Msaidie Mdogo wetu Tafadhari

lumange

Member
Jul 6, 2011
14
1
Habari zenu wana jamii forum,
Mimi nimetumwa kwa niaba ya familia yetu nijiunge humu ili kunusuru ndugu yetu aliye katika hatari ya kupoteza maisha.
Mkasa wenyewe uko hivi;
Tuna mdogo wetu aliyevushwa na Dada mmoja kwenda Kenya kumfanyia kazi za ndani. Baada ya kufika huko wakakorofishana na huyo Dada akamfukuza huyo ndugu yetu bila kumpa nauli ya kurudi huku Tanzania.
Sisi kama ndugu tumejaribu kufuatiria kwa jamaa yake na huyu Dada anayeishi hapa Dar es salaam, lakini akatukatisha tamaa kwa kutuambia kuwa huyo Dada anamdharau sana hawezi kumwambia kitu akafanya, hivyo tutafute namna nyingine ya kumsaidia mdogo wetu.
Tukaona kupitia hapa pengine tunaweza kupata msaada, kwa kuomba mwenye uwezo wa kutuelekeza tunaweza kuchukua hatua gani ukizingatia kuwa sisi hatuna uwezo wa kufika Kenya kutokana na hali ya kiuchumi kuwa si nzuri. Je kuna hatua gani za kisheria zinaweza kutusaidia?
Ahsante kwa kusoma ombi letu.
 
Naomba unipe namba za huyo dada yako ili niweze kuwasiliana naye. unaweza kuni PM ili nimwongeleshe nijue ntamsaidia aje, nipo Kenya na najua naweza kumtoa alipo na kumrudisha nyumbani salama
 
Ahsante kwa kujitokeza kutusaidia

Mdogo wetu hana simu ila huyo Dada aliyempeleka huko anazo simu ngoja nikamuombe huyu jamaa yake wa Dar akinipa nitaziweka hapa kwenye maelezo yangu.
Ahsante tena sana kwa moyo wako mwema.
 
Ahsante kwa kujitokeza kutusaidia

Mdogo wetu hana simu ila huyo Dada aliyempeleka huko anazo simu ngoja nikamuombe huyu jamaa yake wa Dar akinipa nitaziweka hapa kwenye maelezo yangu.
Ahsante tena sana kwa moyo wako mwema.



Vipi jamani huyo mdogo wenu alipatikana au mmekosa msaada? tuwasiliane nitaangalia cha kufanya
 
Yawezekana keshampata ndugu yake lakini inabidia ajulishe jf basi
 
Jamani sijampata ndugu yetu na wala sio kwamba nimeleta mada nikakimbia tatizo sina uwezo wa kuingia kwenye net cafe kila mara, pesa sina. Nilifuatilia kwa yule Baba kumuomba simu ya mwanamke wake akakataa kunipa ila nilipomwambia kuwa nimepata ushauri kupitia jamii forum akasema hata huyo mkewe ni mwanachama wa jamii forum tena mzuri sana!

Kama ananisoma humu na yuko huko kenya tunamuomba aturudishie mdogo wetu kwa wema tu, wala sisi hatuna nguvu ya kifedha kupambana naye ni masikini sisi vinginevyo mdogo wetu asingekuwa mfanyakazi wake wa ndani kama tungalikuwa na uwezo.
 
Naomba siku nyingine usipitie hapa. Nenda polisi maramoja, hiyo inaanza kuchukua taswira ya jinai. Mshitakini huyo anayejiita ndugu yake wa hapa. NARUDIA: NENDA POLISI NI SWALA KUBWA!
 
Naomba siku nyingine usipitie hapa. Nenda polisi maramoja, hiyo inaanza kuchukua taswira ya jinai. Mshitakini huyo anayejiita ndugu yake wa hapa. NARUDIA: NENDA POLISI NI SWALA KUBWA!

Mbona unamkatisha tamaa, nadhani huko Polisi atakuwa amekosa msaada ndio maana kaja jf, si unajua Polisi wetu bila pesa mambo hayaendi?! hasa pale unayeshindana naye kama anakuzidi mshiko!

Cha msingi kama anasema huyo mhusika anasoma hii jf amsikilize kilio chake awarudishie huyo ndugu yao na au atutajie humu jina la huyo dada tusaidie kumueleza humu jamvini.
 
Back
Top Bottom