Msafara wa Rais wasababisha ajali - Visiga.

Huyu Baba kwa Mikosi, hadi 2015 sijui Mangap yatakuwa yeshetokea, Eee Mola Tuepushie Kikombe hiki
 
Katika ajali ya basi la Abood iliyotokea Visiga Kibaha Pwani saa 11 jioni siku ya Ijumaa,watu 15 walifariki. Ingawa ilifanywa siri,taarifa rasmi zilizothibitishwa na Wakuu wa Hospitali Teule ya Tumbi,zinasema kuwa waliopoteza maisha ni 15. Kati yao 7 ni wanawake na 8 ni wanaume. Tukio zima lilifanywa siri kuu kwakuwa lilisababishwa na uzembe wa msafara wa Rais. It was not fair...
 
Sasa hapo nani katambika JK au Abood?kweli nilisikia watu 15 walifariki dunia!
 
Tutasema kila kitu, lakini ukweli ni kwamba kipande cha barabara kati ya Mlandizi na Chalinze ni kibaya mno (at least ni experience niliyopata majuzi). Kuna lami inayojikusanya na kutengeneza matuta katikati na pembezoni mwa barabara. Uendeshaji ni mgumu sana kipande hiki (hata kama ni mzoefu unaweza kusababishiwa ajali kirahisi tu). Naamini hiki ni chanzo cha ajali mf. ya Regia, ya mlinzi ya Salma, etc.
 
hata wafiche Je na kwa Mungu watajificha??? ukweli utabaki pale pale na kila mwenye haki atasimama kwenye haki yake
 
IT IS HAPPENING NOW;Msafara wa Rais JK amesababisha ajali mbaya sana mitaa ya Visiga - Pwani wakati Bus la Aboud likijitahidi kuupisha na kutumbukia mtaroni. Mh Rais alikuwa anakwenda Msoga (home) kwake ! Majeruhi wapo na wanaendelea kutolewa kwenye Bus na Escort moja ya FFU imebaki kusaidia zoezi la uokozi.My Take;Kwanini asiwe anatumia Helkopta ya Polisi ili kuzuia ajali hizi ambazo zinazuilika na kuondoa foleni mjini hasa Dar es Salaam muda anaojiandaa kuondoka ?Source; Radio Imaan=====================================UPDATE==============================================
Kwenye helikopta atacheka na nani?
 
Tutamalizwa kwa ajali, risasi. kubambikiwa kesi nk. Lakini Mungu yupo. Iko siku haya yote yatakoma na OLE WAO
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom