Msafara wa mh. Nahodha Wapigwa Mawe Tunduma-Mbeya

Safi sana wana-mbeya keki ya taifa tule wote na si wao,na niliambiwa kwamba magari ya serikali mwisho saa 9 kutembea.
 
Hiyo sawa kabisa kwann magari ya serikali yatumike kwa shughuli za chama? Hakika state-party fusion haitakufa bora wananchi wamejionea wanyewe. Wadau mkipata wasaa pitieni makala ya nguli wa mambo ya siasa wa udsm Dr. Makulilo katika utafiti wake Tanzania: a de facto one party state?. Nawasilisha
 
Safi sana wana Tunduma, wadau nisionekane mchochezi hapa, kwa kweli haingii akilini waziri kutumia gari la serikali kwa shughuli za chama. Mungu wabariki wana mbeya wote.
 
Naodha anatoa amri washughulikiwe,anawachokoza mwenyewe watu wa Mbeya,alafu baadae waanze kumsumbua Sugu.
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, msafara wa waziri wa mambo ya ndani mh. Nahodha umepigwa mawe na vijana wa huko tunduma. Kisa ni kwamba vijana hawakufuruhishwa na kitendo cha kumuona waziri akitumia magari ya serikali akiwa katika shughuli za kuimarisha chama chake huko Mbeya. Vijana wanahoji kwa nini rasimali hizo zisitumike kusaidia wananchi wengine kama vile wagonjwa walioko hospitalini? Hivi ndivyo nchi yetu inavyokwenda kwa sasa.

Source: Mwananchi
Kwa sababu hii nina waunhga mkono vija wa mbeya kwa 100%....na wengine tuunge mkono sikwa mawaziri tu bali zoezi liendele kwa wote wanaotumia mali za serikali vibaya...
 
Naodha anatoa amri washughulikiwe,anawachokoza mwenyewe watu wa Mbeya,alafu baadae waanze kumsumbua Sugu.
Kama boss wake alitandikwa na hakutoa amri hiyo yeye ndiyo atawaweza ana anadhani ni wa-znz...
 
Ni wana-ccm wachache sana wanaokubalika Mbeya kwa sasa, hasa baada ya saga ya Mwakyembe na afya yake. Sijui kama Mh Nahodha anafahamu hili. Pia kitendo cha waziri kusema watu washughulikiwe ni uchokozi. Waziri anakumbuka fujo za mwaka jana? sio polisi, JKT au JWTZ waliweza kuwatuliza. Kama hakutokeza Sugu leo hii tungekuwa tunaongelea mambo mengine.

aliendaje bila kuomba kibali toka kwa Rais wa Mbeya?pia aelewe kule si pa kuchezea na wasubiri afya ya aumwae itetereke, yatawapata makubwa zaidi.
 
Safi sana wana Tunduma, wadau nisionekane mchochezi hapa, kwa kweli haingii akilini waziri kutumia gari la serikali kwa shughuli za chama. Mungu wabariki wana mbeya wote.
Kama kusapoti mambo yaliyo fanywa na wana Tunduma ni kuchochea acha tuitwe wachochezi maana siwezi kufumba macho kwa jambo jema kama hili.....
 
Kule dar ujuaji mwingi kuna jukumu la kuwakomboa hao watu
Yaani pale dar wanatakiwa makamanda kama Lema, Tindu Lissu, Wenje, Sugu, nk waweke kambi kuamcha vijana mimi naona bado wamelala kama wangekuwa wameamka kama mbeya au Arusha sijui hali ingekuwaje pale magogoni.............
 
Kumekucha Tanzania-mikoani. Dar es laaam sijui kula matende na halua ndio kunafanya vijana kuwa legelege?

Dar es salaam ni mji wa maneno mengi mengi hakuna vitendo mkuu,kwani wdewe haujuhi ilo?bora hata Mwanza wanaelewa wanachohitaji japo walikuaga wapole sana lakini sasa hawataki ujinga tena....Dar baaaado sana tu hata Moro nahisi kuna afadhali kwa sasa
 
Yule waziri aliyesema watu wa mara sio watz tutamsikia sasa hivi akisema watu wa mbeya sio watz halafu mwisho wa siku atakujajikuta kuwa mafisadi yeye na familia yake tu ndio watz
 
Nyinyi mnafurahia watu kurusha mawe akili zenu kidogo zina mafuta ya taa mawe hayabadilishi madaraka pakichukuliwa hatua za kisheria hakika nyinyi ndio mwanzo kusema serekali inaonea raia zake la muhimu ukifika uchaguzi watu wende kwa wingi kupiga kura na kuleta mageuzi sio mawe wala maandamano ya sio kuwa na tija
 
Mbeya itakuwa kitovu cha mabadiliko Tanzania ni mkoa ambao watu wanajua haki zao kuliko mkoa wowote.Hongera wana-mbeya mapambano dhidi ya mafisadi yaendelee.

Pamoja tutashinda
 
Nyinyi mnafurahia watu kurusha mawe akili zenu kidogo zina mafuta ya taa mawe hayabadilishi madaraka pakichukuliwa hatua za kisheria hakika nyinyi ndio mwanzo kusema serekali inaonea raia zake la muhimu ukifika uchaguzi watu wende kwa wingi kupiga kura na kuleta mageuzi sio mawe wala maandamano ya sio kuwa na tija

Kwenye thread hii mchango wako hauna tofauti na wasira katika picha hapo.
 
Naodha anatoa amri washughulikiwe,anawachokoza mwenyewe watu wa Mbeya,alafu baadae waanze kumsumbua Sugu.
kwa hiyo yeye yuko juu ya sheria?aache jazba zake zisizo na msingi,wananchi wamefikisha ujumbe stahiki,utatumiaje rasilimali za nchi au fedha za walipa kodi kwa manufaa ya chama chako?waangalie haya mambo yasije kugeukia kwao huko mbeleni
 
Back
Top Bottom