Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,797
- 1,567
Michango yetu ni msaada mkubwa!Habari zenu, Wiki kadhaa zilizopita nilirudi nyumbani kumkuta mume wangu na mjomba wake wakiwa wanazungumza.Nilitulia sehemu nikawasikiliza kiasi,nilichanganyikiwa.Nikaondoka, badae nikarudi nikajikausha kama hamna nilichosikia.Mume wangu alikuwa anamueleza mjomba wake mpango wa kuoa tena, na mjomba wake alikuwa akimsupport.Sisi wakristo,tulifunga ndoa ya kanisani.Mume wangu alisisitiza kuwa itabidi amuoe huyo mwanamke maana anampenda sana, na mwanamke amesema bila ndoa yeye anataka waachane,hawezi kukubali kuwa hawara.Nanukuu "Hata hivyo sijapata kukutana na mwanamke tukapendana naye kama yule".Maneno haya yanatoka kwenye kinywa cha mume wangu wa ndoa,na baba wa mtoto wangu.Kwa ufupi plan ilikuwa inapangwa namna ya kufanya hili jambo kwa utulivu na makini.Naomba ushauri, mana sijui pa kuanzia, kumbuka haya mambo alikuwa anayaongea na mjomba wake,na mjomba aliongea kama mtu anayemjua kabisa huyo mwanamke anayeongelewa.