilia suala hili kwani ana mambo makubwa ya msingi ya kushughulika.
 
[Standards za Vitambulisho vingi ni kwamba, kwa nyuma huwa kinaandikwa ukikipata kimepotea ukirudishe kwa issuing authority, CHADEMA huwa wanazirudisha hizi card ofisi za CCM?]

Nazani ccm wafike ofisi za CDM kuzichukua mana ni nyingi kweli
 
Aliyeanzisha mchezo huu ni ccm na utaendelea hivyo hivyo na ni vizuri uwepo.jino kwa jino kama linakuuma mzee vua gamba uvae gwanda ndo utaiona raha yake.enzi zile mzee wa kiraracha anazikusanya hukuona ubaya au ulikuwa na makengeza????tulia hivyo hivyo kama unanyolewa.
 
Alianzisha mchezo huo ni ccm hivyo acha tu uendelee mimi sioni ubaya wake hata kidogo.hiyo ndio inaitwa kunya anye kuku akinya bata ataambiwa kahalisha.kumbuka kuwa kuwa wote wamejisaidiatofauti ni aina ya kinyesi walichotoa.

Kadi zenyewe siku hizi zinagawiwa kama njugu wakati wa kura za maoni za CCM. hadhi yake imepungua, ndio maana hata wao hawajali.
 
Standards za Vitambulisho vingi ni kwamba, kwa nyuma huwCCa kinaandikwa ukikipata kimepotea ukirudishe kwa issuing authority, CHADEMA huwa wanazirudisha hizi card ofisi za CCM?

Unaweza kuwaambia CCM wazirudishe za NCCR, TLP, CUF na CHADEMA WALIZOZIPOKEA. Muulize Makamba keshazipokea ngapi
 
LAKINI heshima ni jambo la Bure sana Sangarara , Tafadhali kwa heshima Ng'oa Avatar uliyoweka. Si vema kutumia Picha halisi ya Mtu kama Avatar yako na kuwakilisha mawazo hasi kinyume mtazamo wa itikadi ya kisiasa ya picha ya mlengwa. Humtendei uzalendo. please badilisha Avatar yako.. amavipi tuwasilishe faili kwa Moderators uone kama hawata piga mtu BAN!! Ulalamike nimechongewa na SALMA2015.., au jikumbushe JF Rules..acha ubishi we mkaka..

Nimewakilisha
 
Katika hili nawasilisha mawazo/maoni yake, Yeye Mwenyewe wakati wakampeni za Uchaguzi 2010 aliambiwa na Makamba awarudishie kadi yao, akasema harudishi sababu ni mali yake aliinunua kwa pesa zake mwenyewe.
 
utaratibu ni kwamba ukishachukua uanachama chama kingine, huitaji kuaga chama chako cha zamani, ila katika katiba ya ccm hawaja state urudishwaji wa hizo kadi, walitakiwa waseme kama wanazihitaji kama ilivyo kwa waajiri wetu kitambulisho ni mali ya kampuni!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom