Msaidieni rafiki yangu

Asanteni sana wapendwa nitafikisha michango yenu na nitawapa feedback
wknd njema na mbarikiwe sana
 
kheee, yaani hajawahi kupendana na mwanamke kiasi hicho anachopendana na huyo,,du ina maana wewe na yeye ilikuwa tu, MRADI KUNAKUCHA!!ingelikuwa mimi huyo namkalisha kitako, namuaga tu, mbele ya mashahidi hata 2 wanatosha.Mana kitendo cha kusema hajawahi kupendana na mwanamke mwingine namna ile, basi tayari kingelinifukuza hapo ndani.Tena anaongea na uncle wake, hapana ningeondoka.Sijui wewe, labda kama unataka ujaribu kufight for hiyo ndoa yako, na sijui utaanza kufight kwenye angle gani, wakati mtu ameshaanza kudiscuss na mjomba, Dada ondoka tuu
 
Kama ninaishi na mtu kwa sababu nampenda, na moyoni nikiamini na yeye ananipenda, navumilia mapito ya hapa na pale nikiamini ananipenda, Siku nikisikia sikupendi inatoka mdomoni mwake mara mbili tatu. Naondoka kwa Amani kwa gharama yoyote. Unakaa je na mtu hakupendi sasa, akiwa mama au baba ako utasema hatamsiponipenda mi ni mtoto wenu. Sasa mi nakaa na wewe kwa sababu ulinambia unanipenda leo unasema hunipendi halafu nakaa tu nasubiri nini sasa.

Hapa nahisi hata maombi yatafuata huko huko mbele ya safari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom