Tuhuma za Ufisadi alizoibua Nape: Mwita Waitara ajiengua UVCCM, adai amedhalilishwa

Waitara bwana kaa macho CCM wako tayari kubakia hata 2 Nchi Nzima ili mradi wawe na mapesa an madaraka .Musoma huwa inamashujaa miaka yote na hasa Tarime na Wazanaki.Ukiondoa wapuuzi wachache kama Wasira na Msekwa anayetoka Mwanza.Waitara umeanza kurudisha heshima ya Mkurya na uendelee kutetea yale wangwe amekuwa akiyaamini .

Nina funga novena kukuombea maisha marefu na ujasiri zaidi .



Teh teh teh,mkuu hayo uliyonena hapo chini ni kweli mkuu?
 
Habari wana Jamii.

nakaribia katika jamvi baada ya kua msomaji kwa muda mrefu nimeona nami nipate fursa ya kua mchangiaji.

Mwita kwa alichofanya si jambo la ajabu kwani wanomfahamu ajali alopata mwaka jana ya pikipiki mpaka akalazwa muhimbili kwa miezi mitatu wanaweza kuelewa kua ajali ile ilimsababishia tatizo la akili so anayoya sema na kutenda naamini ni matokeo ya kuchanganyikiwa kwakwe baada ya ajali ile.



Hivi hebu tuambie kwanza,wewe ni yule Bashe,mgombea uenyekiti wa vijana yaani Hussein Bashe?

Sasa umeona uje kupotosha hapa kwa sababu unaona Nape anaungwa mkono na Mwita? Nape ni tishio kwako kiasi gani hadi uje kupotosha hapa?

Well,mkuu hili jamvi lina watu wenye itikadi mbali mbali,sasa ukija hapa njoo kwa nidhamu.upotoshaji ni dhambi kubwa hapa jamvini,sasa hebu wewe tuambie lenye akili kama unaona Mwita kusema hayo aliyosema ni matokeo ya kuchanganyikiwa.

kama utakimbia hoja hapa jamvini basi wewe ni kiongozi ambae ni weak,hautaufaa umoja wa vijana kwa lolote because tayari tuna Rais dhaifu na hatutaki kuongeza type za akina Jk au Nchimbi types.
 
Dk. Nchimbi ageuka mbogo kujibu shutuma dhidi yake

2008-10-05 14:30:33
Na Simon Mhina

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Dk. Emmanuel Nchimbi, jana aligeuka Mbogo baada ya kuulizwa juu ya shutuma zilizotolewa dhidi yake na Katibu wa umoja huo mkoani Tanga, Mwita Mwaikabe Waitara.

Katibu huyo alikaririwa na vyombo vya habari akilalamika kwamba Dk. Nchimbi, anafanya mikakati na hila za kila aina kuwakwamisha vijana wenye msimamo kama wa Nape Nnauye, katika kuwafichua mafisadi.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam, Nchimbi, alisema habari hizo zimemkera na kumnyima raha.

Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake, alisema yeye hahusiki na shughuli za utawala na utendaji wa kila siku katika UVCCM, hivyo kumuuliza maswali ni kuzidi kumnyima raha na kutomtendea haki.

Alipoulizwa ni vipi anakataa kuzungumzia mambo ya UVCCM wakati yeye ndiye bosi wa umoja huo na Waitara alimtaja waziwazi, Nchimbi alijibu ``Lakini wewe Mwandishi kwa nini unataka kunilazimisha niseme mambo nisiyotaka kusema? Kukaa kimya ni haki yangu naomba usiendelee kuninyima raha.``

Nchimbi alisema yeye akiwa mwenyekiti hashughuliki na mambo `madogo madogo` kama hayo bali anazo shughuli nyingi za kufanya.

``Simjibu Waitara japokuwa mnanitaka ni jibu simjibu, nimekataa sina muda mchafu,`` alisema Nchimbi.

Alipoulizwa madai kwamba alitumia ukabila kumpa nafasi ndugu yake aitwaye Sixtus Mapunda, Nchimbi alisema madai hayo ni ujinga, kisha akakata simu.

Baadaye Nchimbi alituma namba za simu za Katibu wake na kumtaka mwandishi wa habari hizi awasiliana naye kuhusu suala la Waitara.

Katibu huyo Francis Issac, alimbeza Waitara huku akisisitiza kwamba si mwanasiasa bali ni mtumishi tu.

``Waitara si mwanasiasa yule ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine sehemu yoyote nimeshangazwa na majigambo yake,`` alisema.

Issac, alisema kama kweli Waitara anataka kibarua chake kiote majani, basi anapaswa kuandika barua rasmi.

``Maneno yale kayasemea nje ya kituo chake cha kazi, yule ni mtumishi tu tuliyemwajiri, sasa kama hataki kazi aandike barua sio kuzungumza kwenye magazeti.

Anazungumza na Magazeti kwani ndiyo yalimuandikia barua ya kumwajiri?� Alihoji na kuongeza ``Yule ni mtumishi anapaswa kujua hilo na sisi ndio waajiri wake.``

Katibu huyo alisema anasubiri kwa hamu barua ya Waitara hivyo aiwasilishe kwake haraka iwezekanavyo.

Kuhusu madai ya upendeleo, Issac alisema si kweli kwamba Mapunda ni ndugu wa Nchimbi.

``Yaani kwa vile wote ni Wangoni, basi ni ndugu? Wewe kama ni Mnyaturu basi Wanyaturu wote wanakuwa ni ndugu zako?`` Alihoji.

Alipoulizwa ikiwa Waitara si mwanasiasa, kwanini aliitwa kwenye kampeni za CCM mjini Tarime, Issac alisema alishiriki kwa vile wanachama wote wanaruhusiwa kukipigia debe chama chao.

SOURCE: Nipashe
 
kama mwita si mwnasiasa, basi mwanasiasa ni yupi? this is new definition of politician, pengine wanasiasa ni mafisadi wote akiwamo nchimbi, lakini yeyote anayewapinga si mwanasiasa ni mtumishi, kuanzia nape, warioba na sasa mwita
 
Huyo Mwita kashasema hataki huo uhamisho. Sasa kwa kuwa ni mtumishi wao na amekataa maagizo yao, wamchukulie basi hatua, mbona wao pia wanalumba kwenye magazeti? Akiamua kutoandika hiyo barua anayodai Mtinga watafanyaje, wataendelea tu kupiga domo kwenye magazeti?

Tukirudi kwenye uungwana na kujitunzia heshima, nadhani ni vema kwa Mwita kuweka vizuri rekodi yake na hao 'waajiri' wake, kama kweli hataki hiyo kazi mbona ni rahisi tu, awaandikie notisi ya mwezi mmoja kuacha kazi, au 24 hours na kusarenda mshahara wa mwezi huo, ndivyo sheria zinavyosema. Kama anataka ku-contest hiyo treatment aliyofanyiwa na bosi wake, afuate tu sheria kama kawaida (hivi hawa 'watumishi' wa wanasiasa wanayo trade union? sisi walimu ya kwetu ni CWT, hawa wenzetu je?). Haya nayasema kumsaidia huyu kijana maana asipochukua hatua, wao wataendelea kumdhalilisha kama wanavyofanya sasa kwenye magazeti, tusije kushangaa tukisikia 'ametimuliwa kwa aibu' kama Lyatonga Mrema kipindi kile.
 
Hivi hebu tuambie kwanza,wewe ni yule Bashe,mgombea uenyekiti wa vijana yaani Hussein Bashe?

Sasa umeona uje kupotosha hapa kwa sababu unaona Nape anaungwa mkono na Mwita? Nape ni tishio kwako kiasi gani hadi uje kupotosha hapa?

Well,mkuu hili jamvi lina watu wenye itikadi mbali mbali,sasa ukija hapa njoo kwa nidhamu.upotoshaji ni dhambi kubwa hapa jamvini,sasa hebu wewe tuambie lenye akili kama unaona Mwita kusema hayo aliyosema ni matokeo ya kuchanganyikiwa.

kama utakimbia hoja hapa jamvini basi wewe ni kiongozi ambae ni weak,hautaufaa umoja wa vijana kwa lolote because tayari tuna Rais dhaifu na hatutaki kuongeza type za akina Jk au Nchimbi types.
Mkuu mimi si Bashe wa CCM bali huenda ni jina Tu kwani majina kufanana ni kitu cha kawaida.

Pili hakuna upotoshaji bali inawezekana hukupenda kusikia na kuona juu ya mtazamo wangu kuhusu Mwita.

Kuhusu hoja kua Nchimi ni kiongozi Dhaifu sijajua umetumia vigezo gani kumpina na wat was ur Benchmark.

Hoja kua kikwete ni Dhaifu si material ktk hili.

About Mwita kumuunga mkono Nape si la msingi hapa kwani hapa hatujadili nani ana muunga mkono nani.
 
Si mambo yote abayoongea mtu ni kweli anamaanisha anachosema.Binadamu pia huwa anaghafilika na kuongea au kufanya asilolitegemea.sasa kama anakuwa anaghafilika mfululizo bila kuwa na stop hapo ndipo tunasema kuwa amedhamiria anachofanya,uongozi ni utumishi na upendo wa hali ya juu,lazima kila mtu anaetaka kuwa kiongozi ajiandae kuwapenda watu wake na kuwatumikia pia.hivyo hakuna haja ya kumshusha mtu au kumkweza kwa kila jambo.
 
Hivi jeuri hii huyu dogo Nuchimbi anaitoa wapi?mara nyingi naona majibu yake ya dharau na kebehi.
 
Tatizo CCM wanashindwa kuangalia alama za nyakati kama zile za Tarime. Watu wamechoka na wamechoshwa!
 
Back
Top Bottom